Walioshinda rufaa vyeti feki

Walioshinda rufaa vyeti feki

Tenths

Senior Member
Joined
Mar 2, 2010
Posts
111
Reaction score
45
Ni takribani wiki tatu sasa tangu katibu mkuu utumishi autangazie umma kuwa watumishi 450 waliokuwa wamekata rufaa wameshinda nà kutakiwa warudishwe kazini. Kwa masikitiko makubwa baadhi ya halmashauri hadi leo tarehe 1/8/2017 hazijawaandia watumishi hao barua za kurudishwa kazini. Ucheleweshwaji huo unazidi kuleta simanzi kubwa kwa waathirika kwani wameshadhalilika vyakutosha lakini baadhi ya maafisa utumishi hawalioni hilo. Kuna wasiwasi huenda hata mshahara wa mwezi wa nane wasiupate. Kutokana na hili msemo wa wahenga usemao mwenye shibe hamjui mwenye njaa unathibitika. Chondechonde Katibu Mkuu Utumishi liangalie hili ili waathirika hawa wapate mshahara wao wa mwezi wa nane na mishahara yao ya nyuma tangu wafukuzwe kazi.
 
Sisi tulishasema; hii serikali ni ya kisanii. Maneno ni mengi kuliko vitendo. Halafu wanafurahi sana wanapowaona raia wakipata taabu kuliko kuwaona wakiwa na ustawi mzuri. Ni serikali ya visasi tu. Mara wakang'oe mchicha shambani kwa Mbowe, mara wakatae kuongeza mishahara ya watumishi, yaani almuradi waone wananchi wakitaabika.
 
mkuu kwani CCM ndio inawalipa? au wanaidau CCM?
Ndy inayo ongoza serikali na kama chama kuna katiba ambyo lazima ifuate na mukulu ndy mweyekiti wa chama lazma ifuate. Fisiemu isipotoka madarakani mambo unayo yaona sasa yataendelea kama kawaida.
 
Dadaangu ni muhanga mpaka anatia huruma kila siku anapiga mizinga tu amegeuka omba omba
 
Ndy inayo ongoza serikali na kama chama kuna katiba ambyo lazima ifuate na mukulu ndy mweyekiti wa chama lazma ifuate. Fisiemu isipotoka madarakani mambo unayo yaona sasa yataendelea kama kawaida.
Haya mambo yanaenda kikanuni na utaratibu. Kila kitu kipo kisheria mkuu
 
MLIVYOAMBIWA MTAISOMA NAMBA MLIJI EXCLUDE AU VIPI?

AU MLIDHANI NAMBA INASOMWA NA WASIO CHAMA TWAWALA PEKEE?

PAMBANENI NA HALI ZENU.
 
mkuu kwani CCM ndio inawalipa? au wanaidau CCM?

Mkuu likiwa jambo lenye mafanikio hilo ni la ccm, ila hili la kuharibu maisha ya watu ndio mnasema sio la ccm!!?
 
Bora sisi tuliojiajiri yan Hata presha sina na Pesa navuna mambo ya kuingia kwenye mfumo wa serikali ni majanga matupu ndo Kama hivi mkiambiwa mjiajiri mnavunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom