Waliopangiwa UDSM soma hapa itakusaidia

Waliopangiwa UDSM soma hapa itakusaidia

Mstaarabu wa ukwee

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2013
Posts
212
Reaction score
140
Nianze kwa kukupongeza mdogo wangu uliyepata chuo bora kuliko vyote Tanzania.
Naamini ni juhudi zako pamoja na Neema za Mungu upo hapo.
mlimani chuo kizuri sana LAKINI umakini mkubwa sana unahitajika.
Naongelea UDSM maana nami pia nilipata Neema ya kusoma pale na nimemaliza mwaka huu.

Nataka nikwambie bata zipo nyingi sana pale usipokuwa makini zinaweza zikakupotezea malengo yako,wapo tulio anza nao wakadisco kisa uzembe japo ambao sio uzembe ila ugumu wa shule na wingi wa majukumu,binafsi sikupata shida sana maana kuna wanaojitambua walitangulia kupita pale wakanipa shule mapema,na mm leo nataka nikupe na ww ili usijute baada ya hiyo miaka yako 3/4/5.

Shetan anakamata sana vijana wa UDSM wasio na nguvu ya ziada(Nguvu ya Mungu) ktk maisha yao ya chuo. Nakushauri tu ukiamua uchukue au ukiamua uache,ukifika chuo tafuta marafiki ambao watakusaidia na kukushauri mambo mema na kukufanya ufikie malengo yako.

Nilipata bahati ya kuwa member wa fellowship moja inaitwa USCF MLIMANI(Interdenomination-yaani haina dhehebu ila kama unamuamini KRISTO tu) imenisaidia sana,nakushauri ukifika chuo itafute hiyo kama umepangwa Main campus kama upo Mabibo ipo pia inaitwa UD-MCF...ukitaka kuwa salama jiunge na moja wapo ya hizo fellowship.

wanafundisha mambo mengi sana ya kukusaidia maana maisha sio cheti tu.
Baadhi ya vitu unavyoweza kujifunza huko na vikakusaidia ni kama:-

1.Kumjua Mungu kwa undani zaidi na jinsi gani anaweza kukusaidia kwenye shule na maisha kiujumla
2.Mahusiano...uchumba..
3.Ujasiriamali
4.Jinsi gani ya kufanya vizur ktk shule yako.
Vyote hivyo utavipata kupitia semina mbali mbali zinazoandaliwa na hao watu na kufundishwa na watumishi wanaojua kama Joel Nanauka,Sam Sasali,Chris Mauki n.k

Zaidi ya yote utapata nafasi ya kujuana na watu wengi na wengine maarufu Tanzania hii na kama unavyojua watu ni mtaji
Utajifunza pia kukuza kiingeleza chako na kukuza confidence yako ya kuongea mbele ya watu ambayo ni mtaji wako baada ya kumaliza chuo.

BINAFSI YOTE HAYO NIMEYAPATA KUPITIA HIZO FELLOWSHIP NA WALA SITANII
Nina mengi ya kukwambia kuhusu UDSM but leo naishia hapo.
kwa msaada zaidi kuhusu ushauri wowote au kuzijua hizo fellowship zaidi nicheck
0768448747
0673448647
 
Huwezi jisifu kwa kusoma chuo fulani eti kizuri kuliko vyuo vyote TZ kikubwa tunaangalia unafanya nini katika jamii na unapata skills za maisha sio nimesoma UDSM cha kwanza ni kuboresha maisha bila kujali umesomea chuo kipi maana kusema hivi ni sawa na mtu kujisifu baba yangu ni professor wakati yeye kaishia chekechea hii haina maana kujisifia utajiri wa kaka yako wakati we maskini, utakuja jikuta watoto wa nduguyo wanakunyang'anya remote sijui utagombana nao ukisema mali ya kaka wakati wao ya baba yao. Jiimarishe kiuchumi na kiroho sio kujisifu umesomea chuo kipi. Naomba kuwasilisha
 
Ikiwezekana ule utafiti unakuhusu maana huwezi jisifu kwa kusoma chuo fulani eti kizuri kuliko vyuo vyote TZ kikubwa tunaangalia unafanya nini katik jamii na unapata skills za maisha sio nimesoma UDSM cha kwanza ni kuboresha maisha bila kujali umesomea chuo kipi maana kusema hivi ni sawa na mtu kujisifu baba yangu ni professor wakati yeye kaishia chekechea hii haina maana kujisifia utajiri wa kaka yako wakati we maskini, utakuja jikuta watoto wa nduguyo wanakunyang'anya remote sijui utagombana nao ukisema mali ya kaka wakati wao ya baba yao. Jiimarishe kiuchumi na kiroho sio kujisifu umesomea chuo kipi. Naomba kuwasilisha
Ndugu yangu kama ww ni muelewa unaweza ukasoma na kuona content kubwa ya ujumbe wangu sio kujisifia na sikutegemea kama ungepercieve hivyo kama umekwazika nisamehe bure ila hata tafiti zinaonyesha UDSM ni chuo bora Tz sasa sijajua ww umetafsiri vipi!!!!
Kuhusu impact katika jamii hiyo ni habari nyingine maana wasomi wengi wanaajiliwa na wasiosoma so cheti na mafanikio ya mtu ni vitu viwili tofauti ila ubora chuo utabaki pale pale kama UDSM Kuwa chuo bora inakukwaza sijui nitakusaidiaje sasa ila kumbuka tu ukweli utabaki paleplale kwamba sikio na kichwa,kichwa ni kikubwa tu.
 
Kwenye vyuo bora Afrika mbona sijaiona udsm mwaka huu, nimeona Makeree ya NNE na to Nairobi ya nane zaidi yahapo southafrica na egypt.
 
Huwezi jisifu kwa kusoma chuo fulani eti kizuri kuliko vyuo vyote TZ kikubwa tunaangalia unafanya nini katika jamii na unapata skills za maisha sio nimesoma UDSM cha kwanza ni kuboresha maisha bila kujali umesomea chuo kipi maana kusema hivi ni sawa na mtu kujisifu baba yangu ni professor wakati yeye kaishia chekechea hii haina maana kujisifia utajiri wa kaka yako wakati we maskini, utakuja jikuta watoto wa nduguyo wanakunyang'anya remote sijui utagombana nao ukisema mali ya kaka wakati wao ya baba yao. Jiimarishe kiuchumi na kiroho sio kujisifu umesomea chuo kipi. Naomba kuwasilisha


Hupendi mtu ajisifu kwa ukweli Mkuu.
Kila mtu anajisifu kwa mafanikio aliyoyapata. Huyu kapata mafanikio ya kusoma katika chuo bora Tanzania hiyo ilikuwa Episodi ya kwanza, Episodi ya pili ni kutafuta Mali. Sasa unamlaumu mtu kwa kujivunia mafanikio ya mwanzo ilihali ananafasi ya kushinda kwenye Episode ya pili.

Watu bhna.
 
Kwenye vyuo bora Afrika mbona sijaiona udsm mwaka huu, nimeona Makeree ya NNE na to Nairobi ya nane zaidi yahapo southafrica na egypt.
Kama haujakiona ina maana gani kwako..!?
Ni chuo bora Tanzania..!?
Ama sio chuo bora Tanzania..!?
 
Kwa hiyo ni dhambi kukipima kwa muktadha wa kimataifa? Go extra mile and think globly men!
 
Back
Top Bottom