Waliomsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955

Siku hizi kuna hizi media za kielektroniki tunasoma sana tu. Si hata wewe umekisoma kisa hiki cha waliomsikiza Nyerere hapo hapo kiganjani mwako?
Hilo sio tatizo tatizo Kuna Aina ya watu hawana uwezo huo wa kusoma katika mitandao na uelewa mdogo wa mambo lakin Yale masimuliz yalifanya watu wawe na morali wa kutafuta story husika

Tatizo usasa mwing Kuna vingne lazima ukose,
 
Wanao soma vitabu n wachache Sana siku hz na zile Baraza za masimuliz hazipo siku hz story nying za viongoz wetu waliopita hazipo Tena kitaaa kuwa na vitabu s tatizo,tatizo Ni wasimuliz wanaongeza chumv na kukupa ushawishi wa kutafuta kitabu husika
Abdi...
Hilo lawezekana lakini baada ya kuandika kitabu hiki historia ya uhuru wa Tanganyika imebadilika walimu vyuoni hawaisomeshi historia hii kama ilivyokuwa ikisomeshwa hapo zamani.

Vyuo vikuu Ulaya na Marekani vivyosomesha historia ya Afrika wanakitumia kitabu hiki kama kitabu cha rejea.

Huu ni karibu mwaka wa 10 hapa JF historia hii inajadiliwa ni kitabu sasa kinakwenda toleo la 4 si kawaida kwa kitabu kuishi umri huu na kikawa bado kiko kwenye mjadala.

Sidhani kama hii historia itakufa kwani mdiyo historia ya taifa letu.
 
Hilo sio tatizo tatizo Kuna Aina ya watu hawana uwezo huo wa kusoma katika mitandao na uelewa mdogo wa mambo lakin Yale masimuliz yalifanya watu wawe na morali wa kutafuta story husika

Tatizo usasa mwing Kuna vingne lazima ukose,
Abdi...
Nadhani unajua kuwa baada ya kitabu hiki kuna miradi miwili ya kuandika historia yetu nilishirikishwa.

Mradi wa kwanza ni wa Oxford University Press, Nairobi (2007) na wa pili ni wa Harvard na Oxford University Press, New York (2011) na kazi zangu mbili zimechapwa.
 
Attachments

  • THE TORCH ON KILIMANJARO.jpg
    THE TORCH ON KILIMANJARO.jpg
    5.5 KB · Views: 2
  • KLEIST SYKES DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY.pdf
    229.2 KB · Views: 1
Abdi...
Hilo lawezekana lakini baada ya kuandika kitabu hiki historia ya uhuru wa Tanganyika imebadilika walimu vyuoni hawaisomeshi historia hii kama ilivyokuwa ikisomeshwa hapo zamani.

Vyuo vikuu Ulaya na Marekani vivyosomesha historia ya Afrika wanakitumia kitabu hiki kama kitabu cha rejea.

Huu ni karibu mwaka wa 10 hapa JF historia hii inajadiliwa ni kitabu sasa kinakwenda toleo la 4 si kawaida kwa kitabu kuishi umri huu na kikawa bado kiko kwenye mjadala.

Sidhani kama hii historia itakufa kwani mdiyo historia ya taifa letu.
Nadhan hatujaelewana bado nacho semea uelewa mpana wa watu,wa Africa weng hawapend kusoma kitu Mpaka wapate kasimuliz kidogo na zaman ilikuwa rahis koz wasimuliz walikuwa weng na ili changia sana kwa maaana mtu alienda tafuta kitabu husika

Kwa kariba ya vijana wa leo Ni ngumu Sana

Na historia ikiwepo bila kusomwa na kuendelezwa Ni sawa sawa imepotea na kukosa Radha yake halisi
 
Hilo sio tatizo tatizo Kuna Aina ya watu hawana uwezo huo wa kusoma katika mitandao na uelewa mdogo wa mambo lakin Yale masimuliz yalifanya watu wawe na morali wa kutafuta story husika

Tatizo usasa mwing Kuna vingne lazima ukose,
Kwa hayo una shauri nini?
 
Nadhan hatujaelewana bado nacho semea uelewa mpana wa watu,wa Africa weng hawapend kusoma kitu Mpaka wapate kasimuliz kidogo na zaman ilikuwa rahis koz wasimuliz walikuwa weng na ili changia sana kwa maaana mtu alienda tafuta kitabu husika

Kwa kariba ya vijana wa leo Ni ngumu Sana

Na historia ikiwepo bila kusomwa na kuendelezwa Ni sawa sawa imepotea na kukosa Radha yake halisi

= ladha

Na wewe sasa unakitoa ladha Kiswahili.
 
