aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 776
- 1,121
1. Suala la CAF na taarifa ya jana ya kufutwa uanachama unadhirisha mambo mawili. Zanzibar ni nchi inayokubalika na mataifa zaidi ya hamsini barani Afrika iliopiyaliopigaga kura ya ndio miezi minne iliopita kutujumuisha nasi katika taasisi hii.
2. Kufutwa kwetu si kwa sababu ya Afrika kutokutukubali na kuyaona yanayotendekea ila kuna wakoloni waoga wengine wanaokhofia nao kupoteza makoloni walioyakalia kimabavu. Fikiri Umoja kama huu lakini kwa upande wa Ulaya majuzi imeikubalia uanachama kijimamlaka cha Gibraltar ambacho ni kimantik na kwa sheria zote ni sehemu ya Umoja wa Himaya ya Malkia wa Uingereza ikiwa na mamlaka yote ya kujiongeza yenyewe isipokuwa "Sovereignty" lakini ni mwanachama kamili. Tumefutiwa uanachama katika mkutano wa Moroco chini ya mamlaka ya Mwenyekiti mbuki, na ndio waliopiga kura ya hapana kutupinga uanachama tangu awali. Wameshindwa kuishawishi Afrika wamekwenda na ujecha, zaidi hakuna ridhaa baina ya "tuwaache walete waislam" na tunaotaka mabadiliko.
3. Kama mtafiti tazama tafauti za kijamii kwa kuzingatia wakati tukikubaliwa uanachama habari hizi zilikuwa na mvuto kwa nani na kusheherekewa na nani. Lakini halkadhalika wakati wa kufutwa mvuto ulikuwa wapi wa habari na masikitiko yalianzia wapi. Nikitegemea kabisa kwa mamlaka husika katika taarifa ya jana nao wangejitokeza pande zote mbili na kutoa maelezo na hatua za kuchukua ukizingatia sababu tulizokubaliwa kujiunga na kufutwa zina mchanganyiko mkubwa hasa katika masuala ya kisheria. Pande zote za mamlaka kimnya, hivi maraika na genge lake waliridhia au yalikuja bila ya kutegemea? Na kibatari chetu kimejaa moshi, hakifurukuti, wakti wa neema hauji kwa wasio na ridhaa ya uongozi. Tumegusa, tumenusa na kuonja ladha ya utambulisho na furaha ya kujulikana, ari izidi hasa mpaka tufike lengo, tunaweza.
4. La mwisho ni kuwa tuboreshe kwanza mfumo wa michezo visiwani na kuhakikisha tumesonga mbele. Nakumbuka kipindi cha Small Simba, Malindi, Kiski, Miembeni, Jamhuri nk. Hatukuwa na habari ya CAF lakini tulikuwa na mvuto mzuri wa masuala ya michezo. Nahisi hili la CAF ni Mungu tu kataka kuwadhihirishia samaki kwamba huwezi ukawa huku na kule na dunia ikutazame tu.
5. Njia ni moja tu nayo ni mabadiliko ya mfumo wa muungano utaotupa fursa kila upande wa kukubaliana kwa ridhaa zetu ya kushirikiana tunayoyataka na kutuacha tukiwa na utambulisho wa kifursa hasa katika masuala ya kimataifa na taasisi za kimataifa. Inafurahisha waliokata viuno Bunge la katiba, ndio wanaolia leo kwa msimamo wa CAF. Bila ya ridhaa ya waliokuchagua kuwaongoza, utafikia tu ukuta maana Mungu atakusuta tu kuanzia ndani ya nafsi na kwa matukio ya namna hii kwa sababu unafik hauna mwisho mwema. Mabadiliko yanakuja na yakifika tutarejesha heshima ya visiwa hivi vinavyofanyiwa juhudi kubwa kuwa manispaa isiojitambua. Hata uchaguzi tatizo si sisi wazanzibari kama tunavyoaminishwa, tatizo nafikiri kwa sasa linatambulikana.