Waliogushi vyeti wana makosa matatu ya jinai

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Wadau nadhani wale wote wataothibitika wamegushi Vyeti huenda wakashtakiwa Kwa makosa 3.

1. Kugushi cheti
2. Kutoa taarifa za uongo Kwa mwajiri
3. Kujipatia mishahara.

Tunawatakia kila la Heri hao walioamua kugushi vyeti
 
Hii inamuhusu mkuu wa mkoa wa Dar Daud Bashite au kwa wauguzi na walimu???
 
Wadau nadhani wale wote wataothibitika wamegushi Vyeti huenda wakashtakiwa Kwa makosa 3.
Kugushi cheti
Kutoa taarifa za uongo Kwa mwajiri
Kujipatia mishahara.
Tunawatakia kila la Heri hao walioamua kugushi vyeti
mishahara halali yao wameitumikia japo wamefoji vyeti... maana hata bashittt ameambiwa achape kazi japo amechakachua makaratasi ya waliosoma kiukweli
 
Wauguzi wameokoa vifo vingi sana, walimu wamesaidia sana kuwaelimisha watanzania mpaka wengine wamekuja kua wahakiki vyeti. Mshahara wao ndo huo sasa maskini hawa hawana kazi tena wapo nyumbani wanasubiri kushtakiwa, mazuri yote waliyolifanyia Taifa yamefutika. Huyu mwingine analindwa eti kwa kua amewafichua wauza unga. Hii ndo double standard kila mtu aliwajibika kwa kadri ya nafasi yake aliyopewa basi na haki itendeke sawa kwa wote
 
Daudi Albert Bashite..
Mhalifu wa Taaluma na Jizi la Vyeti.

Jamani! Jamani! Muogopeni Mungu! Kitendo cha kuwaadhibu wote waliofoji vyeti bila kuangalia upande mwingine wa shilingi siyo sahihi. Watu hawa wana mchango mkubwa katika Taifa letu; kwani wametumia nguvu, akili na maarifa katika kulitumikia Taifa na wengi ni waadilifu. Mkosaji ana mazuri pia aliyoyafanya! Hata hivyo, waajiri wao pia walichangia watumishi hawa kuwepo hadi sasa, kwani wangefuata utaratibu wa ajira wa kuhakiki vyeti kabla ya kuwaajiri, yote haya yasingetokea! Hivyo basi, nashauri busara itumike, badala ya kuwaadhibu kama criminals, utumike utaratibu wa kuwapunguza watumishi serikalini (redundancy) ili ku-balance.
 
Back
Top Bottom