Waliotekeleza agizo tata sitashangaa nao wakaadhibiwa katika mazingira tata

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,315
152,113
Siasa za nchi hii tunazijua na pia tabia za wanasiasa wetu nazo tunazijua.

Inahitaji akili kusoma tabia za wanasiasa hawa na ili ubaki salama mambo mengine ni lazima upime kwanza kabla ya kufanya maamuzi maana kuna kuchomekeana ili uharibu wengine waingie / waweke watu wao,n.k na pia kuna kugeukana / kugeukwa baada ya wao(wanasiasa) kusoma upepo.

Kesho na kesho kutwa sitashangaa kusikia kuna watu wanaanza kutuhumiwa kuwa wanatumiwa na wanasiasa ili kumchonganisha mh.fulani na wananchi,n.k.

Sitashangaa pia kelele zikizidi mamlaka husika zikaja na ufafanuzi kwa lengo la kujaribu kuweka mambo sawa

Sitashangaa pia kusikia watu wanaondolewa kwenye nafasi zao kimya kimya na katika mazingira yenye utata.

Time will tell.
 
hahaha yani wewe unataka barabara za BRT ziharibiwe mapema halafu uje hapa kusema zilijengwa chini ya kiwango na hela ilipigwa........
 
Back
Top Bottom