Maximo ataja kikosi cha CHAN-2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maximo ataja kikosi cha CHAN-2009

Discussion in 'Sports' started by Balantanda, Feb 3, 2009.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  KIUNGO Mwinyi Kazimoto wa JKT Ruvu ameitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Stars pamoja na Zahoro Pazi wa Mtibwa Sugar na kumtema Meshack Abel kwaajili ya fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN).


  Beki wa kati wa timu ya Simba, Meshack Abel anayesumbiliwa na majeruhi aliyoyapa kwenye fainali za Kombe la Chalenji ameachwa katika kikosi hicho kitachokwenda Ivory Coast.


  Chipukizi Kazimoto aliyejiunga na JKT Ruvu msimu huu akitokea timu ndogo ya Ruvu Shooting ni miongoni aliowavutia mashabiki wengi kwenye msimu huu wa ligi kutokana umahiri wake uwanjani aitwa kwenye timu hiyo.


  Mbrazil Marcio Maximo alitangaza majina ya wachezaji 27 jana kwa ajili ya michuano ya afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani ambayo fainali zake zinafanyika nchini Ivory Coast kuanzia Feb 22 hadi Marchi 8 yanayojulikanao kama CHAN.


  Maximo aliwarudisha wachezaji wengine wa tatu ambao walishawahi kuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa siku za nyuma ambao ni Erasto nyoni , Salvatory Ntebe kutoka Azam na Jabil Aziz wa Simba.


  Mbrazil huyo alisema kuwa anapochagua wachezaji kwenye kikosi hicho anaangalia mambo mengi ikiwa na pamoja na kiwango cha mchezaji huyo na jinsi anavyojituma uwanjani katika kuisaidia timu yake.


  Maximo alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa magumu sana kwa sababu kwani kunatimu ambazo zinajulikana katika ulimwengu wa soka kama Senegal na Ivory Coast.


  "Mashindano haya yatakuwa magumu sana kwetu kwa sababu tunakutana na mataifa ambayo yana nguvu na wamejiandaa vizuri, nimewaona jinsi Ivory Coast walivyojiandaa na mazoezi yao japo ni wachezaji wa ndani, lakini wanaonekana wamejiandaa vema,'' alisema Maximo.


  Hata hivyo kocha huyo alisema timu zao zinaonekana nzuri kwa sababu wanamisingi mizuri ya kujiandaa kimpira tangu utotoni na kutoa ushauri wa kuendeleza michezo ya Umiseta na Umintasuta mashuleni ilituweze kuendeleza mpira na kuinua vipaji vya mpira.


  Akiizungumzia mechi ya kirafiki katika ya Stars na Zimbambwe, Maximo alisema mechi hiyo itakuwa ni moja ya maandalizi ya fainali hizo pia aliongeza kuwa timu hiyo ni nzuri kwani imeitoa Afrika Kusini kucheza fainali hizo na ataakikisha timu yake inashinda kwani anamuda wa siku sita za kufanya maandalizi.


  Kikosi cha Taifa Stars kitakuwa hivi: Makipa Deogratius Boneventure ( Simba) Shaban Dihile ( JKT Ruvu), Farouk Ramadhan (Miembeni)

  Mabeki, Shadrack Nsajigwa, Nadir Harob 'Cannavaro', Amir Maftar( Yanga), Kelvin Yondani ' Vidic', Juma Jabu ( Simba) na Salum Swed (Mtibwa),Erasto Nyoni, Salvatory Ntebe (Azam FC).


  Viungo Nurdin Bakari, Godfrey Bonny, Abdi Kassim, Athuman Idd 'Chuji' ( Yanga) Shaban Nditi, Zahoro Pazi ( Mtibwa Sugar) Nizar Khalfan ( Moro United) na Haruna Moshi 'Boban' Henry Joseph na Jabil Aziz ( Simba) na Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).


  Washambuliaji ni Mrisho Ngassa, Jerry Tegete na Kigi Makasi ( Yanga) Uhuru Seleman ( Mtibwa) na Mussa Hassan Mgosi ( Simba).
   
 2. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kikosi kimetulia hicho,wakijituma watatoa upinzani, Mnasemaje wadau?
   
 3. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,030
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 280
  Mambo mukide; mwendo mdundo
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mechi ya kirafiki na Zimbabwe itatupa muelekeo, manake nao Zimbabwe wamefuzu kucheza CHAN. Lakini ilitakiwa wapate mechi mbili ama tatu za majaribio, japo watasema kuwa CECAFA Challenge Cup Uganda ilitosha kwa majaribio manake wachezaji wengi walikuwepo. Kila la heri.
   
 5. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Tatizo kubwa lililopo sio katika kuteuwa timu ama kufundisha uchezaji, mimi nimeona mara nyingi Maximo akiteuwa timu nzuri akifundisha vizuri ila hukosea sana kwenye kupanga timu ya kuanza na substitute wake(yaani combination ya wachezaji uwanjani)
  Kocha aweza kuwa mzuri sana afu akawa na mapungufu, moja ya mapungufu ya maximo ni pressure ya mechi inamzidia.
   
 6. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Habarini za siku wadau, jamani mechi ya Taifa Star na Zimbabwe inachezwa lini?
   
 7. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Mechi ni kesho Jumatano
   
 8. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Thanks for informations.
   
 9. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2015
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Hapa ni wakati ule timu ya taifa ni timu.
   
 10. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2015
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Aaaaaah acha kabisa Mkuu!!!
   
 11. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2015
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,293
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Miaka mitano baadae wanasoka wote hao wanaounda national team wamezeeka. Hii hutokea bongo tu.
   
 12. b5-click

  b5-click JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2015
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 1,974
  Likes Received: 671
  Trophy Points: 280
  Haruna Moshi "Boban"
   
 13. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2015
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Kimsingi asilimia kubwa walitakiwa wawe kwenye kiwango bora zaidi kwa sasa. Lakini ukitazama orodha ni wachezaji wachache tu waliodumu kwenye kiwango.

  Nadir Harob 'Canavan ( Yanga), Kelvin Yondani (Yanga) Erasto Nyoni (Azam)


  Mwinyi Kazimoto (Almarrikhiya).


  Washambuliaji ni Mrisho Ngassa (Bidvest)
   
Loading...