Mayu
JF-Expert Member
- May 11, 2010
- 6,637
- 10,723
Wakuu,
Naona nyuzi mbalimbali za watu wakielezea jinsi walivyoangukia pua baada ya kuingia kwenye kilimo na ufugaji. Hii inawafanya wengi kukata tamaa na kilimo na ufugaji.
Binafsi nilianza kwa kulima mahindi 2015 eka 10 nikaishia kupata gunia 33, siku pata hasara nilirudisha pesa yangu baada ya kuyaweka mahindi stock hadi bei ilipopanda. Mwaka 2018 nikalima alizeti eka 10 nikafeli vibaya, niliambulia gunia 18.
Mwaka jana kwa milioni 3 nikalima vitunguu maji kama ekari 5, mwezi 2 nikauza gunia 25 kwa 520,000 baada ya mahesabu yote nilitengeneza faida kama milioni 10.
Baada ya kunogewa nikalima tena kitunguu cha kumwagilia na nikatumia kama milion 4, sasa hivi navuna tatizo gunia limeshuka hadi elfu 60.
Nimekuwa na ups and down lakini madalali ni tatizo.
Pesa ipo sana tatizo ni timing na soko la uhakika na madalali uchwara na siku mkisikia dalali kapigwa risasi ya kicha na mkulima mjue ni mimi.