Mwandishi HIllary Shoo anaripoti kutoka Singida kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji (MO) amewashangaza walimu wa shule za Msingi Manispaa ya Singida pale alipowapa posho ya shilingi 50,000 kila mmoja wakati wa hafla fupi ya kuzungumzia changamoto zinazowakabili walimu hao.