Waliokuwa na ndoto za kuishi ughaibuni

Waliokuwa na ndoto za kuishi ughaibuni

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,625
Reaction score
65,097
Wengi tulikuwa na ndoto za kuishi sehemu fulani katika hii dunia ila kutokana na changamoto za kimaisha, tumejikuta tunaishi hapa tulipo sasa. Wapo waliokuwa na ndoto za kuishi Ulaya, USA, Afrika kusini, Namibia, Australia n.k ila kutokana na sarakasi za hapa na pale..matokeo yamekuwa ni sifuri na kujikuta hapa tulipo.

Kwa wale ambao wako 'Single' bado wana nafasi kubwa ya kutimiza hizo ndoto zao, kwa kutafuta wenza ambao wako maeneo husika. Ila kwa wale ambao tayari wako pacha, inabidi watumie nguvu za ziada kutimiza yale waliyokuwa wakiyatamani, ikishindikana inabidi wakubali matokeo.
 
Nilifanikiwa kuishi USA na nchi mbili hivi za Amerika ya Kusini asikuambie mtu kama huna mishe za uhakika za hela bora usitoke hata mkoa ulikozaliwa maana hata unaweza chuma embe ukala ukalala. Huko nje gharama tu za kupata viza na vibali vya kuishi ni hela ndefu haswa ambazo hapa kwetu ni mtaji mzuri wa kuanzisha biashara. Kingine nilichokiona ukiwa huna hela kila mtu anakuona kama potential criminal na ukiwa nazo haswa nchi za Latinamerica basi kama ni mwanaume utakuwa kama mfalme maana waafrika wanapendwa mno huko haswa na wanawake kwa sifa zile za kijinga [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nchi gani ulizotembelea amerika kusini
 
Siku hizi huko ughaibuni napo pamejamba kama huku Tz tu.Mi nilichoamuaga ni ni kukomaa tu hapa nilipo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom