waliosoma sengerema sec tukutane hapa

waliosoma sengerema sec tukutane hapa

Mambaenock

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2013
Posts
427
Reaction score
107
Sehisco.jpg

hebu tupia mambo unayoyakumbuka kipindi upo sengerema sec

Sengerema sec.jpg
 
mkuu Nicholaus na we ulikuwa una lala mirambo
me mwenyewe nilifikia apo mirambo kipindi icho naingia five
 
Last edited by a moderator:
Nililala Kimweri, enzi za Headmaster Marwa akituamsha kukimbia Mchakamchaka, akaja field Mwl. John Pombe Magufuli akitukaririsha formula za Kemia na Physics. Migomo ilikuwa kama kawa, tukienda mjini wafanyabiashara wanalazimika kufunga. Nakumbuka walipotufukuza na kutupeleka nyumbani kwa escort.

Nakumbuka samaki wakavu kutoka visiwani na Kaunda na Nyamazugo Road, nawakumbuka walimu wa hesabu Elifuraha, na Mwl. Force (Mwl. wa Physics) Mwisho wa maneno ni mifugo ya shule kitimoto, Cha kusikitisha ni pale jamaa aliyeitwa Edward Nyantogya alivyopotea Bwenini kishirikina tulimatafuta mashambani bila mafanikio kisha kusikia sauti kwenye vyoo ground floor.

Mwisho wa yote ni Mr. Mickenze wa kilimo. Hapo wacha tu, usisahau Kiranja wetu Mkuu Matiku Matare alivyotuongoza kwenye mgomo wa Kihistoria wakati huo huo akiwa ameomba ruhusa kwenda msibani kwao, lakini hakuondoka akaongoza mgomo mpaka kikaeleweka. Alipotajwa kwenye bodi kwamba ni yeye aliyetuongoza alikana vibaya na kuonyesha fomu ya ruhusa akashinda kesi kiaina. Usitukumbushe mambo ya enzi hizo miaka ya 1979 - 1983 ilikuwa balaaaaaaaaaaaaa....
 
Mwl Elibark kwa sasa alikuwa anafundisha St Carol na alijenga nyumba yake mwabaruhi!
 
Mwl Elibark kwa sasa alikuwa anafundisha St Carol na alijenga nyumba yake mwabaruhi!

Yego Magafu za masiku, wewe ulianza lini na kumaliza lini? Jamaa aliyeleta uzi huu amenifurahisha zana. Unamkumbuka jamaa aliyekuwa anaitwa mshenzi mwenyewe? Matiku na Nelson?
 
umenikumbusha mbali sana mdau, Sengerema enzi hizo! tulikuwa na Head Master alikuwa akijiita Master of the Masters, hadi jina lake nishamsahau!
View attachment 140788View attachment 140789
picha za kitambo sana mkuu naona vijana wamependeza na wakawaka kelvin, Faida , Chanai , Marco S Yohana, Salva, George ,Madata wengine nimesahau majina. Ahsante kwa kumbukumbu nzuri
 
picha za kitambo sana mkuu naona vijana wamependeza na wakawaka kelvin, Faida , Chanai , Marco S Yohana, Salva, George ,Madata wengine nimesahau majina. Ahsante kwa kumbukumbu nzuri
Duh, Sesesco nimetoka mwaka 2004. Advance hiyo! Mambo ya mwabaluhi, kupitia chaka ukiwa unaenda zako town, SM na bila kusahau kwenda town kwenye "kikao" kila ijumaa usiku
 
Duh, Sesesco nimetoka mwaka 2004. Advance hiyo! Mambo ya mwabaluhi, kupitia chaka ukiwa unaenda zako town, SM na bila kusahau kwenda town kwenye "kikao" kila ijumaa usiku
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
Duh, Sesesco nimetoka mwaka 2004. Advance hiyo! Mambo ya mwabaluhi, kupitia chaka ukiwa unaenda zako town, SM na bila kusahau kwenda town kwenye "kikao" kila ijumaa usiku
nimetoka advance 2005 hapo, nimekula sana mafuta ya taa kwenye maharage na bondo, uji without sugar
 
nimetoka advance 2005 hapo, nimekula sana mafuta ya taa kwenye maharage na bondo, uji without sugar
Hahahaaaa, hii JF balaa! Unaweza kuta tunafahamiana. Mi nilikuwa PCB, headmaster wetu Mpemba, RIP!
 
Hahahaaaa, hii JF balaa! Unaweza kuta tunafahamiana. Mi nilikuwa PCB, headmaster wetu Mpemba, RIP!
ni kweli chief, Mimi pia nilisoma PCB apumzike kwa amani Mpemba aliondolewa baada ya ule mgomo wa 2003
 
Back
Top Bottom