Waliokoka naombeni muongozo wa kuacha dhambi kabisa

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,967
6,464
Kwa wale waliokoka, kuna hiki kitu, (uwezo wa kushinda dhambi) sasa kuna kitu huwa kinawekwa ndani na kukuzuia kabisa kutenda dhambi?

Ni kweli kijana mzizi akiona msichana kwa uwezo huo hatatamani? Au ni maamuzi tu binafisi ya kuacha dhambi? Maana duh!

Walokole nisaidieni please na muwe tu wakweli.
 
Nani kakuambia tukiokoka tunaacha dhambi kabisa? Kuachana na dhambi hadi mauti itufike. Kwani hutuoni kwa jinsi tulivyo na Majungu, chuki, majivuno ya kujifanya wenye haki kuliko wengine. Hayo yote ni mizizi ya dhambi. Subiri comments za walokole wenzangu uone chuki, majivuno, kejeli, kujikweza na dharau....nadhani jibu utalipata kupitia comments zao.
 
Nani kakuambia tukiokoka tunaacha dhambi kabisa? Kuachana na dhambi hadi mauti itufike. Kwani hutuoni kwa jinsi tulivyo na Majungu, chuki, majivuno ya kujifanya wenye haki kuliko wengine. Hayo yote ni mizizi ya dhambi. Subiri comments za walokole wenzangu uone chuki, majivuno, kejeli, kujikweza na dharau....

mkuu si kuna Roho mtakatifu huzuia kabisa uwezo wa kuona dhambi?
ngoja waje kweli
 
Mtu anaokoka kwaajili yakitu fulani akishafanikiwa basi, ila asilimia kubwa walokole kwa walokole hua wanaaminiana sana hata akimuona mtu ametoka gest na demu/jamaa hawezi amini kua anaweza kua amezini anakuambia huyu nimlokile a.k.a mtu wa mungu hawezi kuzini yaani wameaminiana sana...

kuna ndugu zangu walokole akikukopa ukimpa umerushwa halafu wanajiona waungwana yaani mungu niwakwao peke yao kila siku wanakushauri okoka utakua tajiri ila wao tapeli hawana kitu, siku moja wakamtuma mchungaji wao kwangu nikiwa kazini akaniambia rafiki yangu ukiokoka utapata wateja sana kwenye biashara zako, nikamuuliza kama kuokoka ndo kunaleta wateja mbona banana, viroba na bia zinanyweka sana kwahyo wauzaji wameokoka au wenye viwanda walokole
 
Mleta mada anataka umsaidie namna ya kuacha dhambi, LAKINI wewe umezungumza mambo mengine kabisa.

Nitarudi baadae kufundisha kitu..!
 
Dhambi unazo mwenyewe akilini mwako... Dhambi hushawishiwi kuzifanya.. Ni akili yako ndiyo inaamua... Ni tatizo kubwa sana duniani.. Na halina dawa...
 
"Mtu akifungua mlango mimi na Baba yangu tutakaa ndani yake" kwa hali ya kibinadamu huwezi kuishinda tamaa ya dhambi bila msaada wa Mungu.Hata hivyo kuna watu wengi sana waliojificha kwenye ulokole ili wafanikishe malengo yao.Hapo ndipo neno "waitwao ni wengi lakini wateule ni wachache". Ukiifahamu kweli itakuweka huru.
 
Ni kwa neema na rehema tu,siyo jambo la kujivunia sana maana kazi ya msalaba haikufanywa na wewe ila Yesu mnazareth..Soma waraka wa Paulo kwa warumi. Hutatoka mtupu.
 
Habari zenu wapenzi?
Naomba niongee kwa mtazamo wangu binafsi na pia kama mhanga wa jambo hili kipindi cha nyuma.

Kwanza kabisa wewe kukutana na walokole au wakristo wenye tabia mbaya ama chafu hakumfanyi Yesu kuwa mbaya. Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele.

Tunapokuja suala la kuacha dhambi, hili suala ni gumu kwa akili za kawaida hasa ukizingatia utamu wa mambo yale ambayo tunayaita au biblia imeyaona kuwa ni dhambi. Mfano kuzini, kusema uongo, kusengenya, kutapeli, chuki, husuda, uchafu na mengineyo.

Lakini Yesu wakati anaondoka alisema anatuletea msaidizi ambae atakuwa mfariji na kiongozi ambae ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu watu hudhani ni nguvu tu, la hasha! Ni zaidi ya nguvu, ni nafsi unayoweza kuzungumza nayo na mkajibishana vizuri kabisa. Hii inawezekana pale utakapoamua kujisalimisha kwake mzima mzima. Ukiamka asubuhi ongea nae au unapotaka kufanya jambo jibizana nae muulize kama unalolitaka ni sahihi na atakuambia.

Watu wengi hudhani Roho Mtakatifu ni kwa walio wa Kristo tu, ukweli ni kwamba Roho huyu ni kwa kila alie na mwili Yoeli 2:28. Na mara nyingi ni mpole ukimfukuza anakaa pembeni ukimwita anakuja na kuna muda anafadhaika kwa yale tunayoyafanya ila HATUACHI anakaa kando tu. Na ndio maana ni dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu pekee ndio isiyosameheka, Mungu Baba havumilii suala hili.

Unapotaka kuacha hicho kidhambi chukua hatua, jisalimishe kwake na atakuongoza cha kufanya. Tafuta sehemu ya utulivu tuliza akili yako mwambie Roho nakuita tuongee nae atakusikia. INAWEZEKANA. Mimi nilikuwa muongo sana mpaka nikawa najishangaa, hata sehemu ya kuongea ukweli nadanganya hata pasipo sababu ya msingi ila Roho alinipa nguvu nikajikuta i dont care...naongea ukweli unione mjinga au chizi nasema ukweli napoona sipawezi nafunga mdomo na kumuomba Roho anivushe.

Kuwa mkamilifu kabisa haiwezekani kwa sababu hata biblia inasema makwazo hayana budi kuja ila ole wao wanaoyaleta. Na tukisema hatuna dhambi twajidanganya. Ila kwa damu ya Yesu tunahesabiwa haki. Sijui umenielewa mleta mada....nimeandika sana nimechoka. Kama unataka zaidi njoo inbox tueleweshane taratibu.

Narudia tena, wewe kukutana na wakristo wazinzi, wasengenyaji, matapeli na wengineo hakumfanyi Yesu kuwa mbaya wala wokovu kuwa mbaya. Na hao wenye dhambi ndio aliowajia.

Usiku mwema.
 
Nani kakuambia tukiokoka tunaacha dhambi kabisa? Kuachana na dhambi hadi mauti itufike. Kwani hutuoni kwa jinsi tulivyo na Majungu, chuki, majivuno ya kujifanya wenye haki kuliko wengine. Hayo yote ni mizizi ya dhambi. Subiri comments za walokole wenzangu uone chuki, majivuno, kejeli, kujikweza na dharau....nadhani jibu utalipata kupitia comments zao.
Mmmmh naona kama umtumia akili yako kujibu wala hukuongozwa na roho wa Bwana.
 
Back
Top Bottom