Walinzi wa Suma JKT hawajui wajibu wao

David Goliath

JF-Expert Member
May 16, 2018
929
1,798
Aisee jana nimeponea chupuchupu kuzirusha na Walinzi wa SUMA JKT, ipo hivi mimi ni dereva Bajaj sasa kuna abiria wangu huwa nampeleka ofisini na kumfata, jana akaniambia kapata dharura haendi kazini ila akanipa laptop nipeleke ofisini kwao na namba ya muhusika ambaye anatakiwa kupelekewa hiyo laptop akanipa, nilipofika pale nikampigia simu akaniambia ametoka kidogo hiyo laptop niwaachie Walinzi hapo getini nilivyo maliza kuongea na simu kuna mlinzi wa kike akaniuliza kasemaje?

Nikamjibu kasema niwaachie nyie Walinzi anakuja kuichukulia hapa aisee yule mdada akaanza wewe usirudie tena kutuita Walinzi, nikauliza nyie ni wakina nani?

Akawa ananiambia uwe na heshima usitake kubishana na mimi tukazozana pale wale wengine nao wakaingilia nikawaambia nyie ni Walinzi kama hamfanyi kazi ya ulinzi ondokeni hapa mmoja akamwambia wenzake eti huyu ni wakumpa materials za kijeshi Ili atuelewe nikawaambia hilo haliwezekani mkitaka kuhatarisha ajira yenu mniguse kisa nimewaita Walinzi nikawasha zangu Bajaj nikaondoka.

Nilishangaa sana hawa jamaa sijui ndivyo wanavyoambiwa huko na wakubwa zao au ni uelewa mdogo.
 
Mlinzi ni babu masai tu, hao waliopitia mafunzo ukiwajumlisha na Garda na hizo security companies nyingine + hao suma JKT wote ni askari ‘kitaalamu hiko hivyo.

Sisi tu watanzania na tabia zetu mbaya ndio tunawaita walinzi.
 
Bongo kweli pamefilisika.

Ulaya mpaka mwanajeshi wanamwita mlinzi ila Bongo mtu anataka aitwe askari au afisa. Ok.

Sisi job walinzi wenzangu wanahangahika sana kulikwepa hilo jina la mlinzi. Ila ukweli ni kwamba kama umeajiriwa kusimamia usalama wa mtu, mahali, ofisi au nchi wewe ni mlinzi.
 
Mlinzi ni babu masai tu , hao waliopitia mafunzo ukiwajumlisha na Garda na hizo security companies nyingine + hao suma JKT wote ni askari ‘kitaalamu hiko hivyo.

Sisi tu watanzania na tabia zetu mbaya ndio tunawaita walinzi.
Unajua maana ya mlinzi? Hao JWTZ wenyewe wanaitwa Walinzi wa Taifa ndiyo maana namba zao zinaanza MT
 
Mlinzi ni babu masai tu , hao waliopitia mafunzo ukiwajumlisha na Garda na hizo security companies nyingine + hao suma JKT wote ni askari ‘kitaalamu hiko hivyo.

Sisi tu watanzania na tabia zetu mbaya ndio tunawaita walinzi.
Wewe ndio unachanganya mambo. Babu wala masai sio mlinzi, huyo ni gate man au gatekeeper. Waliopewa mafunzo ya ulinzi ndio hao G4S na hao Suma JKT
 
Hapo kweli walinzi wamezingua,halafu hao walinzi wa Suma JKT Wana Tatizo Gani maana watu Wana malalamiko mengi sana kuwahusu Hiyo kampuni ijiangilie maana raia washaanza kuwasagia kunguni mitandaoni
Wasipochukua hatua watajua hawajui Kwa biashara Yao!
 
Mlinzi ni general term na kwa kiingereza ni protector
Mlinzi ni mchungi wa usalama wa eneo fulani.. Na hapa ndio tunapata tafsiri ya neno security guard
Ulinzi na mlinzi ni nafasi ya kaliba ya juu sana
Mungu ni mlinzi wetu kupitia guardian angels (malaika waangalizi)
Baba ni mlinzi wa familia
Hakimu ni mlinzi wa amani nknk
 
Mlinzi ni babu masai tu , hao waliopitia mafunzo ukiwajumlisha na Garda na hizo security companies nyingine + hao suma JKT wote ni askari ‘kitaalamu hiko hivyo.

Sisi tu watanzania na tabia zetu mbaya ndio tunawaita walinzi.
Kwa hiyo wewe naye ni mlinzi au umeamua kuwatetea askari wenzako?
 
Suma wana tabia hizi:

Ubabe, ujuaji, umbea na uchonganishi maofisini, wagombanishi halafu majungu. Anaweza kukufokea bila sababu ya msingi. Hopeless guards!
 
Ndugu yangu nakusihi usibishane nao siku nyingine watakupiga wakuue, sio kwamba nawaogopa hapana ila hata mimi nilikuwa mlinzi wa Suma Jkt. Kilichopo ni kuwa wengi wa wale walinzi ni vijana kutoka jkt ambao wengi tulikuwa na matumaini ya kuajiriwa na jwtz kwa hiyo unapomuona pale getini sio kwamba kapenda kufanya kazi ile hapana ni kukosa tu kazi kwa hiyo anaishi katika msongo wa mawazo.

Sasa wewe jichanganye hasira zao wakumalizie wewe, kila siku unasikia watu wanauawa na hao sumajkt halafu wewe unajipeleka tu. They have nothing to loose.
 
Kwa hiyo Askari sio mlinzi. Hapo umetaja security companies kwa kiswahili si ndio kampuni za ulinzi. Hivi hizo Shule mnaenda kusoma utaahira!

Kweli elimu ya TANZANIA ni ujinga.
Na huo ndio ukweli. Hawa wanaita chepeo kuwa ni kijiko kikubwa. Chepeo itabaki kuwa chepeo tu.
 
Ndugu yangu nakusihi usibishane nao siku nyingine watakupiga wakuue, sio kwamba nawaogopa hapana ila hata mimi nilikuwa mlinzi wa Suma Jkt. Kilichopo ni kuwa wengi wa wale walinzi ni vijana kutoka jkt ambao wengi tulikuwa na matumaini ya kuajiriwa na jwtz kwa hiyo unapomuona pale getini sio kwamba kapenda kufanya kazi ile hapana ni kukosa tu kazi kwa hiyo anaishi katika msongo wa mawazo.
Sasa wewe jichanganye hasira zao wakumalizie wewe, kila siku unasikia watu wanauawa na hao sumajkt halafu wewe unajipeleka tu. They have nothing to loose.
Acha kuwapa kichwa hao wajinga.

BODABODA zinaua watu kila siku na bado wanazipanda. Hao JKT Kama wanaua watu sio sababu ya kuwaogopa. Ndio maana mnarogwa sio kila mtu ni wa kupelekeshwa.

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Mlinzi ni babu masai tu , hao waliopitia mafunzo ukiwajumlisha na Garda na hizo security companies nyingine + hao suma JKT wote ni askari ‘kitaalamu hiko hivyo.

Sisi tu watanzania na tabia zetu mbaya ndio tunawaita walinzi.

Ni walinzi tu
 
Back
Top Bottom