Waliotimuliwa Chadema waomba huruma ya korti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliotimuliwa Chadema waomba huruma ya korti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jan 11, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mussa Juma, Arusha
  MADIWANI watano wa Jiji la Arusha waliotimuliwa uanachama na Chadema, wameomba Mahakama Kuu kuwarejesha kutumikia nafasi zao wakati wakisubiri uamuzi ya kesi ya msingi kupinga kufukuzwa kwao.


  Katibu wa madiwani hao, John Bayo, alisema waliwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu jana, ili wananchi waliochagua waendelee kupata haki yao ya kuwakilishwa.


  “Katika maombi yetu tunaomba Mahakama Kuu, iturejeshe kutumikia wananchi wakati kesi ya msingi ikiendelea, kwani wananchi tunaowakilisha wanakosa uwakilishi kwenye baraza la madiwani,” alisema Bayo.


  Bayo alisema kesi hiyo inatarajiwa kutajwa Januari 19, mbele ya Jaji Fatuma Massengi na tayari walalamikiwa wamepewa hati ya kuitwa mahakamani.


  “Kama unavyoona muda huu natoka kuwapelekea walalamikiwa ambao ni Chadema na (Freeman) Mbowe, hati ya kuitwa Mahakama Kuu Januari 19 na tumempa nakala Kaimu Mkurugenzi wa Jiji,” alisema Bayo.


  Aliongeza kuwa wanaamini mahakama itawarejeshea udiwani wao wakati shauri lao likisikilizwa, kwani ni haki yao kuendelea na majukumu ya kusaidia wapiga kura wao.


  Madiwani wengine waliofukuzwa na kata kwenye mabano, ni aliyekuwa Naibu Meya, Estomih Mallah (Kimandolu) Charles Mpanda (Kaloleni), Reuben Ngoi (Themi) na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Mohamed.


  Kufukuzwa kwa madiwani hao, kulitokana na kukaidi agizo la kamati kuu ya chama hicho, kuwataka kujiondoa katika mwafaka wa uchaguzi wa Meya wa Arusha na madiwani wa CCM na kuomba radhi kwa kuingia mwafaka bila ridhaa ya chama.


  Hata hivyo, madiwani hao waligoma kujiondoa katika mwafaka na kuomba radhi, wakisisitiza kumtambua Meya wa CCM, Gaudence Lyimo na kufikia uamuzi wa kugawana nyadhifa mbalimbali ni halali.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  #1 rutashubanyuma 2012-01-11 08:30
  ninaamini wanahoja ya kimsingi kabisa.........waendelee kutumikia wananchi hususani vyama vya siasa havina demokrasia........iwaje diwani awasikilize makao makuu ambao hata hawakumchagua..........
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Njaa inawatesa, na hapo wanapigia mahesabu posho za vikao ambavyo so far wanavikosa!
   
 4. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hawa wa ajabu kweli,yani mpaka leo bado wana matumaini ya kuwa wana CDM? Pambafu zao waende wakale jeuri yao sasa
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Kila Mtanzania ana haki yake kwenye nchi yake...hakuna cha kuomba huruma mahakamani wamekwenda kutafuta haki yao ya kikatiba kama Watanzania..

  Na wataipata haki yao na kurudi kwenye nafasi zao walizochaguliwa na wananchi.
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Sijapata kuona majitu majinga kama hawa Madiwani, wanasingizia kuwatumikia wananchi, kumbe wanataka kutumikia matumbo yao!
  Na kama lengo lao ni kuwatumikia wananchi kwani ni lazima iwe ndani ya vikao vya halmashauri? Shenzi yao!
  Nitamshangaa sana hakimu katika hili!
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Wanatafuta haki ya matumbo yao!
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Hizo sio sababu za kwenda mahakamani hizi ni sababu zako binafsi.

