Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,943
- 18,665
Wakuu nimeanza kujiuliza hili swali hivi punde, "Je waliotumbuliwa na Magufuli wamefikishwa mahakamani?"
Toka Raisi J.P. Magufuli ameingia madarakani kumekuwa na utitili wa viongozi serikalini kutumbuliwa. Ila hatusikii nini hatima ya hao viongozi waliotumbuliwa wamechukuliwa hatua gani.
Hata kama wamefikishwa mahakamani sijui kesi zao zinatumia muda mrefu kiasi gani mpaka hukumu kutolewa.
Tumejionea wale waliotoa maneno ya kashfa kwenye mitandao ya kijamii kwa J. Pombe wakihukumiwa tena mapema sana. Ila cha kushangaza wahujumu uchumi mpaka sasa hakuna ambaye kaisha chukuliwa hatua zaidi ya kutumbuliwa publically.
Je, Hii inamaanisha kosa la kutoa kashfa kwa Rais lina uzito zaidi ya wale wanao hujumu uchumi ?
Mimi nilitegemea Watumbuliwaji wangehukumiwa mapema sana maana tuliaminishwa Magufuli yupo tofauti na utawala uliopita lakini kumbe kwenye suala la ufisadi bado ana kigugumizi.
Hizi nguvu nyingi zinazotumika kusaka wanaofanya makosa ya kimtandao na kuziba midomo ya wapinzani zingetumika kusaka na kuhukumu wahujumu uchumi Tanzania ingekuwa at least one step ahead.
Nahitimisha kwa kusema: " Ninahamu ya kuona yule fisadi kuu tuliyeambiwa na Nape juzi akifikishwa mahakamani pia".