Nadhan hatujaelewana bado nacho semea uelewa mpana wa watu,wa Africa weng hawapend kusoma kitu Mpaka wapate kasimuliz kidogo na zaman ilikuwa rahis koz wasimuliz walikuwa weng na ili changia sana kwa maaana mtu alienda tafuta kitabu husika

Kwa kariba ya vijana wa leo Ni ngumu Sana

Na historia ikiwepo bila kusomwa na kuendelezwa Ni sawa sawa imepotea na kukosa Radha yake halisi
Abdi...
Huu mjadala mimi niko hapa karibu mwaka wa 10 watu wananisoma, wanauliza maswali, najibu hadi wewe umenikuta hapa jamvini.

Hili moja.

Pili na ndilo kubwa zaidi ni kuwa historia ya Tanzania imebadilika na haisomeshwi kama zamani ile ya kuanza na kumalizia na Mwalimu Nyerere.

Historia ya Tanzania kama taifa haitoacha kusomeshwa.
 
huu ndio upuuzi ambao hua siupendi yaani mtu na akili yako unawaza udini tu
Bullar,
Wengi hawakuipenda historia ya TANU na uhuru kwa kuwa ilitawaliwa na Waislam.

Lakini tuna hiyari wa hili hivi sasa nao ndiyo ukweli wa historia yenyewe?

Wamejaribu kuufuta ukweli huu matokeo yake leo wengi wanajifunza upya historia ya TANU tena kwa zile ABC zake hatua kwa hatua.
 
Kweli familia ya Sykes unaitukuza. Hivi unajua kuwa Nyerere Aliipoanza kazi Tabora nani alimpokea akaa kwake hadi akamuoa Mama Maria nyumbani kwake? Hizi simulizi zako zimeegemea upande mmoja. Tungependa simulizi neutral
Njinjo,
Hapana sijaegemea upande mmoja hizi simulizi zinztokana na utafiti ambao ulimalizikia kwa kuandika kitabu na nimejitahidi kueleza mengi.

Ikiwa na wewe una taarifa zaidi uhusu historia ya uhuru wa Tanganyika tafadhali tuandikie hapa.

Ila nitakuzindua jambo moja.

Mwalimu alipokuwa Tabora alikuwa bado hajaoa.

Mwalimu kaoa baada ya kutoka masomoni Scotland 1952 na harusi ilikuwa kwao Musoma.

Soma kitabu cha Thomas Molony kitakusaidia kuyajua maisha ya Mwalimu.
 
Attachments

  • THE EARLY YEARS.jpg
    THE EARLY YEARS.jpg
    8.6 KB · Views: 2
Ndinani,
Huyo si Lucy Lameck.

Nimejitahidi kutafuta majina ya hao wanawake wawili bado sijafanikiwa.

Utakataaje kuwa sio Lucy Lameck ili hali humjui ni nani? Mimi nakuhakikishia kuwa ndiye kwani Lucy na Titi Mohamed walikuwa mstali wa mbele kwa mambo ya siasa wakati huo!!! Muulize Juma Mwapachu anaweza kukusaidia kwa hili!!! Pengine hata balozi Paul Rupia anaweza kuwa na msaada hapa.
 
February 1955 TANU Moshi bado haijasimama vizuri kwa ajili ya tatizo la Joseph Kimalando aliyekuwa hataki kufungua tawi la TANU Moshi mjini.

Kipindi hiki ndiyo Mwalimu anakwenda UNO.

Lucy Lameck aliingizwa TANU na Yusuf Olutu baada ya Tawi TANU kufunguliwa.

Hapo ndipo alipochomoza Lucy Lameck.

Lucy Lameck namjua vyema kama niijuavyo historia hii ya TANU.
 
Mwaka 1955 wakati Mwalimu anakwenda U.N.O. Lucy Lameck alishakuwa mwanachama wa TANU na akiishi Dar es Salaam!!! Fortunately, kuna mtu anaweza kutusaidia hapa nae ni Abbas Sykes; yeye nadhani pekee kati ya wazamani aliye hai. Sijui kama una ukaribu nae kama alivyokuwa Ally?
 
Yaani hata wasindikizaji wanaoishia airport wanaanzishiwa uzi?
Faru...
Umekosea kuuliza swali lako.

Ulitakiwa uulize hivi...

Bi. Tatu bint Mzee ni nani katika TANU na ukaendelea hivyo kwa Bi. Chiku bint Said Kisusa hadi ufike mwisho.

