Waliodai wana uwezo wa kumfufua mtoto kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliodai wana uwezo wa kumfufua mtoto kortini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jamadari, Apr 28, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WAKAZI wawili wa Jiji la Dar es Salaam jana wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya Kinondoni wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha baada ya kudai kwamba wana uwezo wa kumfufua mtoto aliyekufa. Akiwasomea hati ya mashtaka mahakamani hapo, mwendesha mashtaka Nassoro Sisiwaya mbele ya Hakimu Suzane Kihawa, alidai watuhumiwa kwa pamoja walijipatia fedha tasilimu Sh 3.6 milioni kutoka kwa Amina Juma kwa makubaliano kwamba wana uwezo wa kumfufulia mtoto wake aliyekufa. Washtakiwa hao ni Shabani Juma (46), mkazi wa Tandale kwa Tumbo mganga wa asili na Godfrey Zakaria (26) mkazi wa Tandale fundi wa umeme wa magari. Sisiwaya aliieleza mahakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo, Mei 5 mwaka jana katika eneo la Kimara Baruti na kwamba walidai wanauwezo wa nguvu za kichawi za kuweza kumfufua marehemu huyo na kumrudisha akiwa hai. Mwendesha mashtaka huyo alisema upelelezi katika shauri hilo umekamilika na kesi hiyo, itaanza kusikilizwa Mei 17 mwaka huu. Washtakiwa wako nje kwa dhamana. Katika tukio lingine mkazi wa Mbezi Juu jijini Dar es Salaam God Msishiri (31) amepandishwa kizimbani akikabiliwa na shtaka la wizi wa kutumia silaha. Akisomewa hati ya mashtaka na mwendesha mashtaka Nassoro Sisiwaya mbele ya Hakimu Suzane Kihawa alidai mshtakiwa aliiba bastola aina ya Star 9.0mm ikiwa na risasi 30. Mshtakiwa alirudishwa rumande hadi Mei 17 shauri hilo litakapotajwa tena mahakamani hapo. http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/1072-waliodai-wana-uwezo-wa-kumfufua-mtoto-kortini
   
Loading...