Waliomsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955

Kiranga,
Umesema kweli kabisa makosa mengi hufanyika na ni vizuri kusikia na mwengine analijua vipi.

Miaka mingi ikipita kumbukumbu hupotea kirahisi sana.

Umenikumbusha mbali sana kaka.
Collection yangu ya ngoma hizo ilikuwa kali sana.

Siku nilipofika Apollo Theatre New York nikakumbuka wakati nina miaka 16 hivi nakua Dar es Salaam mimi na wenzangu tukiziimba nyimbo za Tamla Motown.

Nilisimama kwa muda Broadway nikakumbuka mwimbo wa Wilson Pickett ''Funky Broadway,'' na ikasadifu kuwa barabara nikiipita Manhattan katika shughuli zangu.

Wengi wa hawa ''stars'' walianza ''carrier'' zao hapo Apollo Theatre na tukikuona mbali sana...

Kaka Kiranga Temptations wakaja Paris kufungua Disneyland mimi niko upande wa pili wa English Channel katika kimji kidogo Wales wako mubashara...wazimu kaka sasa tumekuwa watu wazima miaka imekwenda wapi?

Nadhani Temptations aliye hai ni mmoja tu.
Daah

Mzee wewe ni legend sana.

Salute
 
Mhh! kariakoi!
Kwezisho,
Huyu ndugu yangu Mzizi wa Mbuyu amehamaki sana ndiyo zinakuja lugha za "huyu mzee," akidhani kuwa kuniita mzee kutaniudhi.

Ndiyo na huku kusema "najifanya"naijua historia ya TANU.

Utu uzima na uzee kwangu ni jambo la kushukuru sana kwani wezangu wengi wametangulia.

Ama kujidai mimi sijidai ukweli ni kuwa kweli naijua historia ya uhuru wa Tanganyika na si kwa kuwa mimi nimemzidi yeye akili.

La hasha naijua historia ya TANU kwa kuwa chama hiki kimeundwa na wazee wangu.
Kwa ajili hii historia ya uhuru imefungamana na historia ya babu zangu.

Kama siwezi kujua historia ya babu yangu nitajua ya nani?
Anasema vitabu vyangu vinauzwa misikitini.

Kweli bookshop tatu zenye kuuza vitabu vyangu Dar es Salaam ziko karibu na misikiti.
Kwani hairuhusiwi?

Mimi miaka yote nanunua vitabu Cathedral Bookshop na wala sijakasirika na kutangaza kwa watu kwa nini Cathedral Bookshop wana duka la vitabu kanisani.

Hivi huu mbuyu haujui kuwa Dar es Salaam Bookshop ni duka la kanisa?
Hivi huu mzizi haujui TMP Tabora ni duka la kanisa?

Huyu ndugu yangu atulize akili yake atafaidika sana na elimu niliyonayo katika historia ya Tanganyika.

Anazungumza ubaguzi...

Hapa ndiyo zamu yangu kucheka kimoyomoyo.

Hivi kweli haujui ukweli au chembelecho anajifanya?
 
Kwezisho,
Huyu ndugu yangu Mzizi wa Mbuyu amehamaki sana ndiyo zinakuja lugha za "huyu mzee," akidhani kuwa kuniita mzee kutaniudhi.

Ndiyo na huku kusema "najifanya"naijua historia ya TANU.

Utu uzima na uzee kwangu ni jambo la kushukuru sana kwani wezangu wengi wametangulia.

Ama kujidai mimi sijidai ukweli ni kuwa kweli naijua historia ya uhuru wa Tanganyika na si kwa kuwa mimi nimemzidi yeye akili.

La hasha naijua historia ya TANU kwa kuwa chama hiki kimeundwa na wazee wangu.

Kama siwezi kujua historia ya babu yangu nitajua ya nani?

Anasema vitabu vyangu vinauzwa misikitini.

Kweli bookshop tatu zenye kuuza vitabu vyangu ziko karibu na misikiti.

Kwani hairuhusiwi?

Mimi miaka yote nanunua vitabu Cathedral Bookshop na wala sijakasirika na kutangaza kwa watu kwa nini Cathedral Bookshop wana duka la vitabu kanisani.

Huyu ndugu yangu atulize akili yake atafaidika sana na elimu niliyonayo katika historia ya Tanganyika.

Anazungumza ubaguzi...

Hapa ndiyo zamu yangu kucheka kimoyomoyo.

