Walioahidi kuiua CHADEMA kabla ya 2020 wako wapi?

Ni aibu kwao
 
Kwani chadema ipo?
 
Ndio kivysa piga mateke ya kukata pumzi
Huoni aibu kupambana na Chadema, kwa kutumia vyombo vyako vyako vyote vya dola?

Ngoja nikutajie vyombo vyako vichache viliivyoamua kufanya "coalition" na CCM

Jeshi la Polisi, Tume ya uchaguzi, TAKUKURU, Immigration, Msajili wa chama, Mahakama, TISS, kwa kuvitaja vichache

Hata hivyo bado mmeshikwa na bumbuwazi kuiona Chadema inaendelea "kudunda" kwa uwezo wa Mungu!
 
Mods futeni tena nimewazoea
 
CHADEMA ipo jf, tweeter, fb na IG...kule field ambako ndiko inakotakiwa kuwa haipo, kule field CHADEMA imekufa, October sio mbali uzi huu nitaufukua.
 
Mimi nafikiri CCM kama wanaamini CDM inakufa wangeiacha ijifie yenyewe badala ya kuikandamiza kwa kutumia vyombo Vya Ulinzi na usalama.Mgonjwa aliye mahututi kwanini umpige tena risasi ya kichwa si umuache tu ajifie mwenyewe?
 
Hicho chama kilishakufa mkuu, unajidanganya tu.
 
Mwaka 2020 umeisha ?kumbe unakili kisoda hivi
Kununua viongozi haiwezi ua upinzani na faida waliyo nayo upinzani ni kwamba kwa kuto kuoneshwa live bunge na kuzuiwa mikutano ya hadhara imesaidi chama kwa wabunge kushindwa kuji brand hivyo wabunge wengi viti maalumu hawajulikani,na pia wa majimbo wanafahamika majimboni kwao tu,kwa hiyo ile impact ya kitaifa haiwezi tokea.
 
Mimi nafikiri CCM kama wanaamini CDM inakufa wangeiacha ijifie yenyewe badala ya kuikandamiza kwa kutumia vyombo Vya Ulinzi na usalama.Mgonjwa aliye mahututi kwanini umpige tena risasi ya kichwa si umuache tu ajifie mwenyewe?
Vyombo vya ulinzi na usalama ndo vinavyowafungua macho wananchi waone maajabu yalofanywa na JPM kwa kujibu hoja zote za upinzani ndani ya miaka 5? ni vyombo vya ulinzi na usalama ndo vilowafanya CHADEMA na Zitto kuungana na maadui wa Taifa na kutubetray katika vita vya kiuchumi? ni vyombo vya ulinzi na usalama vinavyowafanya waishi maisha ya kihuni kinyume na maadili ya viongozi wa umma kwa kulewa chakali, kuumia na kusingizia serikali? Haya ni baadhi tu ya mambo yalofanya wasiaminike tena.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…