Taarifa ya vifo vya watu wawili waliobanwa na roli kwa zaidi ya masaa 16 iliyotangazwa leo na ITV inasikitisha sanasana.
Jana ITV waliwaonyesha watanzania hao wakiwa wamebanwa na mizigo, huku wakiwa kwenye maumivu makali waliomba msaada kwa serikali yao sikivu ya CCM, cha kushangaza hakuna msaada wowote uliotolewa. Kamanda alijaribu bila mafanikio kuomba gari la kuinua mizigo winch.
Hivi serikali ilishindwa kutoa msaada wa haraka kwa kupeleka winch kwa zaidi ya masaa 16 au walifanya makusudi maana walionaswa kwenye tukio walikuwa walalahoi?
Hivi angekuwa kigogo amenaswa au fisadi papa kanaswa si wangepeleka winch kwa Helikopta? Watanzania umefika wakati wa kujiuliza,hivi serikali ya sasa ya CCM inajali usalama wa watanzania walalahoi?
Nini kifanyike ili watanzania wote tuwe na uhakika wa kupata msaada tunaouhitaji toka serikali sikivu ya CCM pale tunapokumbana na majanga?
Imeniuma sana aisee maana jana niliwaona wakiongea kwenye tv leo hatunao,lkn ingekuwa mtu ,wenye title tungeona hata meli za kijeshi maseyu zikitoa msaada. RIP comradesHii nchi ya ajabu sana,watu wamebanwa ndani ya ajali iringa baada ya malori kugongana,zaidi ya masaa 8,hakuna huduma ya kuwanasua,jana walikua wanaongea na kuomba msaada,leo tunaambiwa wamefariki.Hata dripu wangewekewa hapo hapo kwenye ajali wakati wanasubiri kunyofolewa.tanroads kazi kupima uzito tuu?kwa nini wasiwe na crane la kunyanyua magari kila baada ya umbali fulani?