Waliogawa Sanda Nachingwea ili Kudhibiti M4C Wafariki Dunia!

MgungaMiba

JF-Expert Member
Aug 28, 2011
999
815
Kifo kwa mwanaadam ni jambo la kuhuzunisha, linahusika zaidi na mipango ya Mungu, sio la kufurahia wala kubeza.

Lakini kuna mazingira mengine ingawa inawezakuwa ni mere coincidence lakini kwa akili za kawaida za kibinaadam, mtiririko wake unaweza kumkosesha mtu raha.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita, siku moja kabla M4C haijaingia Nachingwea, Mh Mbunge wa jimbo hilo Bw Chikawe alikuwa akigawa sanda kwenye misikiti ya Kata za jimbo lake kwa kutumia wasaidizi wake, Msimamizi mkuu wa shughuli hiyo alikuwa Ndg Fahida Mpoyo ambaye ni Diwani wa Kata ya Stesheni akisaidiana na Ndg Amani Rahisi maarufu "Bata".

Siku walipokamilisha shughuli hiyo ya kugawa sanda hizo jioni, usiku wake Chadema ikapata msiba mzito wa Muasisi wake Mzee Bob Makani, kwa hiyo Operation Sangara ikasitishwa, haikuingia Nachingwea kama ilivyopangwa, ingawa viongozi wachache walienda kuomba radhi kwa wananchi kwa dharura iliyotokea.

Cha kusikitisha wagawa sanda hao walijiona kama washindi fulani kutokana na kauli walizozitoa. Baada ya mazishi ya Mzee Makani J'5 iliyopita, juzi Ijumaa Mkuu wa kugawa sanda Mh Diwani Fahida Mpoyo, alifariki dunia, kwa hiyo Kata ya Stesheni, Wilaya ya Nachingwea iko wazi, cha kushangaza, (Mungu si Athumani) leo hii Ndg Amani Rahisi aka Bata, nae kafariki dunia, hivi tunavyoongea maiti yake bado iko kitandani ikisubiri kukamilishiwa faradhi zake.

Mtiririko huu wa misiba umezua Taharuki kubwa hasa kwa waliohusika na ugawaji wa sanda hizo, hasa muhusika mkuu aliezigharimia! Kwani kwa simple calculations za Law of Probability, unaweza ku determine anaefuatia anaweza kuwa ni nani. Tumuombe Mungu aepushe kusitokee maafa zaidi.

"WHAT GOES ROUND, COMES AROUND!"
 
Jamani hii kitu ni cha kweli?????, Mbona kama inatisha????... Wakuu Mods na Invisible ply your part to verify this issue.
 
Walikuwa wanajiandalia wenyewe, sasa bado mtoa wazo,na mgharamikiaji,

hakika mwenyezi mungu ni mwenyerehema hawezi kumwacha mja wake apate aibu
 
Uchuro huo kugawia binaadamu wenzako sanda. By simple logic unawaandalia kuzikwa.
 
Usishangae na mbunge akafuata
tusubiri tuone....
Itakuwa booonge la rahaaaa!
 
Badala ya kuandika RIP, nimejikuta nacheka hahahaha... Kama sinema vile, siasa za Bongo bana

Ni siasa au wazee wa kule wamechukia... Maana watu wana njaa wewe unawapeleka jeneza unategemea nini..
 
Back
Top Bottom