Hivi kweli haujui ukweli au chembelecho anajifanya?
Huyu bwana, anasoma unayoyaandika na kuyaelewa halafu anajifanya hajui. Hii elimu unayoitoa huwa inawafumbua macho wengi. Mimi nilisoma elimu ya msingi, sekondari zote mbili, historia yetu inaacha matundu mengi sana, nyie mnayoijua mnapojitahidi kuyaziba ndivyo tusioijua tunavyoelimika. Najua wapo wengine kama wewe wanayajua mengi ila wamenyamaza na wanayoyajua. Yawezekana hawataki tuyasikie au wanaogopa maneno ya watu wanakatisha wenzao tamaa pale wanapoeleza ufahamu wao.
Huyu anajua ukweli ila anajifanya hajui. Sie tunasema muache kama alivyo!
 
Mohamed Said shukrani kwa darasa na elimu.

Lakini kuna mambo mawili nimeyaona, kwanza kuna mchangiaji mmoja Ndinani amerejea mara kwa mara kwamba huyo mwanamke ni Lucy, lakini umeendelea kupinga ilihali yeye anaeleza kwanini anasema ni Lucy na wewe unatoa fafanuzi ambazo huenda zikawa ni za kweli lakini hazijibu ikiwa huyo ni Lucy au sie.

Jambo la pili Kiranga ametolea mfano kuonyesha umuhimu wa kufanya peer review (kutafuta ukweli wa jambo kwa zaidi ya chanzo kimoja tena vyenye kukubalika na kusadikika kuwa na mamlaka kuhusu uwezo wao) hii inamaanisha jambo lolote ili kuondoa sintofaham ya maoni, taarifa au jambo kuchukua upande mmoja wa habari.
Matokeo yake umeeleza mambo mengi sana kukuhusu wewe binafsi, sio jambo baya kitu ambacho hata Kiranga angeweza kujimwambafy akatuonjesha yeye ni nani lakini ameamua kujikita kwenye hoja iliyopo mezani.

Kwa ufupi nnachokusema ni kwamba, unaweza kuwa na uelewa au taarifa nyingi sana lakini kuweza kujiridhisha kutoka vyanzo kadhaa vyenye vigezo ni muhimu sana. Pia haimaanishi unachokijua wewe ndio kipo sahihi na wengine hawaelewi au taarifa zao si za kweli.

Mwisho kabisa kujaribu kwenda kwenye hoja moja kwa moja bila kuweka mambo mengi kama hakuna ulazima.

Endelea kutupa shule kadri upatapo nafasi mkuu. Shukran
 
The Monk,
Ahsante.

Nikienda kwenye jibu moja kwa moja kuna mengi mtayakosa.
Hii ndiyo sababu natoa jibu pamoja na yale ninayoona ni muhimu kufahamika.
 
Mohamed Said shukrani kwa darasa na elimu.

Lakini kuna mambo mawili nimeyaona, kwanza kuna mchangiaji mmoja Ndinani amerejea mara kwa mara kwamba huyo mwanamke ni Lucy, lakini umeendelea kupinga ilihali yeye anaeleza kwanini anasema ni Lucy na wewe unatoa fafanuzi ambazo huenda zikawa ni za kweli lakini hazijibu ikiwa huyo ni Lucy au sie.

Jambo la pili Kiranga ametolea mfano kuonyesha umuhimu wa kufanya peer review (kutafuta ukweli wa jambo kwa zaidi ya chanzo kimoja tena vyenye kukubalika na kusadikika kuwa na mamlaka kuhusu uwezo wao) hii inamaanisha jambo lolote ili kuondoa sintofaham ya maoni, taarifa au jambo kuchukua upande mmoja wa habari.
Matokeo yake umeeleza mambo mengi sana kukuhusu wewe binafsi, sio jambo baya kitu ambacho hata Kiranga angeweza kujimwambafy akatuonjesha yeye ni nani lakini ameamua kujikita kwenye hoja iliyopo mezani.

Kwa ufupi nnachokusema ni kwamba, unaweza kuwa na uelewa au taarifa nyingi sana lakini kuweza kujiridhisha kutoka vyanzo kadhaa vyenye vigezo ni muhimu sana. Pia haimaanishi unachokijua wewe ndio kipo sahihi na wengine hawaelewi au taarifa zao si za kweli.

Mwisho kabisa kujaribu kwenda kwenye hoja moja kwa moja bila kuweka mambo mengi kama hakuna ulazima.

Endelea kutupa shule kadri upatapo nafasi mkuu. Shukran

Inaelekea Sheikh Mohamed Said hapendi wazo la peer review kwani amejiaminisha kuwa kile anachoamini yeye ndio sahihi!! Nimejaribu hata kumpa references za watu ambao wangeweza kumsaidia akapata uhakika wa picha ile lakini bado anang'ang'ania kile anachoamini yeye. Daisy alikuwa mtoto mdogo sana wakati wa haraketi za marehemu baba yeke lakini kuna baba yake mdogo aitwae Abbas ambale pia alikuwa mwanasiasa wakati huo,yeye anaweza kuwa na kumbukumbu sahihi kuliko mwanae.

