Waliotandikwa viboko Ikulu hawa hapa

Sijui sifa za kiongozi kwa wadanganyiika lakini pengine hiyo much much better inasimamia mtu alopata F na point 24 badala ya 26..
 
halafu baadaye akampa madaraka kwenye serikali!!
 
halafu baadaye akampa madaraka kwenye serikali!!
Kuna mchapo alinipa marehemu Mwabulambo. Siku moja Julius ameenda ziara ya kikazi mkoani na miongoni mwa waliokwenda
kumpokea alikuwa ni Mwabulambo. Akamuuliza " na wewe uko hapa?" Wote wakaangua vicheko. Mwabulambo was funny (rip)
 
Kwako Bluray nakuelewa lakini jua hata mzazi kumchapa mtoto kwa nia nzuri ya kumrudi wengine watasema ni sawa wengine kama huko USA watasema huna haki mzazi mueleze tu zuri na baya yeye ataamua badala ya kumlazimisha kwa kumpa adhabu. Matokeo ya USA tunayajua.

La muhimu hapa ni kujiuliza kwa ujumla JKT ni kitu kizuri (yaani kwa maoni ya wengi siyo ya mtu mmoja, kama wewe pekee utasema ni kitu kibaya na wengi wanafikiri hivyo?). Shuleni masomo ni pamoja na malezi ya tabia na maadili mema. Kama wengi wanasema JKT ni kitu kizuri au hata kuwa si kitu kibaya basi tusimulaumu Nyerere maana alikuwa na anafanya kitu kizuri kwa nia nzuri.

Pia kumbuka ubaya wa tendo uko katika nia ya mtendaji.
 

acha kutudanganya dr kleruu aliuliwa na mkulima wa kawaida tu!tena akiwa nyumbani kwake na baada ya huyo mkulima kumuua dr kleruu alimpakia kwenye land rover akaburuza mwili mpaka kituo cha polisi na kujitaja mwenyewe kuwa amemuua dr kleruu!uliza wanaojua historia ya mji wa iringa watakwambia.
 
By Masatu
Hapana bana, binafsi nimeenda JKT 1990's utawala wa Mkapa. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!





Asante Mkuu (Keil) Uko makini sana nashukuru umeweka Sawa hapo chini....uongo wa masatu umeishia hapo...



 
Nasikiaga hiyo JKT inaongezaga uzalendo eti. Hili huwa lina ukweli wajameni???

Aah wapi! hawa mafisadi wote wanaotusumbua sasa hivi wamepitia JKT. Na kama kuna mtu leo hii anaamini kuwa wanafunzi wakilazimishwa kwenda JKT basi tatizo la ukosefu wa uzalendo litaisha basi atakuwa ana matatizo makubwa sana kwenye uwezo wake wa kufikiri na kutafakari.
 
Hivi mtu aliecharazwa bakora na nyerere anakua amelaniwa au ujumbe gani tunaupata na somo gani? Je,nyerere was an angel?

Kwa inavyoonekana watanzania wengi tunasumbulia na suala la kiitikadi,kila anachofanya wa itikadi/kundi tofauti kiwe kizuri wengine wataona yaleyale, akifanya kitu kibaya wa itikadi/kundi lake utaona kinavyopambwa na wafuasi ili tu kionekane kizuri.

Kitu mhimu ni kupata uhuru wa kufikiri kila mmoja na si kufikiri kwa kupitia mtu fulani
By kilaza fulani.
 
I can equally say ukitaka kufahamu jinsi Mwalimu alivyokuwa dikteta wa one man show aliyeshindwa kuandaa leadership ya kuja kuchukua uongozi baada yake angalia uongozi wote baada yake.

Makosa ya Mwalimu ni kwamba aliondoka madarakani bila ya kutengeneza Taasisi Imara na Huru kimfumo ambazo zingetusaidia kuwadhibiti watawala wahuni na wezi ambao wamejaa ktk utawala wa sasa.
 
nimewasikia majina ya waliotandikwa viboko na mwalimu JKNyerere nao ni wawili mimi ninaowafahamu:-
Samuel Sitta.
Wilfred Mwabulambo.

I STAND TO BE CORRECTED.
 
Wanabodi naomba tu kufahahamishwa mpaka post no 92 kuna wachangiaji ambao kwa kweli ukisoma hoja zao kwa unafurahi lakini jamvini siku hizi hawaonekani apart from Mkandari, Nyani Ngabu, Jasusi and very few others. Nyie wakongwe hawa watu wameenda wapi? i really miss these guys kwenye hoja
 
Hii maneno niliwahi kusikia kitambo kidogo watu walikula viboko kwa kwenda mbele.Niliambiwa Samwel Sitta na Mark Bomani walikuwemo.
Sitta alikuwepo kati ya waliogoma,hizi ni habari za kuaminika;habari za kuaminika pia kuwa yeye alikuwa particularly stubborn. Kwa hiyo kama mtu yoyote alipigwa viboko,labda itakuwa ni Sitta. Lakini hii habari ya viboko bado sijaisikia hata siku moja.
 
Hapana. Mark Bomani hakuwemo. Wakati huo tayari alikuwa Attorney General.
Namfahamu mmoja tu, marehemu Mwabulambo. JKT iliuliwa enzi za Mwinyi.

Marehemu W.James Panjinga Mwabulambo hakucharazwa bakola kwa sababu ya kugomea National service yeye kweli akipata adhabu hiyo lakini kwa kushusha bendera ya muingereza[ Union Jack] wakati wa maanadamano ya wanafunzi kupinga UDI ya Rhodesia!!
 
Hapana bana, binafsi nimeenda JKT 1990's utawala wa Mkapa. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!

Kumbukumbu zangu za uhakika ni kuwa kweli JKT iliuliwa wakati wa Mwinyi maana mimi nilikuwa intake ya Pili kutoenda JKT mwaka Juni 1995 nikiwa Milambo High School. Wa kwanza kutoenda ni intake ya Nehemia Mchechu - Director wa NHC na wenzake kama Myenzi Mkurugenzi wa Haki za Binadamu. Kwa hiyo si wakati wa Utawala wa Mkapa!
 
Dah, kweli kizazi kipya kinajifunza sana kupitia hizi thread za kipindi hicho. Shukrani wanajamvi!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…