  Jamaa wamekwenda mahakamani kutafuta haki yao walichaguliwa na wana Arusha sio Makao Makuu ya Chadema.
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ama kweli JF kuna Kenge na mamba watoto
   
 10. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wachumia tumbo hawa hawana lolote,wala hawana hoja ya msingi,kama ni hoja ya msingi basi ni kwa ajili ya matumbo yao na wala si kwa ajili ya wananchi wa Arusha,na hata wakirudishwa na mahakama kuu,pindi uchaguzi utakapotokea wasahau kura zetu kabisa,hata kama watarudi kugombea kupitia Cdm,wana Arusha hatutaki watu wenye ubinafsi na uchu wa wazi,watafute mikoa mingine ya kuwarubuni na si Arusha
   
 11. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sheria iko wazi,hakuna haja ya kuumiza kichwa,wanawakilisha wana Arusha kupitia chama gani kama sio wanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa?kesi yao haina merrit,these guys are fighting a loosing battle,labda sheria ibadilike leo
   
 12. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Njaa inauma mkuu,lawama kutoka mpaka kwenye family sasa kwa maamuzi ya kung'ang'ania kumtambua meya wa Arusha!
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0

  Nyamburi.

  Punguza jazba, subiri sheria ichukue mkondo wake.

  Kinachonifurahisha hawa jamaa hawashindi kwenye ukumbi wa habari maelezo kama anavyofanya hamad rashid.
   
 14. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Utamtukanaje mkunga wakati bado unazaa?hawa ni wehu,ndo wanashtuka sa hivi kwamba wanataka kuwatumikia wananchi?damn!njaa imewakamata kisawasawa!na waondoe imani ya kurudi cdm,kama wanataka kuwatumikia wananchi basi wasubirie uchaguzi then wagombee na chama kilichawahonga!wakichaguliwa basi ndo watumikie wananchi maana bado wanawahitaji!la sivyo wakapige debe stand.
   
 15. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  hawa wamefungiwa duniani na Mbinguni. walipewa karibia mwezi kuomba msamaha wakaleta jauri. kuomba msaha ina maana kubwa sana. unaweza kupoteza udiwani, ubunge, uenyekiti, mchumba kwa kushindwa kuomba msamaha. bora ujifanye mjinga siku ipite. Mia
   
 16. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkut naona mapovu bado yanakutoka kwa kuwatetea hawa jamaa. Kama unafahamu vizuri sheguzi huna sababu ya kuumiza kichwa namna hiyo. Kiongozi yeyote wa kisiasa anadhaminiwa na chama. Kwahiyo chama kikiondoa udhamini wake wanapoteza uongozi kupitia chama hicho. Mbona ni raisi sana kuelewa, hata kama umesoma shule ya kata!? Mahakama haiwezi kuwarudisha kwenye nafasi walizokuwanazo maana itakuwa inakiuka sheria za uchaguzi
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Waombe msamaha kwa kosa gani waliofanya?
   
 18. k

  kiche JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni bora tukawa makini na tunachozungumza,tukumbuke kuwa katiba hiyo ndiyo inawanyima haki!!!,kwenda mahakamani ni suala lingine na kufanikiwa madai yao ni suala jingine,Hakimu anaweza kusema kwenye hukumu kuwa kifungu hiki kinamnyima mtu haki lakini hawezi kusema kuwa hao madiwani warudi!wanaweza kurudi kama mchakato wa kuwaondoa ulikuwa na mizengwe na haukufuata katiba ya chama chao,hapa tunapigana na upepo!tatizo ni katiba na wenye uwezo wa kurekebisha kifungu hiki ni bunge na si mahakama,mahakama inaweza kuonyesha udhaifu unaopatikana kwenye hii katiba yetu,hii ndiyo sheria labda tu siasa iingie kwenye hukumu kama ilivyokuwa kwenye suala la mgombea binafsi!!!!!
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Heri ya kubaka kuliko kuwasaliti wapiga kura wako!
   
 20. MUIKOMA

  MUIKOMA Member

  #20
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama avatar yako inamaanisha sura yako basi watanzania bado tuna kazi ngumu ya kuelimishana laa sivyo tutazidi
  kuchaguana kwa kutizama sura tu. Hapo kwenye bolded red unamaanisha nini?. Kwani katiba yetu inasemaje kuhusu kiongozi
  wa kisiasa anayevuliwa uanachama wake? Au mimi ndo sielewi? Ninachofahamu mimi ni kwamba suala hilo likitokea kiongozi huyo anakuwa amepoteza sifa ya kuwaongoza watu wake kwa mujibu wa katiba ya sasa that why hata mahakama kuu inazidi kuwa na kigugumizi juu ya hili. Dawani katiba mpya itakayotambua nafasi ya mgombea binafsi
   
Loading...