Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,522
- 22,457
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwepo na hali ya sintofahamu pale ambapo watu wapotea tu mitaani na vitongojini na baadae kuja kupatikana wakiwa hoi na taabani.
Wananchi hawa hukutwa maeneo hatarishi kama misituni na pembezoni mwa barabara huku wakiwa na majeraha makubwa kwenye miili yao na huenda majeraha hayo ni ya kudumu.
Natoa pendekezo kwa serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani na bunge kubadilisha sheria ya makosa ya jinai ili kuwapa nafasi wale wanokamatwa au kutekwa na polisi waweze kueleza wapi wapelekwa.
Yaani wa kifupi ni kwamba polisi/ wasojulikana na watu wa aina hiyo ni lazima watoe taarifa kwa mjumbe wa nyumba 10 pamoja na mwenyekiti wa serikali ya mtaa kuhusu kutaka kumkamata mtu yoyote waneona kwamba amevunja sheria.
Sheria hii pia izuie vyombo vya dola kuwasaka, kuwawinda na kuwkamata watu mitaani hovyo kwa kuwafunga vitambaa machoni na kuwapeleka kusikojulikana bila kibali maalum cha kamanda wa polisi wa Wilaya.
Sheria hii itamke kwamba watu wakamatwe rasmi majumbani ,au maofisini ambako wapo mashahidi.
Hiyo itasaidia uweka kumbukumbu sawa endapo kutatokea mtu kapotea kitaa na vitongojini.
Copy kwa waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Masauni.