Waliofanikiwa katika kilimo na ufugaji share uzoefu wako hapa

Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
6,491
10,485
Wakuu,

Naona nyuzi mbalimbali za watu wakielezea jinsi walivyoangukia pua baada ya kuingia kwenye kilimo na ufugaji. Hii inawafanya wengi kukata tamaa na kilimo na ufugaji.

Binafsi nilianza kwa kulima mahindi 2015 eka 10 nikaishia kupata gunia 33, siku pata hasara nilirudisha pesa yangu baada ya kuyaweka mahindi stock hadi bei ilipopanda. Mwaka 2018 nikalima alizeti eka 10 nikafeli vibaya, niliambulia gunia 18.

Mwaka jana kwa milioni 3 nikalima vitunguu maji kama ekari 5, mwezi 2 nikauza gunia 25 kwa 520,000 baada ya mahesabu yote nilitengeneza faida kama milioni 10.

Baada ya kunogewa nikalima tena kitunguu cha kumwagilia na nikatumia kama milion 4, sasa hivi navuna tatizo gunia limeshuka hadi elfu 60.

Nimekuwa na ups and down lakini madalali ni tatizo.

Pesa ipo sana tatizo ni timing na soko la uhakika na madalali uchwara na siku mkisikia dalali kapigwa risasi ya kicha na mkulima mjue ni mimi.
 
Faida ipo shida ni kutokuwa na consistence katika kufanya jambo , leo unalima hiki kesho kile , keshokutwa kile.

Kwa uzoefu wangu niliwahi kulima mahindi ya pop msimu wa kwanza nikawa nimechelewa yakawa hayako katika standard nzuri nikayaunza wenyewe kwa kuchoma bis nikapiga hela nzuri tu ila msimu uliofuata nikayapanda kwa wakati na kuzingatia abc zake nikatengeneza pesa ambayo sikuitegemea kabisa tatizo likawa ni kwamba nililima kiasi kidogo sana kuliko msimu wa kwanza yaani nikabaki naombwa mzigo najificha

Ipo hivi pia kilimo bila kuwa na stoo kitakutesa na utaona hakilipi ila kinalipa vizuri tu ni suala la kuwa na akili nzuri tu ya kufanya jambo sahihi kwa wakati sahihi.
 
Faida ipo shida ni kutokuwa na consistence katika kufanya jambo , leo unalima hiki kesho kile , keshokutwa kile
Kwa uzoefu wangu niliwahi kulima mahindi ya pop msimu wa kwanza nikawa nimechelewa yakawa hayako katika standard nzuri nikayaunza wenyewe kwa kuchoma bis nikapiga hela nzuri tu ila msimu uliofuata nikayapanda kwa wakati na kuzingatia abc zake nikatengeneza pesa ambayo sikuitegemea kabisa tatizo likawa ni kwamba nililima kiasi kidogo sana kuliko msimu wa kwanza yaani nikabaki naombwa mzigo najificha

Ipo hivi pia kilimo bila kuwa na stoo kitakutesa na utaona hakilipi ila kinalipa vizuri tu ni suala la kuwa na akili nzuri tu ya kufanya jambo sahihi kwa wakati sahihi.

Bado unalima?
 
Na mimi nina mpango wa kulima kilimo cha kumwagilia, hasa kilimo cha mahindi mabichi, Target market yangu iwe DSM. Ila bado nina wasi wasi
 
Mkuu unalima mkoa gani na wapi....kijiji/wilaya/kitongoji kipi?
Je,maji yapo ya kutosha huko kwa ajili ya umwagiliaji?
 
Kilimo hakiitaji kukata tamaa, mara zote bei inaweza kuwa sawa au isiwe sawa kwa kila msimu. Mwaka jana nyanya mwezi huu ilikuwa 8000 tena kwa kutafuta wateja.

Now imeanza kupanda sasa ni 20,000 Shamba. Ukiwa na mtaji lima vizuri uwe na product ya ukweli, bei itajulikana wakati huo.
 
Wadau njooni mtoe maoni, maana wengine tunajifunza kwa maoni ya wadau waliofanikiwa.
 
Wakuu,

Naona nyuzi mbalimbali za watu wakielezea jinsi walivyoangukia pua baada ya kuingia kwenye kilimo na ufugaji. Hii inawafanya wengi kukata tamaa na kilimo na ufugaji.

Binafsi nilianza kwa kulima mahindi 2015 eka 10 nikaishia kupata gunia 33, siku pata hasara nilirudisha pesa yangu baada ya kuyaweka mahindi stock hadi bei ilipopanda. Mwaka 2018 nikalima alizeti eka 10 nikafeli vibaya, niliambulia gunia 18.

Mwaka jana kwa milioni 3 nikalima vitunguu maji kama ekari 5, mwezi 2 nikauza gunia 25 kwa 520,000 baada ya mahesabu yote nilitengeneza faida kama milioni 10.

Baada ya kunogewa nikalima tena kitunguu cha kumwagilia na nikatumia kama milion 4, sasa hivi navuna tatizo gunia limeshuka hadi elfu 60.

Nimekuwa na ups and down lakini madalali ni tatizo.

Pesa ipo sana tatizo ni timing na soko la uhakika na madalali uchwara na siku mkisikia dalali kapigwa risasi ya kicha na mkulima mjue ni mimi.

Kilimo cha msimu kinatesa sana, ndipo nikaamua nilime mazao ya kudumu! Nilitafuta hekari 120 nikapata, nimepanda mikorosho yangu kisasa kabisa!

Hapo nina uhakika kila mwaka kupiga pesa, itavuruga mwaka huu na mwaka kesho lakini mwaka keshokutwa nitapata tuu!

Nimepata hekari zingine 150 mahali, nipo kwenye hatua za mwisho kuhamishia miche ya parachichi kutoka kwenye vitalu! Yaan zinaumiza gharama lakini sijali, nitatoboa tu muda utapofika!

Mawazo haya niliyasoma humu humu! Nikaachana na vilimo vya msimu
 
Ukilima kwa ufasaha kabisa kwa hekari moja ya mahindi inaweza kukupa kiasi gani ( in terms of gunia?)
 
Kilimo cha msimu kinatesa sana, ndipo nikaamua nilime mazao ya kudumu! Nilitafuta hekari 120 nikapata, nimepanda mikorosho yangu kisasa kabisa!

Hapo nina uhakika kila mwaka kupiga pesa, itavuruga mwaka huu na mwaka kesho lakini mwaka keshokutwa nitapata tuu!

Nimepata hekari zingine 150 mahali, nipo kwenye hatua za mwisho kuhamishia miche ya parachichi kutoka kwenye vitalu! Yaan zinaumiza gharama lakini sijali, nitatoboa tu muda utapofika!

Mawazo haya niliyasoma humu humu! Nikaachana na vilimo vya msimu
Hongera sana mkuu, hiyo investment kubwa sana ,
 
Wapi unalima parachichi mkuu na mashamba yanapatikana huko.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom