Waliopo Mishamo na Katumba ni Wakimbizi au ni Raia wa Tanzania?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Nimeona msimamo wa serikali dhidi ya watu wenye asili ya Burundi wanaoishi Mishamo na Katumba huko Katavi, nimeshtushwa na idadi aliyotaja Mh. Rais ya watu laki moja na sitini kuwa walipewa uraia wa Tanzania na ikanibidi nifuatilie kwenye mitandao kuhusu historia ya hao watu na walipewa lini Uraia.

Kupitia kumbukumbu za UNHCR zinataja kwamba Mh. Kikwete aliwahi kuutangazia umma na Dunia kwamba Tanzania imeamua kuwapa raia wa Burundi laki na sitini Uraia akiwa kwenye kikao cha UN. Lakini nikajiuliza Hawa watu ambao wanatoka kabila la Hutu laki na sitini kupewa Uraia na kuendelea kuishi Mishamo na Katumba siyo njia kweli imetengenezwa ya wao kuwa na utawala wao kuanzia Mbunge Hadi viongozi wengine wa kisiasa?

Kwanini tuliamua kuwapa Uraia watu wengi kiasi hiki na bila kuwachuja? Je Mhe Rais anaposema amesogeza jeshi karibu na eneo wanapoishi tafsiri yake ni kwamba Hawa bado ni raia wa Burundi yaani Wakimbizi au ni Watanzania? Kama Ni Watanzania kwanini wapewe ulinzi maaalumu au tayari wameanza chokochoko?

Serikali ipitie upya maamuzi yake na waombe pia mawazo ya wasomi mbalimbali kuhusu namna ya kuwaondoa hawa watu kutoka wanapoishi na wasambazwe maeneo mengine ya nchi. Kukaa pamoja siyo afya kwa Tanzania wala Burundi kwa sababu Kati ya watu laki moja na sitini watu mia tu wanaweza wakaanzisha vuguvugu na kuivuruga nchi yetu au asili yao.

Tukumbuke nao Ni binadamu na wanapenda kutawala siyo kuendelea kutawaliwa, Wana kiu ya kuwa viongozi na Wana haki ila Tanzania Kwanza.

Ahsante JPM kwa kuona tatizo nadhani ufumbuzi utapatikana bila kuathiri haki zao za kuishi na za kibinadamu.
 
Na Magu amesema watawanyima uraia wa Tz watoto wa hao waliopewa uraia sababu ya tabia za hovyo hovyo za wazazi wao kama vile kuteka magari ya abiria,ujambazi wa kutumia silaha etc maana watoto wao wanaweza pia kua na traits hizo.
 
Na Magu amesema watawanyima uraia wa Tz watoto wa hao waliopewa uraia sababu ya tabia za hovyo hovyo za wazazi wao kama vile kuteka magari ya abiria,ujambazi wa kutumia silaha etc maana watoto wao wanaweza pia kua na traits hizo.
Hawabebeki walipewa hifadhi ila wakuwa vinara kuingiza saraha toka kwao Burundi
Na kukaribisha jamaa zao na kutengeneza mitandao ya kuteka mabasi vuwavamia wenyeji kupola mali
 
Hawabebeki walipewa hifadhi ila wakuwa vinara kuingiza saraha toka kwao Burundi
Na kukaribisha jamaa zao na kutengeneza mitandao ya kuteka mabasi vuwavamia wenyeji kupola mali
Nadhani roho ya utulivu haiko ndani kwao,wao ni vurugu vurugu hata huko Kagera,Kagera jamaa shughuli zao kubwa ni kuteka magari na maduka ya watu.

Sijajua vigezo gani vilitumika kutoa uraia kwa watu 160,000 ni wengi sana aisee na wale jamaa hua wanazaliana sio kitoto unakuta familia 1 ina watoto 8.
 
kwa nini wasitawanywe mikoani?
Hamna haja ya kuwatawanya.Sema tu serikali itangaze kuwa Kuna kabila jipya limeongezeka Tanzania Kama tuna makabila Mfano 120 tutangaziwe Kuna la 121 kabila la wahutu
 
Wahutu hawana shida ni km watu wa kigoma tu
Wastaarabu sana na wengi wamezaliwa Tanzania
Watu hatari kuwapa uraia kwa wingi ni wasomali na watusi hawa huwa hawasahau kwao
Walipewa uraia mwaka 2015 kwa mkakati maalumu, ndiyo maana nafsi zinawasuta kwani haijawashi kutokea mahali popote duniani kutoa uraia kwa wakimbizi 120,000. jambo la msingi serikali iwasambaze sehemu mbalimbali nchini ili wakachangamane na wengine.
 
imebidi nifuatilie hotuba ya jpm huko duuuh jamaa wamefuga majambazi serikali inashindwa nini kuwadhibiti hao wahuni wachache wanaochafua hao wahutu kama miongoni mwao wapo wema?
 
Ukweli ni kwamba, rais Kikwete hakuutangazia umma wa dunia kuwa amewapa uraia hao wakimbizi kwa maana ya kutamka tu. kuna mchakato wa muda mrefu uliohusisha nchi za Burundi na Tanzania pamoja na UN kupitia UNHCR kuanzia mwaka 2007 kuwaandikisha na kisha kuwapa choice.

Waliopenda kurudi Burundi walirudishwa tena wlipelekwa bure na kila mmoja alilipwa kiasi kidogo cha pesa ya kujikimu.

