Waliotembelea Hillbrow Johannesburg tukutane hapa

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
18,878
Reaction score
29,388
Screenshot_20250418_085506_Facebook.jpg

Hillbrow ni moja ya maeneo ambayo yamekuwa na mabadiliko makubwa tangu miaka ya 1980 hadi sasa. Katika kipindi hicho, eneo hilo lilijulikana kwa kuwa na maisha ya jiji yenye msisimko, majengo marefu, na jamii tofauti. Hata hivyo, kama katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuongezeka kwa biashara haramu kama vile biashara ya dawa za kulevya, mauaji, silaha, na ukahaba.

Biashara hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa katika hali ya usalama na utulivu katika eneo hilo. Dawa za kulevya zimekuwa zikiingizwa na kusambazwa kwa wingi, zikihusishwa na matatizo ya kijamii na uchumi. Mauaji na uhalifu umekuwa ni tatizo sugu, ukikosesha amani wakazi wengi wa Hillbrow. Aidha, biashara ya silaha na ukahaba pia imeshindwa kudhibitiwa, na kuleta changamoto zaidi kwa mamlaka za usalama.

UJUMBE:
Leta uzoefu wako kwa ulichokiona mwaka ulioenda Hillbrow ndani ya Joburg CBD
 
Ushawahi kwenda ORANIA wewe?
Orania sijafika kwa vile siyo rahisi kufika.
Orania ni mji mdogo ulioko Kaskazini wa Cape nchini Afrika Kusini. Ni wa kipekee kwa kuwa ni jamii inayozungumza Ki-Afrikaner na ilianzishwa mnamo mwaka 1991. Mji huu ulianzishwa kwa misingi ya kibaguzi kwa vile wanayo mpaka sarafu yao ya kutumia ukiwa ndani ya Orania
 
Highbrow,Yeoville,Soweto,Tembisa,Mamelodi,Alexander haya ni maeneo hatari sana kuishi au kupita tu sio sehemu salama sana hata kipindi hiki ila miezi hii miwili nimepita sana Yeoville ili nifike Pritchard Street ni rahisi kwa hiyo route kama haujapita free way ukitokea Woodmed kufika commissioner Street au End Street.
 
Huwa sitaki mazoea na Joburg kabisa, huwa ni pass ndefu Tu naelekea Capetown hapo jozi sitaki hata kulala
 
Nikiwa mdogo nilikua naona kila anaerudi kutoka SA kutafuta maisha anarudi akiwa teja
 
Mwaka 1999 nilisafiri ndege moja na Kamishna wa Polisi aliyekuwa anakwenda kuhudhuria mkutano wa kudhibiti jinai katika eneo la SADC.

Alipoteremka na ndege pale Oliver Tambo mara akachukua taxi halafu akaenda bureaux de Change. Baada ya kubadili dollars zake wakaanza kuelekea hotelini kwake Protea. Dreva akawa anaongea na simu kizulu ambacho Kamishna hakukielewa.

Walipfika tu reception ya hoteli, mara wakavamiwa na majmbazi wakiwanna bunduki. Wakawa search kila kitu Taxi driver, Kamishna wa Polisi na ma receptionist wa Protea. Ila ilikuja gundulika kuwa wale majambazi ndiyo waliokuwa wanaongea kuzulu na taxi driver. Kwa kuficha aibu kwa Serikali na Protea hotel, Kamishna alifidiwa hela zake zilizochukuliwa
Highbrow,Yeoville,Soweto,Tembisa,Mamelodi,Alexander haya ni maeneo hatari sana kuishi au kupita tu sio sehemu salama sana hata kipindi hiki ila miezi hii miwili nimepita sana Yeoville ili nifike Pritchard Street ni rahisi kwa hiyo route kama haujapita free way ukitokea Woodmed kufika commissioner Street au End Street.
 
View attachment 3308224

Hillbrow ni moja ya maeneo ambayo yamekuwa na mabadiliko makubwa tangu miaka ya 1980 hadi sasa. Katika kipindi hicho, eneo hilo lilijulikana kwa kuwa na maisha ya jiji yenye msisimko, majengo marefu, na jamii tofauti. Hata hivyo, kama katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuongezeka kwa biashara haramu kama vile biashara ya dawa za kulevya, mauaji, silaha, na ukahaba.

