Walimu wanavyoibiwa na CWT & PSPF

nlitegemea mapambano makal baada ya walimu wenye digrii kuongezeka kuanzia miaka ya 2005 nikiamin kuwa watapambana kisom zaid lakin hamna lolote
Kwa kweli ni bahati mbaya kabisa, japo hao walimu wenye digrii wameongezeka kama ulivyo sema lakini wanaongozwa na msukumo wa ndani wa hofu huku wakikumbana na matishio mengi ya kukatiwa mshahara, kufukuzwa kazi n.k,iwapo watajaribu kupigania haki zao as if hawakusoma na kwamba maisha yao yote yameambatana na hiyo kazi ya ualimu tu.
 
Nimeamua kuwatetea walimu manake imeonekana ni sector ilidharaulika kuliko hata udereva
Unawatetea walimu wa wapi Kenya au Tanzania? Kuna post zako humu JF ulishswahi kuukana utanzania sijui kwa sababu umeolewa Mombasa.
 
CWT ni tawi la ccm baada ya uwt. Haiingii akilini miaka nenda rudi cwt hakijaweza kujenga majengo yake yenyewe wilaya zote hadi sasa. Kimsingi inabidi wafanye mabadiliko ili kuwalipa walimu kiinua mgongo au hata warejeshe 55% ya michango ya mwanachama. Hii inaweza kuwatia moyo walimu.
 
Chuoni kwetu walikuja wanaojiita raawu na kuomba hy 2%. Nikasema 2% my foot sijiungi. Sisi inafuu wetu ni kwamba kujiunga ni hiari. Nadhan ifike point hata cwt iwe kujiunga ni hiari. Ikiwa hvy hata benefits baada ya kustaafu zinakua lucrative. 2% kwa mwezi kwa walimu wote hao ni kubwa. Bora wangesema 50000 kwa mwaka. Mbaya zaidi ukiwa na madai yako serikalini wao watakwambia gomeni serikali iwasikilize. Kama soln ni kugoma, cwt inaexist kwa sbb gani. Hizi labour unions nyingi zipo kwa ajili ya viongoz wa unions na sio maslahi ya wachangiaji
 
je utetezi wa shida za walimu ni kwa percentage ? CWT ni majizi ya mishahara ya walimu.hawana utetezi wowote kwa walimu.ni chombo cha wanasiasa cha kuwazuga na kuwakejeli walimu.
 
Walimu wanapaswa kuwekwa kwenye kundi la special group kwa kutojitambua licha ya kuwa sie wengine tumeamua kuvaa mabomu kuwatetea
Walimu ni waoga sana, sijui kwa nini? Utafikiri huko vyuoni wanafundishwa kozi ya woga pia ili wafikapo makazini wai-apply. Mimi nina ndugu yangu wa karibu, ana first digrii na ni mwalimu lakini mwoga sana na ni tegemezi mno kimawazo mpaka huwa nashangaa. Sijui tuwasaidieje!
 
Unawatetea walimu wa wapi Kenya au Tanzania? Kuna post zako humu JF ulishswahi kuukana utanzania sijui kwa sababu umeolewa Mombasa.
We jamaa baada ya mamako kufutwa ukuu wa mkoa umeanza ulevi sasa usio na tija

Mbona huna hoja ya msingi?kwani kuwatetea walimu ni lazima wawe wa tz au ke?
Elimu elimu elimu
Lumumba hili neno elimu litawatafuna mno,ni msamiati mzito mno kwenu
 
Hata hili sakata la watumishi hewa ,CWT wanahusika ....kwanza wao wanakuwa na idadi ya walimu ,hawakuitaarifu hata serekali kuhusu hao walimu hewa ?? Au walinyamaza ili wavute mkwanja tu.......pia kuhusu bank ya walim niliona ni uasnii mtupu ,et mwanzoni walianza kusema walimu wanunue hisa nikashindwa kuelewa ,fedha ya kuanzishia bank walipata wap ? Naona badae walirekebisha ....walimu amkeni jaman.....Baba yangu alikufa kwa kupooza mwili nilimuuguza alikuwa mwalim mustafuv,kwakwel amekufa huku akiwa anasononeka ,alichangia chama lakin hakupata chochote .....teachers amkeni
 
Bila shaka hata hao malecture wao ni waoga mno,
Nafikiri hatutakosea kuwafananisha walimu na kunguru
 
May his soul rest in peace
 
...inasikitisha iwapo kweli wewe ni Mwl. usiyejua hata umuhimu wa 'trade union' ya walimu. What is Tzs. 16,400.00 iwapo zinachangia wahusika kutatua matatizo yenu ya ajira kwa pamoja (collectively). Kama ni tatizo haliwezi kuwa michango ya 2% ya mishahara au walimu kuwa na trade union yao. La hasha. Pitia, zungumza, fuatilia na pendekeza marekebisho kwenye governance software/hardware za CWT! Kubumbuka kuna waliopoteza kazi na maisha kuwezesha kuanzishwa kwa CWT. Hao hawakuwahi kuwa na malengo ya kunufaika binafsi na CWT bali kuhakikisha walimu wananufaika na jasho lao! zamani za kabla ya miaka 24 iliyopita hali ya walimu haikuwa kama leo. Apumzike kwa Amani Mwl. Mashanga.
 
je utetezi wa shida za walimu ni kwa percentage ? CWT ni majizi ya mishahara ya walimu.hawana utetezi wowote kwa walimu.ni chombo cha wanasiasa cha kuwazuga na kuwakejeli walimu.
Hivi walimu waliopo vijijini huko uyui,shule nzima wako walimu wawili,hakuna nyumba ya walimu,mshahara hata wa konda wa daladala anakuzidi hivi wanaishije?
 
Wewe ni mmoja wa viongozi dhalimu wa cwt,unatetea cwt ili uendelee kula mishahara hewa ya walimu.tambi lako.
Cc : Meljons
 
Tuendelee kupaza sauti huenda Magufuli ataelewa atutumbulie hili dubwasha
 
Kumbe wewe ni mwalimu? Si ulisema unaishi Kenya?

Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…