Waliombeza maximo wako wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliombeza maximo wako wapi?

Discussion in 'Sports' started by Kizimkazimkuu, Dec 16, 2008.

 1. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Lilikuwapo kundi kubwa la watu waliombeza sana Kocha mbrazil Marcio Maximo,hasa baada ya kushindwa michezo ya Chalenji na matokeo ya kutoridhisha katika baadhi ya mechi.Kocha alipata lawama kubwa sana katika uchaguzi wa kikosi chake.majina kama Shaban Dihile,Jerry tegete( kuna baadhi ya magazeti yalimuita mtalii),Kigi makassy,nk yalionekana hawakustahili kuwamo kwenye kikosi.
  Wapo wanahabari waliodiriki kuandika kuwa maximo sio kocha ,bali ni mtaalam wa uhamasishaji,na kuwa kikubwa alichofanikiwa nchini ni kuhamasisha mashabiki kuipenda na kuishangilia timu.Kati ya watu walioongoza kumponda kocha maximo waziwazi ni Kocha 'maarufu' nchini Syllersaid Mziray kupitia makala zake kwenye magazeti.Sijui leo wako wapi hawa critics wetu wa soka la bongo?
   
 2. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35  Wataalamun wanasema bila cricisms hakuna maendeleo, lakini criticism za huyu jamaa kwa kocha Maximo mimi zimekuwa zikini-bore sana mpaka kufikia kiasi kumweka kando kabisa. Sijaelewa mpaka leo kwanini alikuwa akiimponda namna ile. Inawezekana ni issues za interests. Lakini mbaya sana. Nina hakika hana pa kushika sasa
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mziray anamuonea wivu maximo.
  na kinachogomba hapa ni kuona kwamba maximo anavuta mpunga wa maana.
  anatamani kama angekuwa yeye ndiye anavuta huo mpunga.kitu kingine ni kuwa mziray alikuwa anajiona kuwa yeye ndiye kocha maarufu sana tanzania lakini ghafla maximo kacjichukulia ujiko wooote.hata waandishi wa habari walichonga sana, lakini kama alivyosema mwenyewe maximo, na kama wanaoufahamu vizuri mpira wa miguu, walijua kuwa kutengeneza mpira sio jambo jepesi kihivyo, mpira unahitaji muda wa kutosha ili kuutengeneza. na ama kwa hakika timu imekuwa ikiimarika kadri siku zinavyokwenda na kadri maximo anavyofanya mabadiliko.Kama ni hamasa yanga na simba kuna hamasa kubwa vile vile lakini hakuna mafanikio yoyote ya kujivunia zaidi ya migogoro.
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Yaani ushindi tu Sudan sifa zote hizi???
  Watu bwana!
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Fungua macho ndugu yangu, kama kweli wewe ni mzalendo halisi kama unavyojiita huitaji kusimuliwa.We unafikiri sudani ni sawa na mji mpwapwa???
  yaani hata hujui mpaka kufikia kucheza na sudan stars imezifunga timu ngapi???
  Yaani hata hujui kuwa miongoni mwa nchi 51 za bara africa zilizoshiriki michuano hii, tanzania imekuwa ni miongoni mwa nchi chache (8) zilizofuzu kucheza fainali za CHAN mwaka 2009 huko ivory coast???
  inaonekana nawewe ndio walewale, tatizo lenu mna chuki kiasi kwamba hata mafanikio ya maximo mnayafumbia macho.na hizo chuki zetu hazitawasaidia chochote zaidi ya kuwaongezea maumivu.na kwa taarifa yako maximo ana mpango wa kuongeza mkataba wa kuinoa stars, zaidi ya ule mwaka mmoja aliokuwa amesaini, mwaka huu mtavimba mpaka mpasuke!!!
   
 6. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mimi ninawapongeza Stars kwa kutuondolea aibu ya kushiriki mara kwa mara bila kufuzu katika fainali zenyewe kwa kipindi kirefu. Hata hivyo bado sioni kama ni kitu cha kujivunia sana, ukizingatia kwamba njia ya kufuzu ilikuwa imegawanywa makusudi na CAF katika kanda kadhaa; Southern Zone, Northern Zone, Central Zone, Central East Zone, Zone West A na Zone West B.
  Tanzania tuliwekwa Central East Zone, kwa maana kwamba kuelekea kufuzu, tulikuwa na possibility ya kukutana na na timu hizi TU: Rwanda, Burundi, Eritrea, Kenya, Uganda na Sudani. Sudan hawakuwekwa raundi ya awali, walisubiri raundi ya kwanza, ila wengine tukatoana toana na sisi tukawapitia Kenya, Uganda na hatimaye Sudan.
  Kwa maana hiyo hatukuwa na ugumu wa mataifa ya West na North ambayo ndo yana ligi ngumu za nyumbani.
  Nataka kusema hivi, tujipongeze lakini tusijisifu sana kwani njia ilikuwa ni rahisi sana !!
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Yap..anastahili Sifa zote hizi,kwani ukiacha Maximo makocha wengine si ndo hao waliosababisha tukaanza kuitwa 'Kichwa cha Mwendawazimu'??,na ukumbuke kuwa ukiachana na mashindano ya challenge ambayo huwa tuna tiketi ya moja kwa moja,Tanzania hatujashiriki mashindano makubwa yenye hadhi kama haya kwa muda wa takribani miaka 28(mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1980),,na pia kua timu zenye majina makubwa tu kisoka Afrika kama Nigeria na Cameroon zimeshindwa kupata tiketi ya kushiriki mashindano haya(CHAN) lakini sisi tumepata so Maximo anastahili sifa zote hizi otherwise ni DONGE tu hilo mkuu
   
Loading...