Biashara hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa katika hali ya usalama na utulivu katika eneo hilo. Dawa za kulevya zimekuwa zikiingizwa na kusambazwa kwa wingi, zikihusishwa na matatizo ya kijamii na uchumi. Mauaji na uhalifu umekuwa ni tatizo sugu, ukikosesha amani wakazi wengi wa Hillbrow. Aidha, biashara ya silaha na ukahaba pia imeshindwa kudhibitiwa, na kuleta changamoto zaidi kwa mamlaka za usalama.

UJUMBE:
Leta uzoefu wako kwa ulichokiona mwaka ulioenda Hillbrow ndani ya Joburg CBD
Mmmmh.......!!!
 
Mkuu mi mwisho Kigoma mwisho wa reli. Hiyo passport niliomba ni kama naenda mbinguni nikasema isiwe tabu
 
Daa aibu kwa Govt...na waliopanga tukio zima na aliompokea...
 
View attachment 3308224

Hillbrow ni moja ya maeneo ambayo yamekuwa na mabadiliko makubwa tangu miaka ya 1980 hadi sasa. Katika kipindi hicho, eneo hilo lilijulikana kwa kuwa na maisha ya jiji yenye msisimko, majengo marefu, na jamii tofauti. Hata hivyo, kama katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuongezeka kwa biashara haramu kama vile biashara ya dawa za kulevya, mauaji, silaha, na ukahaba.

Biashara hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa katika hali ya usalama na utulivu katika eneo hilo. Dawa za kulevya zimekuwa zikiingizwa na kusambazwa kwa wingi, zikihusishwa na matatizo ya kijamii na uchumi. Mauaji na uhalifu umekuwa ni tatizo sugu, ukikosesha amani wakazi wengi wa Hillbrow. Aidha, biashara ya silaha na ukahaba pia imeshindwa kudhibitiwa, na kuleta changamoto zaidi kwa mamlaka za usalama.

UJUMBE:
Leta uzoefu wako kwa ulichokiona mwaka ulioenda Hillbrow ndani ya Joburg CBD
Haya ni matokeo ya kuongozwa na CCM ya Africa Kusini.
 
Mwaka 1999 nilisafiri ndege moja na Kamishna wa Polisi aliyekuwa anakwenda kuhudhuria mkutano wa kudhibiti jinai katika eneo la SADC.

Alipoteremka na ndege pale Oliver Tambo mara akachukua taxi halafu akaenda bureaux de Change. Baada ya kubadili dollars zake wakaanza kuelekea hotelini kwake Protea. Dreva akawa anaongea na simu kizulu ambacho Kamishna hakukielewa.

Walipfika tu reception ya hoteli, mara wakavamiwa na majmbazi wakiwanna bunduki. Wakawa search kila kitu Taxi driver, Kamishna wa Polisi na ma receptionist wa Protea. Ila ilikuja gundulika kuwa wale majambazi ndiyo waliokuwa wanaongea kuzulu na taxi driver. Kwa kuficha aibu kwa Serikali na Protea hotel, Kamishna alifidiwa hela zake zilizochukuliwa
Oliver Tambo walikuwepo polisi wezi wakishirikiana na hao madereva wa Taxi kama unakumbuka kulikua na hao polisi kabla hamjatoka airport wanaanza kuserch magari na walikua wanapata tip kutoka kwa madereva wa taxi wakigundua mtu ana hela wanaita kikosi kingine kuwafuatilia mpaka mtakapofika na hiyo Protea ni ya East gate mpaka wale wahudumu walikua wanahusika maana kwenye mgao wanawekwa ila baadae baada ya kugundulika huo mchezo wao wamekufa wengi sana sasa hivi hakuna hiyo mambo ya kutokea airport wengi wanatumia tren au private car na wengi ni wenyeji michezo kama hiyo wanaijua.
 
Naatamani kufika s.a
Kama hujafanikiwa Tanzania na huna professional education ya kufanya mashirika makubwa, usithubutu kwenda South Africa. Majumba na miundombinu ni mizuri lakini watu hasa wazawa ni watoto wa shetani
 
SA kinachosumbua ni vibali vya kuishi na kufanya kazi ila unyama uliopo SA na Tanzania upo hapa tunalia kutekwa kitu ambacho SA hakipo unyama waliofanya wale polisi Mtwara na kesi Yao inaendelea SA polisi watakupokonya hela kukuua mara chache sana SA mgeni unaweza kutibiwa hospital ya Serikali buree na ukaruhusiwa hata mtu akifa mnapewa maiti kitu ambacho Tanzania tutaomba wadau watusaidie ili tupewe maiti..Wazimbabwe na WaMozambique ndio viongozi wa uhalifu SA wazulu na mataifa mengine yapo kwa mbali sana.
 
Back
Top Bottom