Sasa tunaongelea maridhiano, tunaongelea uponyaji wa Taifa, lakini unaliponya vipi Taifa bila kuyatambua majeraha? Kwa nini tusifuate mfano ule wa Afrika Kusini?
Waliotenda makosa, walitakiwa kujitokeza, walitakiwa kueleza uhusika wao katika maovu, kisha walikutanishwa na waathirika, waliomba msamaha, na mwisho walipewa hati ya kinga ya kutoshtakiwa kwa makosa waliyoyatubia.
Hapa kwetu, washiriki wote wa uharibifu wa uchaguzi wa 2020, wangejitokeza na kuweka wazi ushiriki wao.
Waliompoteza Ben Sanane, Azory, Kanguye, waliomshambulia Lisu, walioharibu uchaguzi wa ndani ya CCM kuwapata wagombea wa ubunge, waliowatengenezea watu kesi za uhujumu uchumi, waliopora pesa iliyoporwa toka kwa walioitwa wahujumu uchumi, n.k. Wote wangetakiwa kueleza kwa uwazi juu uhusika wao. Na wale ambao wasingejitokeza au kuficha ugusika wao, wangefikishwa mahakamani kama wahalifu.
Zoezi hili mwishowe lingewaacha huru, watuwaovu kama Sabaya, na watuhumiwa wengine kama Makonda, Mambosasa, Kalemani, Siro, Goodluck na wenzake, na wale majaji wa mchongo aliowatengeneza marehemu na kuwaingiza mahakamani kwa lengo maalum. Kwa sasa watu hawa, hakuna uhakika wa wao kutoshtakiwa siku moja kwa jinai wanazotuhumiwa.
Rais Samia, ufanye mchakato wa maridhiano kuwa halisia.