Nitakupa kidogo.
Bi. Chiku bint Said Kisusa alikuwa mke wa Shariff Abdallah Attas.

Huyu Shariff Attas alikuwa Collector Kariakoo Market chini ya Abdul Sykes Market Master.
Nyerere kamjua hapo kwa kujulishwa na Abdul Sykes.

Watu siku zile wakiogopa kuwa karibu ya Nyerere wasipoteze kazi zao.

Hawa akina mama ndiyo walikuwa wauza kadi za TANU nyumba kwa nyumba chumba kwa chumba.

Iddi Faiz Mafungo yeye Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na pia Mweka Hazina wa TANU kadi yake ya TANU No. 24.

Yeye ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Mwalimu UNO.
Bi. Tatu bint Mzee alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU.

Umetosheka au bado niendelee kukusomesha historia ya hawa wazalendo?
 
Mwaka 1955 wakati Mwalimu anakwenda U.N.O. Lucy Lameck alishakuwa mwanachama wa TANU na akiishi Dar es Salaam!!! Fortunately, kuna mtu anaweza kutusaidia hapa nae ni Abbas Sykes; yeye nadhani pekee kati ya wazamani aliye hai. Sijui kama una ukaribu nae kama alivyokuwa Ally?
Ndinani,
Historia ya Lucy Lameck nimeipokea kutoka kwa Mzee Yusuf Olotu.
Hebu soma historia ya TANU Moshi hapo chini:

''Wakati sehemu nyingine zikihamasika na harakati za kudai uhuru Moshi ilikuwa katika usingizi. Uongozi wa TANU Arusha, chini ya Japhet Kirilo ulikuja Moshi pamoja na Rajab Chamshama na Robert Otieno kuja kuchunguza kwa nini TANU ilikuwa inachelewa kusajiliwa Moshi.

Viongozi hawa waliitisha mkutano wa uchaguzi Welfare Centre ambao ulihudhuriwa na watu takriban 25, mmoja wao akiwa Yussuf Ngozi.

Mkutano ule ulimchagua Mzee Yussuf Ngozi kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa tawi la TANU Moshi mjini.

Taratibu Kimalando akawekwa pembeni.

Katika halmashauri ya kwanza ya tawi lile alikuwapo msichana mdogo wa miaka 24, Lucy Lameck ambae baadaye alikuja kuwa waziri katika serikali ya wananchi.''

Lucy alikuwa mwanachama Moshi na si Dar es Salaam na TANU Moshi ilikuwa imechelewa sana kuanzishwa.
 
Je wanachama wa bara wakija Dares salaam walisita kuwa wanachama wa TANU? Unaposema TANU ilichelewa sana kuanzishwa MOSHI hudhani kuwa kulikuwa na wanachama wa TANU mkoa wa Kilimanjaro ikiwamo Moshi kabla ya tawi la TANU kuanzishwa rasmi? Mzee Olotu alikwambia tawi la TANU lilianzishwa rasmi lini mkoani Kilimanjari[ Northern Province wakati huo}?
 
Je wanachama wa bara wakija Dares salaam wanasita kuwa wanachama wa TANU? Unaposema TANU ilichelewa sana kuanzishwa MOSHI hudhani kuwa kulikuwa na wanachama wa TANU mkoa wa Kilimanjaro ikiwamo Moshi kabla ya tawi la TANU kuanzishwa rasmi?
Ndinani,
Itakushangaza lakini nyaraka za TANU kutokea siku ya kwanza zipo katika uangalizi wa akina Sykes.

Nyaraka hizi ndizo nilizotumia kuandika kitabu cha Abdul Sykes na historia ya TANU.

Nimesoma mengi ya siku za mwanzo za TANU Dar es Salaam na ni wanawake gani walikuwa mstari wa mbele katika chama katika siku zile za mwanzo.

Jina la Lucy Lameck sijakutananalo popote ila Moshi kama nilivyokueleza.

Hakuna ushahidi wa kuwa kulikuwa na wanachama Moshi waliojiunga na TANU Dar es Salaam kisha wakarejea Moshi na kuanza harakati.
 
Huyu mzee amejaa hila, na maandishi yake mimi nayaona kama ya hovyo tu kwakuwa yamejiegemeza ktk kubagua watu kidini kwa kujifunika na blanketi la kujifanya anaijua sana historia ya nchii!!
Hayo maneno hapo ni uthibitisho tosha!

Nimeona vitabu vyake vinauzwa misikitini kariakoi, nikacheka kimoyomoyo!
Mhh! kariakoi!
 
Back
Top Bottom