Anko Sam
JF-Expert Member
- Jun 30, 2010
- 3,254
- 907
kuna hoja hawajajibu
1. Thamani ya IPTL ilikuwa milioni 6 za kitanzania? yaani mtambo, ardhi, magari n.k? Kama la usafi wenu uko wapi wakat mmeanza kukwepa kodi mapema kabisa kwenye mauziano.
2. Sheria za kodi kwenye mauziano zilifatwa? TRA kodi imelipwa siku moja baada ya kuwa IPTL ishauzwa. Mlitoa wapi nyaraka za TRA kuidhinisha ununuzi huo? Mfano, hairuhusiwi kuuziana gari na haitakubalika kuhamisha umiliki kama kodi ya motorvehicle haijalipwa yote na mmiliki wa awali. IPTL ilihamishiwa umiliki wakat wanadai kodi.
3. Kwa msingi wa hoja ya pili hapo juu, mbona mlipeleka document fake mahakaman na wizarani kuomba malipo mkijidai zimetoka TRA? Baada ya kufanikiwa nia yenu ovu ya kuhamisha umiliki ndo mkalipa kodi BAADA ya nyie PAP kulipwa pesa za escrow. Sheria ya kodi inasemaje kwa wanaoforge documents?
4. Kama pesa haikuwa ya mlala hoi mtanzania, mbona mnaficha ukweli kuwa pesa iliyokuwa tegeta Escow akaunt ni dola 250 molioni na sio 120 mnayoitangaza kwenye media? Iliyobaki 130 ni ya wabia wa IPTL pia? kama la mbona imebaki kuwa ya umma? Hapa ieleweke kuwa jamaa wamepiga 120 kati ya 250 zilizokuwa Escrow akaunt. Hizo 130 zinabaki kuwa za nani? hazina mwenyewe au nazo mnazirudia?
5. Swali kwa AG, Maswi na mmelipwa ngapi kati ya hizi dola mil. 120 (over 200bn)
6. Swali kwa Maswi. lini utampeleka Kafulila mahakamani? maana alhamis aliongelea hii scandle nje ya bunge, DW Ujeruman.
7. Swali kwa AG. Lini utaomba radhi na kujiuzuru ili kurudisha utu wa Kafulila. Watanzania tunamjua si tumbili nawe unakwepesha hoja ya escrow kwa kumbagua kafulila awe tumbili. Lini utaachia ofisi?
8. Hivi pesa za watu binafsi hufanyiwa auditing na serikali? Pac ilishafanya ukaguzi wa fedha hiz, ilikuaje hapa?
Note: we mtanzania mwanasheria njaa unayeumiza watanzania wenzako kwa kutetea uharamia jitokeze ujibu maswali haya. WE NEED BACK OUR MONEY.
Kwenye point ya kwanza tu, yaani mi umeshanichanganya tayari, huku kwingine ndo ntaelewa kweli?
Mimi nuinachojua ni kwamba sasa hivi CCM wanatafuta hela za kuhonga kwenye uchaguzi mkuu 2015, na ninakubaliana na wale wanaosema, hizo pesa zinazostukiwa ni 10% ya pesa zote za serikali zinazokwapuliwa na maCCM! Nchi imekwisha hii bora tuache kulipa kodi mpaka uchaguzi ujao upite.