Waliopandikizwa uboho (bone marrow transplant) wafikia 11

sunguramjinga

Senior Member
May 11, 2023
175
227

1683959608097.png

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo ametoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Afya kwa Mwaka 2023/2024 ambapo amesema katika kipindi cha July 2022 hadi March 2023 Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila ilifanikiwa kutoa huduma ya upandikizaji wa uboho (bone marrow transplant) kwa Wagonjwa 11, huduma hii ni mara ya kwanza kufanyika nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Ummy amesema “Gharama za kumpeleka Mgonjwa mmoja nje ya nchi ni shilingi milioni 250 wakati katika Hospitali hii ni shilingi milioni 70 tu, hivyo Hospitali imetumia shillingi milioni 770 na kama wangeenda nje ya nchi, Serikali ingetumia shilingi bilioni 2.75, hivyo jumla ya shilingi bilioni 1.98 zimeweza kuokolewa”

“Ili kuboresha huduma kwa Wagonjwa wenye matatizo ya ubongo na mishipa ya fahamu, Hospitali ya Taifa Muhimbili iliamua kuwahudumia wagonjwa hawa chini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila na kuwapangia kazi Madaktari bingwa na wabobezi wa fani hii, utaratibu huu wa kutoa huduma mahsusi chini ya Hospitali mahsusi na Mabingwa/ Wabobezi mahsusi ni msingi wa dhana ya Vituo vya Umahiri (Centres of Excellence) ambayo ndio dhana tunayoijenga kwa sasa katika utoaji wa huduma za kibingwa na kibobezi hapa nchini”
 
Haya matibabu yatasaidia Sana Kwa watanzania wengi.... Mwaka juzi nilipata shida ya upungufu wa bone marrow kwenye magoti Yale maumivu yalikuwa makali mno
 
Mimi Sina tatizo na Hilo.Ila tatizo langu ni Hawa BAKITA,hivi wanajielewa kweli,wanashindwaje kutafuta jina lingine linaloendana na bone maro,wakaachana na Ubohoo?
Ubooh uheshimiwe
 
Back
Top Bottom