Waliopenda kuwa Watanzania waliukana uraia wa Burundi na kuamua kuwa watanzania. Kwa maana hiyo, hatutegemi hoja ya kutawaliwa iwe na mashiko kwenye suala hili kwa sababu ukiwa umeamua kuwa Mtanzania na unaishi tanzania chini ya utawala wa tanzania, kuna habari gani tena ya kutawaliwa? Na nani?

Kuhusu uhalifu, hilo nadhani ni suala individual na hakuna mantiki ya kulifanya liwe la jamii nzima. Kuna kabila gani tanzania hii haina watu wanaofanya vitendo vya kihalifu.

Mimi naamini kama kuna wahalifu, basi wachukuliwe hatua. jamii isihukumiwe kwa makosa ya baadhi ya wanajamii hadi itakapodhihirika kuwa uhalifu huo unakuwa organised katika level ya jamii, jambo ambalo siamini wanaweza kufanya tena ikizingatiwa ni watu waliopewa uraia miaka kumi tu iliyopita.
 
imebidi nifuatilie hotuba ya jpm huko duuuh jamaa wamefuga majambazi serikali inashindwa nini kuwadhibiti hao wahuni wachache wanaochafua hao wahutu kama miongoni mwao wapo wema?
Siamini kama ni sahihi kusema jamii imewafuga majambazi. Kama kuna wanajamii majambazi hilo linawezekana, lakini utasemaje jamii imewafuga? Kwani majambazi waliopo maeneo mengine ya nchi wamefugwa na akina nani? Nashauri jeshi la polisi lifanye kazi yake kama linavyofanya kazi maeneo mengine ili kuwalinda hao raia wapya dhidi ya majambazi ambao inawezekana ni mchanganyiko wa wanajamii wahalifu pamoja na watanzania asilia wa maeneo ya jirani. Ujambazi huchochewa na tamaa ya fedha na mali, hivyo yeyote anaweza kujiingiza katika uhalifu huo kwa sababu amepata tamaa ya mali. Ujambazi hauwezi kuchanganuliwa kwa misingi ya kijamii kama ilivyo uhalifu wa kisiasa au kiitikadi. Kwa hiyo masuala ya ujambazi na ujangiri sioni kama ni sahihi kuyaambatanisha na jamii nzima.
 
Walipewa uraia mwaka 2015 kwa mkakati maalumu, ndiyo maana nafsi zinawasuta kwani haijawashi kutokea mahali popote duniani kutoa uraia kwa wakimbizi 120,000. jambo la msingi serikali iwasambaze sehemu mbalimbali nchini ili wakachangamane na wengine.
Correction: Walipewa uraia mwaka 2010 na aliyetangaza kwa mara ya kwanza ni Waziri Lawrence Masha. Mchakato huo ulianza mwaka 2007 na kukamilika mwaka 2009. Sasa nimesikia jambo jipya kuwa walipewa uraia kwa mkakati maalum, ningefurahi sana kujua huo mkakati ulihusu nini. Hayo mengne yanatokana na serikali kuchelewesha zoezi la kuweka miundombinu ya kiutawala maeneo hayo kama ilivyo maeneo mengine ya Tanzania. Hoja ya kuwatawanya ilishakuwepo tangu miaka hiyo walipopewa uraia lakini ikafutwa. na kwa kuangalia kwa makini, kuna sababu gani ya kuwatenganisha watu wa jamii na kabila moja? Kuna uovu gani umefanyika huko hadi ifikie hatua hiyo? Kusema wakachanganyikane na wengine si sahihi kwa sababu hata hao wengine walioamua kuchanganyika, wamefanya hivyo kwa hiari yao na kila mara wana mahali wanarudi wanapopaita nyumbani kwao. Wachagga wanakwenda Kilimanjaro, wahaya Kagera, na kadhalika. Hawa wakitawanyika maana yake ni sawa na kusema umeiua jamii hiyo. Mimi naamini hao raia hawawezi kushindikana kama wakiwekewa miundombinu ya kiuongozi.
 
Nadhani roho ya utulivu haiko ndani kwao,wao ni vurugu vurugu hata huko Kagera,Kagera jamaa shughuli zao kubwa ni kuteka magari na maduka ya watu.

Sijajua vigezo gani vilitumika kutoa uraia kwa watu 160,000 ni wengi sana aisee na wale jamaa hua wanazaliana sio kitoto unakuta familia 1 ina watoto 8.
Fuatilia. Serikali za Burundi na tanzania pamoja na umoja wa mataifa ziiamua pamoja. Na kigezo cha kwanza ilikuwa mtu mwenyewe achague kuwa Raia wa Tanzania au arudishwe Burundi. Waliochagua kurudi walisafirishwa hadi kwao na serikali ya huko iliwapokea kwa kushirikiana na UNHCR. Waliochagua kubaki waliingia kwenye mchakato wa maombi yao kufanyiwa kazi. Ninaamini kulikuwa na ufuatiliaji kujua kama mtu ana rekodi ya uhalifu au la kabla ya maombi yake kukubaliwa.

Suala la kuzaliana si la jamii moja. Umeshafuatilia jinsi Wasukuma wanavyozaliana? After all Rais wetu amesema watanzania wazaliane sana ili kuongeza nguvu kazi na soko la bidhaa zetu wenyewe kama wachina.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom