Colleagues,
Nimesikitishwa na tamko la Serikali kufungwa kwa mda kwa huduma ya mchungaji huyo huko Loliondo. Ukweli ni kwamba kama serikali ingekuwa makini vya kutosha ingekuwa tayari imetoa matokeo ya uchunguzi wake kwa wananchi juu ya dawa hiyo. Hapa nilipo nimeona ktk picha msululu wa magari mengi ya serikali yakiwa huko. Watumishi hawa tayari walisha pata dawa na hivyo wamekuwa tayari kutoa tamko wakiwa wameishahudumiwa. Nionavyo mimi and I would stand for my vision:
Serikali itoe tamko la uchunguzi wa dawa hiyo haraka ili huduma ziendelee au zisitishwe. Kama haiwezi kufanya hivyo haraka basi iache hali hiyo ya ki-IMANI iendelee kama ilivyokuwa huko nyuma. Itoe ulinzi na resources nyingine za kumwezesha mchungaji huyo kutoa huduma hiyo. Kama serikali haiwezi, Kanisa linaweza kufanya hivyo kwa utukufu wa Mungu mwenyewe.