'Waliohukumiwa kifo watej wenzao'

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,137
'Waliohukumiwa kifo watej wenzao'
Written by Administrator
Thursday, 01 October 2009 07:12
Na Benedict Kaguo

MWENYEKITI wa Chama cha Albino nchini (TAS), Bw. Ernest Kimaya amesema kuwa watu watatu waliohukumiwa kifo kwa kumuua albino mkoni Shinyanga kabla ya kunyongwa hawana budi kuwataja washiriki wengine katika biashara hiyo.

Akizungumza jijini Tanga juzi, Mwenyekiti huyo alisema hatua ya kuwataja wenzao itaisaidia serikali kubaini mtandao wa biashara hiyo ambao wanaaminika kuwa ni watu
wenye uwezo kifedha.

Alisifu uamuzi huo wa mahakama na kumshuruku Rais Jakaya Kikwete kwa juhudi na ushirikano anaouonesha kwa kuiwezesha jamii hiyo kwa kumteua Mbunge wa Viti Maalumu Al-Shymaa Kwegyir kuwa mwakilishi wao.

Bw. Kimaya aliwataka watumishi wengine kwenye idara za serikali na mashirika binafsi kumuunga mkoni Rais Kikwete kwa kuthamini kundi hilo kwani lina wasomi wengi lakini bado halijaweza kuthaminiwa na kupewa nafasi kubwa za uamuzi zaidi ya kubaki kufanya kazi ya ualimu tu.
 
Muwe makini tu wasije anza kuwataja wabaya wao mkawaua watu wasio na hatia....
 
Back
Top Bottom