Walimu wakimbia shule kwa kubakwa na wanafunzi


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,069
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,069 2,000
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa

KWA UFUPI
Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.

WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.


Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.


Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.


Akizungumza kwa simu akiwa Dar es Salaam, mwalimu huyo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 485, imepoteza mwelekeo, haitawaliki na mazingira yake hayavutii walimu, hasa wa kike, kuishi na kufanya kazi.


“Tumevumilia vya kutosha, lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Walimu wanafikia mahala wanabakwa! Kibaya zaidi wazazi na mamlaka nyingine hazionyeshi ushirikiano kwetu, wazazi wanawa-support (wanawaunga mkono) watoto wao,” alieleza.
Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku.


Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea baada ya wanafunzi hao kuwatongoza walimu wao na kukataa kufanya nao mapenzi.


Mwalimu huyo alidai kuwa walimu wamekuwa wakitishiwa kuchomwa visu na nyumba zao kuchomwa moto, huku walimu wanne wa kike wakidhalilishwa kimapenzi kwa kupigwa mabusu na kutongozwa na wanafunzi.
“Wanafunzi wamefanya mtihani wa kidato cha pili chini ya ulinzi wa askari polisi wenye silaha kitu ambacho si cha kawaida,” aliongeza.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Ofisa Elimu Sekondari, Adnan Mwenda alisema asingependa kuzungumzia tatizo hilo kwa kuwa siyo msemaji. Akashauri atafutwe mkurugenzi wa wilaya… “Unaweza kuzungumza mambo mengine yakakuletea matatizo,” alisema Mwenda kabla ya kuelekeza atafutwe mkurugenzi.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Leonard Rwegasira alithibitisha walimu hao kuikimbia shule hiyo na kusema kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, itakutana hivi karibuni kujadili suala hilo.
“Ni kweli shule hiyo imetelekezwa, walimu wamekimbia na wanafunzi hawaendi shule. Tatizo tunalifahamu na Mkuu wa Wilaya anafanya jitihada mbalimbali kurekebisha tatizo hilo,’ alisema.


Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruaruke, Hemedi Mpullu pia alithibitisha walimu hao kuitelekeza shule hiyo na kusema Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu ameagiza kufanyika kwa kikao cha dharura ili kupatikana mwafaka kati ya walimu hao, wanafunzi na wazazi.
“Mbunge wa Kibiti, Abdul Marombwa amepanga pia kufanya mkutano hapa Ruaruke ili kutafuta mwafaka,” alisema Mpullu.
Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT), Wilaya ya Rufiji, Manyama Lazaro alisema kuondoka kwa walimu hao, kumefanya shule hiyo ijifunge yenyewe, kwani wanafunzi nao sasa hawaendi shule.


“Wanafunzi wamefikia hatua ya kuwachora walimu wa kike wakifanya mapenzi na walimu wa kiume katika kuta za vyoo! Huu ni udhalilishaji mkubwa,” alisema.
Lazaro alieleza kuwa katika siku za hivi karibuni, wanafunzi hao walichoma moto nyumba tatu za walimu na Bodi ya Shule iliamua kuwa wanafunzi hao waitwe na wazazi wao ili walipe gharama za uharibifu.Walimu wakimbia shule kwa kubakwa na wanafunzi - Kitaifa - mwananchi.co.tz 
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
7,053
Points
1,225
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
7,053 1,225
Walaaniwe wote wanaohusika na udhalilishaji wa walimu wetu. Inasikitisha kuona hadi wazazi wanahusika katika kuchochea udhalilishaji huu. Ualimu ni kazi inayotakiwa kuheshimiwa na kuthaminiwa. Bahati mbaya serikali yetu hailisimamii hili.
 
B

Bahati Risiki

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
530
Points
0
B

Bahati Risiki

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
530 0
Watanzania tunakokotwa na viongozi walioshindwa kudhibiti uingizwaji wa madawa ya kulevya nchini. Tumefika kubaya mno na hii ni ishara tosha. Tubadili mienendo na kuchagua viongozi bora. Tunauawa kwa jasho letu wenyewe. Hili ni moja tu masuala yanayoidhalilisha nchi yetu na uongozi wake mpaka basi. Tuamke, tufikiri, na tutende. Taifa letu polepole lakini linaangamia.
 
