BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Watumishi hao ni Dkt. Zakayo Kyomo ambaye ni Kaimu Mkuu wa chuo cha VETA, Projestus Kabyemela (Mhasibu), Waziri Shaban Waziri (Mgavi) na Upendo Aidan Nindi (Afisa Ununuzi).
Watumishi hao wanashitakiwa kwa Matumizi Mabaya ya Mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 329 na Shitaka la pili ni kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Milioni 22.8 kinyume na kifungu 284 A (1) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Washitakiwa walishindwa kupata wadhamini waliokidhi vigezo vilivyowekwa na kupelekwa Mahabusu, shauri hilo litatajwa tena Oktoba 13, 2022.
=======================
Watumishi wanne wa chuo cha Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) mkoani hapa wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Tabora wakikabiliwa na mashitaka mawili ya uhujumu uchumi.
Watumishi hao, Dk Zakayo Kyomo ambaye ni kaimu mkuu wa chuo hicho, Projestus Kabyemela (mhasibu), Waziri Shaban Waziri (mgavi) na Upendo Aidan Nindi (ofisa ununuzi), wamefikishwa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi mkoa Tabora, Jovin Alphonce Kato leo Septemba 29.
Mashitaka yanayowakabili maofisa hao ni pamoja na shauri la uhujumu uchumi Namba 36 la mwaka 2022 yaliyosomwa na wakili wa Takukuru, Yunis Masalu.
Katika shauri hilo, watumishi hao wanashitakiwa kwa matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi sura 329 na shitaka la pili ni kuisababishia mamlaka hasara ya Sh22.8 milioni kinyume na kifungu 284 A (1) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Masalu amesema makosa hayo yamefanywa katika kipindi cha Februari 22, 2022 na Mei 25, 2022.
Wakili wa washitakiwa hao, Kelvin Kayaga amesema kwa kuwa dhamana iko wazi, atahakikisha wanadhaminiwa.
Mahakama imeweka masharti ya dhamana kwa washitakiwa wote kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini nusu ya hasara huku mmoja wa wadhamini hao awe ni mtumishi wa Umma.
Hata hivyo, washitakiwa wameshindwa kupata wadhamini waliokidhi vigezo hivyo na kupelekwa rumande na shauri hilo litatajwa tena tarehe tena Oktoba 13 mwaka huu.
Kesi hiyo ni matokeo ya ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani humo, ambapo alikagua ujenzi wa chuo hicho na kubaini ubadhirifu ukiwemo ujenzi wa chumba cha mlinzi kwa gharama ya Sh11 milioni na kumwagiza mkuu wa Takukuru kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.
MWANANCHI