Zaidi ya hayo sio wakina mama wa Kiislam peke yao ndio walijishuhulisha na siasa za TANU iwe Dar es Salaam [ mfano huyo mama aliyevaa sketi kwenye hiyo picha ] hata huko bara. Ntakupa mfano mmoja ninaoufahamu sana ni kule Nyanda za juu kusini ambako vinara wanawake wa siasa enzi za TANU walikuwa mama BINTI MATOLA na mama BINTI MWASHAMBWA. Kama ilivyokuwa, mmoja alikwa muislam na mwingine alikuwa misheni! Hata baada ya kuundwa UWT wakina mama wa madhehebu mbali mbali walichaganyika.
 
Ndinani,
Kipi kinachokufanya wewe useme mimi nang'ang'ania kuwa huyo bint si Lucy Lameck?
Hiyo picha kwanza nikufahamishe mimi ndiyo niliyoiweka mtandaoni.

Picha hii nimeipata kutoka kwa Jim Bailey mwaka wa 1993 mmimiliki wa gazeti la Drum.
Nimeikuta katika mswada wa kitabu, "The Story of Julius Nyerere," alichonipa kuhariri.

Kitabu kimeshachapwa na miaka mingi kipo sokoni.
Hiki ni kitabu cha picha na maelezo ya picha.

Picha hii ya Bi. Chiku bint Said Kisusa nimewaonyesha watu wengi kupata majina sijafanikiwa.

Picha nyingine nilizopata katika mswada huo ni picha hizo mbili za safari ya Mwalimu Nyerere UNO akisindikizwa.

Bailey kanipatia picha ya Sheikh Hussein Juma na picha ya Sheikh Suleiman Takadir yuko jukwaani na Mwalimu Nyerere, Mama Maria, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Bi. Titi Mohamed na John Rupia.

Picha hizi zote juu ya umuhimu wake hazikupata kuonekana na watu hadi mimi nilipoziweka mtandaoni.

Picha hizi zinatoka Bailey Collection, Johannesburg.
Ally Sykes ndiye aliyenijulisha kwa Jim Bailey.

Hilo la wanawake wa Kiislam wala sioni umuhimu wa mimi kueleza chochote.

Sasa badala ya kuhangaika na mambo madogo madogo ndugu yangu Ndinani angeishughulisha akili yake kujua picha muhimu kama hizi ambazo mimi nimeziweka hadharani kwa watu wote wazishuhudie zilikuwa wapi miaka yote hazionyeshwi hadi nazionyesha mimi tena katika historia inayokwenda na picha hizo?.
 
Attachments

  • The Story of Julius Nyerere (1).jpg
    The Story of Julius Nyerere (1).jpg
    29.7 KB · Views: 2
  • SHEIKH SULEIMAN TAKADIR.JPG
    SHEIKH SULEIMAN TAKADIR.JPG
    8.4 KB · Views: 2
Sawa, sisi wengine historia ya Tanzania tunaiona inayumba maana kila mtu anatoa yake na sisi hatukuwepo
 
Sawa, sisi wengine historia ya Tanzania tunaiona inayumba maana kila mtu anatoa yake na sisi hatukuwepo
Code...
Hapana "kila mtu" wala mimi usiniingize katika "kila mtu."

Labda ni bahati kuwa historia hii ya wazee wangu imefungamana na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Labda nikueleze vipi historia ya maisha ya babu yangu Salum Abdallah akikueleza maisha yake atakuwa anakueleza historia ya African Association na historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia yake ni historia ya athari za ukoloni.

Baba yake kaingia Tanganyika 1880s kutoka Belgian Congo kama askari katika jeshi la Wajerumani.

Babu yangu kaongoza general strikes 3 nazo ni 1947, 1949 na 1960.

Babu yangu ni muasisi wa TANU Tabora 1955 na pia ni muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU)akiwa founder president.

Babu yangu akiwa Rais wa TRAU na Kassanga Tumbo akiwa Katibu aliunganisha harakati za TANU na TRAU katika kupambana na Waingereza.

Sasa huwezi kusema ati kila mtu kwani mimi si kila mtu mimi naeleza historia iliyoishi ndani ya nyumba yetu.

Hili si suala la kila mtu kutoa historia yake.

Historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya TANU ni moja tu kokote watu walipokuwapo na kuunda TANU.

Mimi naijua historia hii na mashujaa wake na ndiyo hii mnaisoma hapa.
 
trueee...............

Kweli historia ya nchi yetu inayofundishwa mashuleni imechujwa chujwa lakini hata hivyo tunahitaji historia ambayo ni ya kweli bila chembe za bias kuwa jamii moja ndio Ilikuwa zaidi kuliko nyingine katika harakati za kudai uhuru ili hali wanannchi wote irrespective of religious affiliation walishiriki!

Nitakupa mfano mmoja dhahiri unaooneshwa na Mohamed Said nao ni pale anaposema babu yake aliongoza migomo mitatu ya wafanyakazi wa shirika la Reli [TRAU]; lakini wote tunajua kuwa wakati huo kufanikiwa kwa migomo ya wafanyakazi halikuwa jukumu la mtu mmoja [ Mohamed anataka tuamini hivyo] bali ushirikiano wa wengi!! Na sio ushirikiano wa chama cha wafanyakazi wa reli peke yao bali pia ushirikiano na vyama vingine vya wafanyakaza kwa mfano wale waliokuwa wanafanya kazi mikongeni wakiongozwa na wakina Mkello!!!

Tunahitaji historia ya kweli isiyokuwa na bias ya aina yeyote ya kupendelea sehemu ya jamii!!
 
Kweli historia ya nchi yetu inayofundishwa mashuleni imechujwa chujwa lakini hata hivyo tunahitaji historia ambayo ni ya kweli bila chembe za bias kuwa jamii moja dio Ilikuwa zaidi kuliko nyingine katika harakati za kudai uhuru ili hali wanannchi wote irrespective of religious affiliation walishiriki!

Nitakupa mfano mmoja dhahili unaooneshwa na Mohamed Said nao ni pale anaposema babu yake aliongoza migomo mitatu ya wafanyakazi wa shirika la Reli [TRAU]; lakini wote tunajua kuwa wakati huo kufanikiwa kwa migomo ya wafanyakazi halikuwa jukumu la mtu mmoja [ Mohamed anataka tuamini hivyo] bali ushirikiano wa wengi!! Na sio ushirikiano wa chama cha wafanyakazi wa reli peke yao bali pia ushirikiano na vyama vingine vya wafanyakaza kwa mfano wale waliokuwa wanafanya kazi mikongeni wakiongozwa na wakina Mkello!!!

Tunahitaji historia ya kweli isiyokuwa na bias ya aina yeyote ya kupendelea sehemu ya jamii!!
Kwa upande wa mkongeni ule mgomo wa Mazinde Sisal Estate ulitikisa sana serikali ya mkoloni.
 
Hiyo picha ya kwanza juu ,umewataja majina hao wakina mama wengi waliovalia mabaibui lakini umemuacha huyo aliyevaa sketi humjui? Huyo mama ni Lucy Lameck!!!!
Hawezi kumtaja Mkristo, na hata akimtaja...atamtaja yuko na jazba tayari na kaghafilika moyoni.

Wallah,
 
Abdi...
Historia hii nimeiandika ni kitabu hivi sasa kipo huu mwaka wa 21 na kiandikwacho hakipotei mradi wako wasomaji.
Na vipi kama wasomaji ni 2% tena wa misikitini tu?

Wakati huo 98% wana historia tayari iliyotangulia na wakaikubali na kuiweka ubongoni na mioyoni?
 
Katika wote waliomzsindikiza nimeona wakristo wawili tu lakini wengi ni WAISLAMU,Kweli uhuru wa Tanganyika umeletwa na waislamu.
Hapa umemfurahisha Sanaa mzee Mohammed Said na wenzie kina FF

Nenda akakununulie gahawa

Hahahaha.........!!!!
 
Nyerere ndiye alianzisha kudai uhuru. Nyerere ndiye alianzisha ofisi za kudai uhuru Tanganyika. Nyerere ndiye alianzisha TANU. Nyerere ndiye alibuni jina la TANU.

Hao wote hapo kwenye picha walikuwa wanajipendekeza tu kwa Nyerere.

Historia ya kudai uhuru wa Tanganyika inaanzia na kuishia kwa Nyerere.

Nyerere kaja Dar kakuta watu hawajui kusoma wala kuandika. Kakuta watu wajinga wajinga tu hata uhuru hawaujui ni nini.

Sio hayo yanayompa utakatifu? Au kuna mengine yanayompa utakatifu ambayo hatuyajui?
UNAFIQ ni dhambi ewe Ajuza.

Elewa hilo.
 