Brother Jero

Brother Jero

Senior Member
Joined
Jan 31, 2012
Messages
134
Points
225
Brother Jero

Brother Jero

Senior Member
Joined Jan 31, 2012
134 225
nidhamu siku hizi ni zero,hasa kwa wanafunzi wa shule hizi za st.kayumba na ambapo hukosa msukumo wa kusoma huwa balaa.ni vema wazazi na wananchi wote wanaozunguka shule hizi wakashirikishwa katika kurekebisha tabia za vijana wetu.isiwe ni jukumu la walimu peke yao.
 
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
17,822
Points
2,000
Age
36
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
17,822 2,000
Malezi mabaya ndio yaliyochangia
 
ARV

ARV

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2011
Messages
2,305
Points
2,000
ARV

ARV

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2011
2,305 2,000
Kumbe ni huko Rufiji, nilishtuka maana nilidhani tukio limetokea katika mikoa hii iliyoendelea,inayojua maana ya elimu.
Kwa stahili hii wataendelea kuwa nyuma miaka yote.
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,447
Points
2,000
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,447 2,000
Huko Raruke kuna tabia za ajabu sana na wazazi wanachangia sana kuendeleza tabia za ajabu kama hizo,na ushirikina umepamba moto huko,wazazi hawana mwamko wa elimu....kazi kubwa kweli kweli wizara ifanye maamuzi magumu na labda wapelekwe walimu wanaume na wenyeji wa huko huko Rufiji watawezana
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
46,428
Points
2,000
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
46,428 2,000
Then baada ya miaka kadhaa utawasikia kina mohamedi said wakidai kuwa mfumo kristo
 
Last edited by a moderator:
S

sweke34

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Messages
2,526
Points
1,195
S

sweke34

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2010
2,526 1,195
Huko Raruke kuna tabia za ajabu sana na wazazi wanachangia sana kuendeleza tabia za ajabu kama hizo,na ushirikina umepamba moto huko,wazazi hawana mwamko wa elimu....kazi kubwa kweli kweli wizara ifanye maamuzi magumu na labda wapelekwe walimu wanaume na wenyeji wa huko huko Rufiji watawezana
Inasikitisha sana. Wenzetu kwenye nchi zilizoendelea wanafanya mavitu kama hapo chini sisi huku bado kuna jamii zenye mtazamo wa watu wa kale walioishi kwenye mapango. Cha ajabu hawahawa utawakuta wanajiita watu safi wenye kumuamini Mungu wakiwa kwenye nyumba zao za ibada.


 
T

timbilimu

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Messages
4,805
Points
1,250
T

timbilimu

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2010
4,805 1,250
Then baada ya miaka kadhaa utawasikia kina mohamedi said wakidai kuwa mfumo kristo
Utawala wa Mwl. Nyerere ulijua matatizo ya shule hizi zilizoko ktk maeneo ya wacheza ngoma kwa kuwapeleka sekondari zilizoko ktk mikoa ambayo inathamini elimu.
 
Last edited by a moderator:
S

Sangomwile

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2012
Messages
3,084
Points
1,250
S

Sangomwile

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2012
3,084 1,250
Watawala kama Mzee Mnali ndio wa kupelekwa huko,fimbo kufutwa mashuleni nalo tatizo.Utukutu hatukatai upo lakini hadi kubaka walimu?NO!
 
trachomatis

trachomatis

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Messages
3,671
Points
1,250
trachomatis

trachomatis

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2011
3,671 1,250
Walaaniwe wote wanaohusika na udhalilishaji wa walimu wetu. Inasikitisha kuona hadi wazazi wanahusika katika kuchochea udhalilishaji huu. Ualimu ni kazi inayotakiwa kuheshimiwa na kuthaminiwa. Bahati mbaya serikali yetu hailisimamii hili.
Watakuwa wanasomea ukubwani hao wanafunzi wala si watoto!
 
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Messages
30,101
Points
2,000
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2010
30,101 2,000
Inawezekana waalimu wanajiweka kwenye mazingira hatarishi pia
 

Forum statistics

Threads 1,286,232
Members 494,902
Posts 30,887,828
Top