Mto_Ngono
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 686
- 589
"..why do you look so, look so, look so sad, Look so sad and forsaken?
Don't you know, when one door is closed, when one door is closed
Many more is open?.."Bob Marley - Coming In From The Cold
Mafanikio ni hatua, maisha ni safari yenye vikwazo vingi. siamini kama mwanadamu anaweza kuzaliwa akakua hadi kufikia utu uzima asikutane na vikwazo, hata mtoto anavyo vikwazo kipindi anazaliwa kutoka tu ni mthihani, kupumua hadi kufikia kutambua anakuwa kakutana na vikwazo vingi. Vipo vikwazo unavyojitengeneza mwenyewe, vikwazo kutokana na mazingira na vile vinavyotengenezwa na wengine. hivyo, unapokuwa na kuendelea kuishi katika akili yako lazima utegemee kukutana navyo. Suala la msingi ni je unapokutana navyo unahimili vipi? Hapa tunaangalia degree of tolerance na zaidi tunaangalia ni namna gani unaweza kukivuka hapa kinachoangaliwa ni brain capacity.
Sakata la vyeti feki limewakumba wengi sana huku likiwa na madhara makubwa kiuchumi, kijamii na kisiasa pia. Linaonekana kuwaumiza sana wahusika pengine wenda baadhi wamepoteza maisha japo hatujui idadi yake. Ni jambo ambalo laweza kumshtua mtu pale ambapo linatokea na hakujiandaa kwa muda huo japo alitakiwa kuwa na tegemeo la namna hiyo haswa pale ambapo alikumbuka kuwa vyeti vina figisu.
Wenye vyeti feki na umeondolewa kazini usikate tamaa kwa sababu utampa shetani smile. Shetani ana tabia hii, hukuingiza kwenye matatizo na akishaona yamekupata hukuacha na kukaa pembeni akicheka kuwa amekuweza. Sasa ili kumuonesha kwamba hajaweza usikate tamaa Uvumilivu kupita kwenye kipindi kigumu na uwezo wa akili ni vitu vinavyotakiwa kukusaidia.
USIKATE TAMAA "...Don't you know, when one door is closed, when one door is closed
Many more is open?.." yawezekana kwa kukuachisha kazi wamekuwahisha kwenye mafanikio, ulikuwa unachelewa sana kwa kukaa ndani lakini yawezekana pia wamekuepusha na matatizo ambayo yangeliweza kutokea baadae. Usilalamike wala usikate tamaa kila kitu kinatokea kwa sababu.
Tumia akili vizuri kwa kuweka mawazo endelevu, weka jitihada lakini kama una imani usisahau kutii imani yako mwisho utapata mafanikio. Use another door.