Waliomshadidia Makonda ni watu wanaochelewa kuelewa

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
Tuwasamehe waliokuwa wakishadidia uhuni wa Paul Makonda, wao na waliomshadidia ni watu wanaochelewa kuelewa, au tuwaite 'low birth score'. Lakini baada ya Rais kuwateua wataalamu wa fani husika katika kupambana na dawa za kulevya, na kwa kile kilichotokea leo tar 13/2/2017 ni ishara kwamba Makonda mwenyewe angalau ameelewa, ingawa bado sio mtu wa kumuamini, muda wowote anaweza kuibuka na kituko kingine.
Sasa, tunaweza kupambana na dawa za kulevya, angalau kwakuwa watu wenye ujuzi wamepewa nafasi, lakini ole wao waanze kutumikia wanasiasa ambao lengo lao kubwa ni kupata sifa na umaarufu kwa mashabiki wao.

Nakumbushia pia kauli ya waziri wa afya, Mh. Ummy Mwaimu kwa mkemia Mkuu wa serikali kuangalia uwezekano wa kuanza utaratibu wa kuwapima wanafunzi wa secondari na vyuo ili kubaini wanatumia dawa za kulevya na kuwadhibiti.
Lakini hilo linapaswa kwenda mbali zaidi, kuhusisha maofisi ya serikali, vilabu vya michezo, makundi ya wanamuziki nk.

Namshauri pia Mh. Rais Magufuli, kwakuwa amoenesha nia ya dhati ya kupambana na dawa za kulevya, basi ni wakati wa kuteketeza hadharani madawa yote yaliowahi kukamatwa na jeshi la polisi huko nyuma ili ku-discourage biashara hiyo haramu. It is a tricky request, lakini ndio jambo rahisi litakaloonesha 'useriousness' wa vita hii. La! Kama upelelezi bado unaendelea kwa matukio ya mikaa 10+ nyuma, basi sawa!!!

Tupambane na dawa za kulevya kwa njia sahihi, tusiwape nafasi wahalifu/wajinga wajifanye kupambana na uhalifu kwa njia za kihalifu, zinazowapa wahalifu nafuu na utakaso na kuwajengea huruma wasiostahili katika jamii yetu.
 
Hyo ya kuteketeza hadharani labda kwa Duterte na yakichomwa wanaweza uchoma hata wa ugali kumbe zuga tu
 
Kati ya single zote ambazo amewahi kutoa hii ameuza sana na mwenzake wa Arusha nadhani yupo studio anarecord single itakayotoka march.
 
"Ujinga ni mzigo mkubwa sana!! Omba busara ya Mungu kwa kila jambo kuliko utajiri na kiburi" Nape
 
Back
Top Bottom