Kweli historia ya nchi yetu inayofundishwa mashuleni imechujwa chujwa lakini hata hivyo tunahitaji historia ambayo ni ya kweli bila chembe za bias kuwa jamii moja dio Ilikuwa zaidi kuliko nyingine katika harakati za kudai uhuru ili hali wanannchi wote irrespective of religious affiliation walishiriki!

Nitakupa mfano mmoja dhahili unaooneshwa na Mohamed Said nao ni pale anaposema babu yake aliongoza migomo mitatu ya wafanyakazi wa shirika la Reli [TRAU]; lakini wote tunajua kuwa wakati huo kufanikiwa kwa migomo ya wafanyakazi halikuwa jukumu la mtu mmoja [ Mohamed anataka tuamini hivyo] bali ushirikiano wa wengi!! Na sio ushirikiano wa chama cha wafanyakazi wa reli peke yao bali pia ushirikiano na vyama vingine vya wafanyakaza kwa mfano wale waliokuwa wanafanya kazi mikongeni wakiongozwa na wakina Mkello!!!

Tunahitaji historia ya kweli isiyokuwa na bias ya aina yeyote ya kupendelea sehemu ya jamii!!
Ndinani,
Nadhani umeninukuu au umeuelewa mfano wa babu yangu ''out of context.''

Nimetoa huo kama mfano wa kukufahamisha kuwa historia hii ninayoieleza hapa mimi ni mwenyeji nazungumza kitu ninachokijua.

Sikuwa na maana kuwa migomo yote hiyo kaiongoza peke yake.
Bahati mbaya sana kwako kuwa umeelewa vinginevyo.

Tuje kwa hili la ''jamii moja.''

Ikiwa huamini mimi sina tatizo na hilo lakini historia ya uhuru wa Tanganyika ndivyo ilivyo na ushahidi uko tena mwingi tu.

Angalia historia ya Abdul Sykes.

Baba yake ni muasisi wa African Association mwaka wa 1929 na kaacha mswada ambao leo ni sura katika kitabu alichohariri John Iliffe.

Hili nimelieleza mara nyingi hapana haja ya kulirudia.
Sasa tuje kwa babu yangu Salum Abdallah.

Yeye hakuwa muasisi wa African Association kuwa alikuwapo katika ule mkutano wa uasisi lakini alikuwa moja wa wanachama wa mwanzo kabisa.

Babu yangu na Kleist Sykes walikuwa majirani nyumba zao zikitazamana hapo Mtaa wa Kipata na wote wakifanya kazi Tanganyika Railways katika miaka ya 1920s.

Hii ndiyo sababu kubwa unaniona historia hii naijua vizuri.

Babu yangu alihamia Tabora mwaka wa 1947 baada ya Loco Shed idara ambayo alikuwa akifanya kazi kuhamishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Tabora.

Akiwa Tabora ndiko alipoongoza hiyo migomo niliyoitaja.

Mwaka wa 1953 TAA Tabora ilimtuma Germano Pacha TAA HQ na maelekezo aliyopewa ni kuwa afike nyumbani kwa Abdul Sykes na amweleze mipango ya TAA Tabora kutaka kuunda chama cha siasa.

Hiki ni kisa kirefu hapa nafupisha laikini nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes kwa ukamilifu wake.

Jibu ambalo Abdul alimpa Germano Pacha ni kuwa Tabora wawe na subra mipango inafanyika TAA HQ na ikikamilika watafahamishwa.

Huu ndiyo ukawa mwanzo wa mikutano ya siri Town School, Tabora kila Jumapili na aliyekuwa akiwafungulia darasa kukutana hapo alikuwa Abubakar Mwilima ambae alikuwa mwalimu hapo na agenda yao ilikuwa moja tu nayo ni kupata taarifa kutoka TAA HQ New Street kuhusu chama cha siasa kudai uhuru wa Tanganyika.

Haya ndiyo maisha ya babu yangu yalivyofungamana na TANU.

Ulipokuja mwaliko wa mkutano wa TAA wa mwaka wa 1954 wa kuunda TANU Germano Pacha kama Katibu wa TAA Western Province akahudhuria mkutano ule.

Mchango mkubwa wa kumwezesha Pacha kusafiri kuja Dar es Salaam alitoa babu yangu na ilikuwa shs. 20.00.

Hii ndiyo historia ya wazee wangu sidhani kama kuna mtu ana haki ya kunikataza kuihifadhi historia hii kwa kuwa tu ni historia ya uhuru wa Tanganyika.
 
Attachments

  • SALUM ABDALLAH NA KASSANGA TUMBO.jpg
    SALUM ABDALLAH NA KASSANGA TUMBO.jpg
    76.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom