Walimu wanavyoibiwa na CWT & PSPF

du nchi hii wasomi hawajitambui....sasa walimu wanashindwaje kuvunja hicho chama na kuunda kingine..

note Tanzania ni nchi ya kwanza duniani kwa unafiki.

Ndomana tunaongea sana vitendo sifuri


Umeliweka vizuri sana hili. Katika fani ambayo ukombozi wao unategemea kudra za Mungu labda miaka 1000 ijayo, ni walimu wa Tanzania. Hawana umoja ni sawa na nyumbu wa Serengeti. Kulalamika tu lakini hakuna hatua wanazochukua.
 
Ukujitoa hamna madhara!

Ni chama cha hiari!

Andika tu barua kwa mwajiri wako ndani ya mwezi mmoja hawatakukata tena!

Mfano SUA ni asilimia tu 20 ya wafanyakazi wako RAAWU!

Acha kulalamika jitoe!

Ukipata tatizo kuna sheria za kazi!

CHAMA Hawatakusaidia na hawana historia ya kusaidia wanachama!!!
 
MASWALI KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT)
1.Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano: Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), je vinamnufaishaje mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu?

2.Kwanini C.W.T wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine?

3.Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini? Tofauti hizo zinaletwa na mfumo wa asilimia zilizowekwa na hivyo kuweka wachangiaji katika matabaka yasiyo na tija wakati huduma ni sawa.

4.Je kuna uhalali gani wa kiinua mgongo cha mwanachama anayestaafu kwa uwiano na alichochangia toka uanachama wake hadi kustaafu? Ikiwa kiinua mgongo kilichopangwa na C.W.T kwa sasa ni mabati ishirini (20) tu.

5.Je C.W.T kwa mwaka inakusanya kiasi cha shilingi ngapi kwa waalimu wote Tanzania kwa makato ya asilimia mbili (2%) ya kila mshahara wa mwanachama ambayo pia inatofautiana kulingana na madaraja na fedha hizo zinatumikaje ilihali tayari kuna vitega uchumi?

6.C.W.T inawafanyakazi wangapi kwa kila mkoa na taifa kwa ujumla na posho zao zikoje?

7.Kwa kuwa waalimu wamekua wakinyanyasika na kudharaulika na kutosikilizwa katika halmashauri, Je C.W.T inafanya nini kurudisha hadhi ya mwalimu katika ngazi ya halmashauri ilihali mambo haya yanaendelea kumgandamiza na kumnyanyasa mwalimu?

Watag wadau wote wa Elimu.plz share we need changes.
 


Ukisoma public standing order kifungu 61(1) mwaajiri haruhusiwi kukata mshahara wa mtumishi ama mtumishi amemuelekeza kwa maandishi kwa kujaza fomu namba tatu TUF 3, Hivyo wakurugenzi watashitakiwa kukata mishahara ya wafanyakazi bila ridhaa yao. Walimu waamke Wasome sheria za kazi waungane waishitaki Cwt na washenga wao wakurugenzi kwa kuvunja sheria za utumishi wa umma.
 
nlitegemea mapambano makal baada ya walimu wenye digrii kuongezeka kuanzia miaka ya 2005 nikiamin kuwa watapambana kisom zaid lakin hamna lolote
Imekuwa hivyo kwa kuwa
1. Wakati wa uchaguzi akigombea mwalimu mwenye shahada anawekewa mizengwe, na viongozi waliopo madarakani wanafanya kila hila ili asipite. Wanataka viongozi waalimu ngazi ya cheti tu (walio waoga kuhiji).
2. Sii rahisi waalimu wa sekondazri kushika nafasi za juu za yongozi kwa kuwa wapiga kura wengi ni waalimu wa shule za msingi (wenye vyeti wengine vya kughushi). Shule za msingi zina wawakilishi wawili ili hali shule za sekondari zina mwakilishi mmoja. Wale wapiga kura (waalimu wa msingi) huunganisha nguvu kumpigia kura mwenzao wa shule ya msingi.
Ndiyo maana hata kesho, CWT haiko tayari kuwa na uwakilishi sawa kwani wanajua kitakachofuata ni kuwa na CWT ya Msingi na CWT ya Sekondari.
3. CWT ni tawi la chama cha siasa, si chama cha Waalimu.
Pamoja na mambo mengine, CWT imechangia kuwanyonya sana waalimu na kuzorotesha Elimu ya nchi hii.
 
Kuna mkurugenzi amewahi kushtakiwa (nimesahu halmashauri husika), na waalimu walishinda kesi. Sijui utekelezaji wa ile hukumu ulifikia wapi.
 
It's simple, hutaki makato acha ualimu.

Pia, wingi wa neno MWALIMU ni WALIMU na sio WAALIMU.
 
Mwl hebu sema malalamiko yako ya msingi.
Weka katiba bullet form iwe rahisi kuyapitia na kujadili!
Mi nitajaribu kufafanua juu ya percentage ktk makato!
Nadhani huo ni mfumo sahihi zaidi, Mwl mwenye elimu kubwa ana advantage zaidi over Yule mwenye elimu ya chini, lkn uwiano wa michango usipofuata asilimia kuna mwingine 5000 ni zaidi ya 5% ya mshahara wake, so ktk mwezi yeye ana kuwa relatively kaumia zaidi!
Chama chenu kama hakina maslahi kwenu, kulikoni kulalamika weka hoja ktk mpangilio!
MF.
1. Utetezi wa maslahi ya walimu
Chama chetu kimeshindwa kusaidia walimu kupata maslahi yao. Hadi sasa kuna jumla ya walimu xxx ambao wanadai zaidi ya TSh. Yy huku chama kikishindwa kuchua hatua.
Maoni yangu: chama kupitia matawi yake kiandae orodha ya madai ya walimu yote, kifungue kesi dhidi ya waajiri na kisaidie kulipa mawakili watakaosimamia kesi etc.
Ukitumia mtindo wa aina hii sio kwamba mawazo yako yataeleweka lkn pia unaweza kusaidia viongozi wako wakapata kujua potential ya wanachama wao!
Wapo wanaodhani kuwa hata walimu wenyewe hamjui kitu ndio maana wanawachezea!
 
CWT ni jipu,kiukwel haina faida kwa Waalimu,ipo kwa maslahi ya wachache,na Waalimu nao wameshindwa kujitmbua ili kujiondoa kwenye chama hiki cha kidhalimu,haiji akilini mwanachama anayestaafu anapewa mabati 20 ambayo thamani yake ni laki tatu,
 
Kazi ya cwt ni kujenga maghorofa ya vitega uchumi na kugawa T-shirt kwa walimu
Na vp kuhusu ile bank yenu inaaza lini?
 
mi naon mapenzi hayafundishwi inatokea tu unajua
 
Halafu viongoz wez wa CWT wakistafu wanapewa ukuu wa wilaya....
 
Tunawasaidia kuwaamsha akili zao mkuu
 
Walimu wanapaswa kuwekwa kwenye kundi la special group kwa kutojitambua licha ya kuwa sie wengine tumeamua kuvaa mabomu kuwatetea
 
Ni lazima waungane, waache hofu na woga ili wajikwamue kutoka mikononi mwa huyo mnyonyaji dhalimu alimaarufu CWT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…