Walioharibu na kutumbuliwa kutopangiwa kazi nyingine; Kwanini Rais ameshindwa kuishi ahadi zake?

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
4,332
10,540
Rais Magufuli nakukumbusha tu kama mtanzania mwenzako, Kipindi cha kampeni ulituahidi kuwa mtu atakayekosea sehemu moja hutomuhamisha sehemu nyingine.Sasa ulianza kwa kumteua pProf. Mgaya, Leo kwa Mama Maleccela sasa Rais naamini wewe ni msema kweli.Tena huwa unasema msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Je, kwa hizi teuzi za walioharibu kuwaweka sehemu nyingine unahitaji niendelee kuamini kuwa wewe ni "msema kweli?" .

Au haya unauofanya sasa hivi ndio uliyoahidi?.

Rich Ze Best anaandika haya.

Unaikumbuka hii kauli tamu na yenye matumaini nyakati zile!?

“....., Unakuta mtu kaharibu Tarime anapelekwa Mwanza, akiharibu Mwanza anahamishiwa Tanga, kwenye serikali yangu hakutakuwa na utaratibu mbovu kama huo, ukiharibu sehemu moja ujue umeharibu maisha yako yote, kwangu ni kazi tu, ukiondoka umeondokahakuna kuhamishwa,” - John Pombe Magufuli, 11-09-2015, Tarime, Mara (wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu)

NAOMBA SASA KUULIZA; Jana, 21-01-2017 (mwaka 1 na mwezi 1 baadae) nakutana na habari ya kwamba, Anne Kilango Malecelaameteuliwa kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awali alitumbuliwa mkoani Shinyanga, (11-04-2016) kwa kosa la kudanganya kuwa mkoa huo haukuwa nawatumishi hewa (wakati huo Anne akiwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga),

(i) Je, Anne Kilango Malecela hakufanya kosa awali (kudanganya), wakati ule anatumbuliwakwa kuhusishwa na kudanganya kwenye taarifazake kwamba mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa, na alitumbuliwa kimakosa!?

(i) Je, Anne Kilango Malecela alisingiziwa nakutolewa 'kafara' kwenye hilo zoezi lawatumishi hewa hadi sasa kurejeshwa kwenyenafasi nyingine, tena kwa uteuzi kutokamamlaka ile-ile ambayo ilitengua uteuzi waawali kwa makosa ya 'kudanganya'!?

(iii) Kama ndivyo (wanakula matapishi yaowenyewe), sasa tunapaswa kuendelea kuamini kauli zote za hawa jamaa wa CCM na chamachao ambazo walizitoa kwenye kampeni zauchaguzi mkuu au tuwapuuze kabisa, nakuwaona nao ni 'wale-wale' kama wao wa siku zote!?

..., maana naona wanasahau haraka sana.., walisema katika ahadi zao kutakuwa hakunakitu kinaitwa 'mchakato-unaendelea' lakini hadi sasa sijaona ahadi ya milioni 50 kila kijiji ikitekelezwa, ukithubutu kuuliza, jibu la kwanza unalopata, 'mchakato-bado-unaendelea'..,

Ok.., hakuna shida, tumshukuru Mungu wetu ni mwema sana, tuendelee kumuomba uzima, atukopeshe ili tuendelee kuona maajabu ya ndimi-mbili yakitamalaki..,

Martin Maranja Masese (MMM)

Francis 12 nae anaandika haya .

Baadhi ya watu walivyochukulia uteuzi wa mama baada ya kufukuzwa kabla ya kuteuliwa tena. Didas Tumaini ametafakari kwa kutumia maandiko matakatifu 2Petro 2:22

Biblia inasema “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na “Nguruwe huoshwa na kurudi kugaa-gaa matopeni.” Tafsiri ya kiingereza (King James version) "The dog is turned to his own vomit again; and the sow that was washed to her wallowing in the mire."

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Aliyerudia matapishi sijui ni nani, na matapishi yaliyorudiwa siyajui. Mimi nimefikisha tuujumbe wa Didas. I dont know who is"matapishi" and who turned to his ownmatapishi. Tafuteni Biblia msome wenyewe.!
 
c3f6e595cc46a28d6b798466e2a2cef1.jpg

Kama kuna kingine sema
 
Huyu bwana ni kichaa/popoma wa hali ya juu,halafu watanzania wote ni kama wanaume wa Dar wanamuangalia tu.
Nimetafuta maneno ya kuongeza ili kuipa uzito hoja yako lakini nimekosa. Kumwangalia tu isingekuwa tatizo, kinacho-scare ni kuona anashangiliwa, anapigiwa makofi. Majuzi alikwenda bukoba na kuwatukana matusi ya nguoni na kejeli kemkem lakini watu hao hao kwenye mkutano na mitandaoni wanashangilia! Kwa kifupi Watanzania wote ti vichaa/mapopoma ya hali ya juu. Haishangazi tunayachagua mapopoma menzetu
 
uwezo kufikir na kutenda, wa uyu bwana, unareflect uwezo wa kufkir na kutenda wa wapga kula wake,
 
Wadau naomba kufahamishwa maana ya dhana nzima ya Utumbuaji Majipu unaoendelea katika Nchi Yetu.Binafsi nilikuwa naamini MTU mpaka anatumbuliwa jipu basi anakuwa amefanya vibaya katika eneo lake la Kazi hivyo anapoteza sifa Na kuondolewa Na hastahili kuwa mtumishi.Lakini pia kuna watu wametumbuliwa majipu lakini wamepewa Kazi nyingine tena kubwa zaidi ya awali.Kutokana Na hali hiyo naomba tutafute neno zuri ambalo likitumika halitaleta mkanganyiko kama huo nilioupata.Naomba tujadili neno zuri la kutumika.
 
nalitambua hivyo hapo mwanzo, kumbe muasisi wa utumbuaji ana maana zaidi ya hiyo

mliokaribu yake tunaomneni mtusaidie ili tupatiwe maana NA usahihi wa UTUMBUAJI MAJIPU
 
Tatizo sio wafuatiliaji wa habari..kumbuka Anna killango hakufanya ubadhirifu wowote ila alitoa taarifa bila kufanya utafiti wa kujiridhisha..na nyie mlitetea humu kuwa alidanganywa na walio chini yake..na rais aliahidi kumpangia kazi nyingine na ametimiza hilo..sasa povu la nini??
 
Huyu bwana ni kama alihaidi kupambana na watumishi wa umma na si miungu watu wateuliwa, hii imethibitika kupitia wengi walio chemka kwa kashfa alafu amewarudisha kama kina Kilango na wenzie, next time asituhaidi tena porojo zake
 
Back
Top Bottom