Walimu watelekeza shule, watimkia mgodini kuchimba dhahabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu watelekeza shule, watimkia mgodini kuchimba dhahabu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 21, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Walimu watelekeza shule, watimkia mgodini


  na Sitta Tumma, Mwanza


  [​IMG]
  WALIMU wa Shule ya Msingi Nyakunguru B iliyopo katika Kijiji cha Nyakunguru, Kata ya Kibasuka, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, wametelekeza kazi yao na kutimkia katika mgodi wa dhahabu wa Itandura kwa ajili ya kuchimba madini.
  Wanadaiwa kukimbilia mgodini hapo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni maisha magumu, hali ambayo imewafanya muda mwingi washindwe kufundisha ipasavyo.
  Vyanzo vya habari kutoka mgodini hapo vimeieleza Tanzania Daima kuwa, walimu hao wamekuwa wakifika mgodini nyakati tofauti, huku baadhi yao wakiapa kutoendelea na kazi yao ya kufundisha wanafunzi shuleni.
  Kwa mujibu wa habari hizo, shule hiyo inadaiwa kuwa na walimu wanne, lakini wote wamekacha kazi hiyo na kujiunga na wachimbaji wadogo na kuwaacha wanafunzi wakishinda madarasani bila kufundishwa.
  “Mimi namiliki mashimo kwenye mgodi huu wa Itandura na ninapozungumza na wewe, wapo walimu kutoka Shule ya Nyakunguru wanachimba dhahabu na tunapata fedha nyingi tu.
  “Lakini cha kushangaza tunapowauliza juu ya kazi yao ya ualimu, wanasema kazi hiyo haina maslahi na serikali imewasahau wanaishi maisha ya tabu,” alisema mmoja wa wachimbaji katika mgodi huo.
  Aidha, inadaiwa kwamba walimu hao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wanafunzi kwenda kuchimba madini mgodini hapo.
  Mmoja wa walimu wa shule jirani ya Nyakunguru A, alithibitisha kuwapo kwa hali hiyo na hata yeye huenda machimboni siku za Jumamosi na Jumapili.
  “Hata mwenyekiti wa kijiji yupo hapa tunachimba naye dhahabu, na wananchi wenye shida za kiofisi dhidi ya mwenyekiti, wanalazimika kuja huku machimboni kuonana naye,” alisema mwalimu huyo. Ofisa Elimu wa Wilaya ya Tarime, Emmanuel Johnson, alipoulizwa kwa njia ya simu juu ya madai hayo, alisema hana taarifa za walimu wake kutimkia machimboni. “Mimi sina taarifa juu ya hilo, na anayepaswa kuzungumzia suala hilo ni Mkurugenzi wa Halmashauri kwa sababu ndiye msemaji mkuu wa halmashauri yetu,” alisema ofisa elimu huyo.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  kazi unayo kikwete....!!!!
   
 3. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kila mtu anahaki ya kuamua aina ya maisha anayotaka kuishi kama walimu hawa wameona watatoka kwa kuchimba dhahabu heri wakafanya hivyo kuliko kuendelea kusubiri maisha bora kwa mtanzania kupitia mishahara ya ualimu na inaweza kuwa fundisho kwa serikali kuwapa umuhumu wao kama wanavyostahili.
   
 4. G

  Ghati Makamba Member

  #4
  Nov 21, 2009
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tukubaliane kwamba hapa Tanzania baada ya Uhuru toka kwa watu weupe, walipatikana wazungu weusi ambao waliona pana haja ya kuendelea kutumiwa kwa mifumo ya unyonyaji bila kujali umuhimu wa idara kadhaa ambazo ni mihimili ya ustawi wa Taifa letu. Kuna haja ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ili kila mmoja wetu asihisi kunyonywa ndani ya nchi yake, tofauti na hapo, tutapishana sana kwenye hizi idara zetu zisizo na uwezo wa kufungua milango ya mafanikio kimaisha.
   
Loading...