TIQO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 13,786
- 2,104
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Hiki ni choo cha muda cha kwanza cha shule ya msingi Lipangala Ludewa mkoani Njombe kilichobomoka toka mwaka 2004 [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hiki ni choo cha kisasa ambacho kimejengwa sasa katika shule ya Msingi Lipangala ambacho pia kimeanza kubomoka
Hiki kilikuwa ni choo cha walimu miaka hiyo kwa sasa shimo jipya linachimbwa mbele ili kurejesha huduma ya choo kwa walimu
Hii ndilo hali halisi ya choo hiki cha walimu shule ya Msingi Lipangala Ludewa ,kwa sasa hakitumiki
Mbunge Filikunjombe akiagiza choo kujengwa haraka
WAKATI serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ikiendelea kuweka mikakati ya kuboresha elimu ya awali na msingi ,mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe asikitishwa na shule ya msingi Lipangala wilaya Ludewa mkoani Njombe kukosa choo cha walimu na wanafunzi na kupelekea walimu wa shule hiyo kuendelea kujisaidia vichakani kwa zaidi ya miaka 5 hivi sasa .
Kutokana na shule hiyo kukosa vyoo vya wanafunzi na walimu mbunge huyo aagiza uongozi wa kata hiyo pamoja na tarafa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi vyoo ndani ya siku 10 kunzia juzi na pindi shule zitakapofungua kuwepo na vyoo vya uhakika shuleni hapo.
Wakizungumza katika mkutano wa mbunge Filikunjombe wananchi wa kijiji cha Lipangala walisema kuwa wnasikitishwa kuona walimu wa shule hiyo wakikimbi kwenda kujisaidia vichakani huku baadhi yao wakilazimika kwenda majumbani kwao kupata huduma ya choo jambo ambalo wmedai ni hatari katika maendeleo ya elimu shuleni hapo.
Saraha Edward alisema kuwa mbali y walimu kuendelea kufundisha shule hiyo bila ya choo bado wanafunzi wamekuwa wakipata tabu kubwa kupata huduma ya choo kutokana n vyoo vilivyokuwepo shuleni hapo kuwa na hali mbaya zaidi.
"Hii shule yetu ni vema ikafungwa kabisa kwani tunawasiwasi mkubwa watoto wetu kuja kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na shule kutokuwa na choo cha uhakika ni kama wanajisaidia porini kwani hivi si vyoo vya kujivunia kama shule"
Mmoja kati ya walimu wa shule hiyo ambae hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa shule hiyo alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikiendeshwa bila choo toka mwaka 2004 ambapo wanafunzi walianza kukosa choo cha uhakika baada ya kile kilichokuwepo awali kubomoka .
Kutokana n tatizo hilo la choo cha wanafunzi kubomoka wananchi walilazimika kujenga choo cha muda ambacho pia hakikuchuku muda kilibomoka na hivyo kuendelea kushirikiana choo kimoja na walimu kwa kipindi cha mwaka mmoja na baada ya hao hata choo cha walimu pia kilibomoka hivyo kukosa choo cha walimu na kulazimika kujenga choo cha muda ambacho ni hatari pia kwa usalama wa wanafunzi huku walimu wao wakilazimika kwenda kupata huduma hiyo majumbani kwao ama porini .
Uchunguzi uliofnywa na mwandishi wa habari hizi shuleni hapo umebaini kuwa choo cha walimu chenye matundu mawili kilichokuwepo awali kimekuwa hakitumiki toka mwaka 2005 kutokana na choo hicho kubomoka kutokana na kujengwa chini ya kiwango pasipo kujengewa saruji huku ardhi ya eneo hilo ikiwa inaongoza kwa kuwa na unyevu unyevu.
Afisa tarafa ya Liganga Edward Wayotile alithibitisha madai hayo ya shule kuendeshwa bila choo na kuwa tayari wameweka mkakati wa kujenga vyoo katika shule hiyo .
Alisema kuwa mkakati ni kujenga vyoo vipya vyenye matundu 16 kwa wavulana na matundu 12 kwa wasichana pamoja na kujenga choo chenye matundu mawili kwa ajili ya walimu wa shule hiyo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo la Ludewa Bw Filikunjombe mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya shule hiyo kukosa vyoo bado aliuagiza uongozi wa kata ,tarafa na wilaya kufika mara moja katika shule hiyo ili kujenga choo hicho ndani ya siku 11 kuanzia juzi ili wanafunzi watakapoanza masomo kuwepo kwa huduma ya uhakika ya choo cha wanafunzi na walimu.
"Haiwezekani shule kuendeshwa bila vyoo ....sasa naomba viongozi wa elimu wilaya kushughulikia tatizo hilo mara moja kwani kama tutaacha suala hilo ni kutoitendea haki elimu ya watoto wetu"
Mbunge Filikunjombe pia alikabidhi msaada wa bati 50 kwa diwani wa kata hiyo kwa ajili ya ukamilishaji wa darasa la awali katika shule hiyo huku akimuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kutoa fedha katika mfuko wa maafa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo kwenye shule hiyo.
Wakati huo huo mbunge huyo aliwataka wazizi wenye watoto waliofaulu kujiunga na elimu ya sekondari mwakani kuhakikisha wanafanya maandalizi mapema na kutotumia fedha zote katika sherehe za kufunga mwaka na kuacha kutenga fedha kwa ajili ya kusomesha watoto sekondari.
MWISHO
source:Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD][/TR]