Walimu waanza mgomo.

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Huku chama cha walimu kikiwa bado kimya kuhusiana na mgomo wa walimu.Walimu mkoani Dodoma wameanza mgomo huo kimya kimya katika shule mbalimbali za mkoa huu.

Nikiongea na baadhi ya walimu ambao hawakutaka majina yao kutajwa hadharani wamesema hawatasubiri tamko la CWT kwani wao ndio wanaoathirika kwa kiasi kikubwa.

Wametoa wito kwa walimu nchini kote kupigania haki zao wenyewe na wameomba kuungwa mkono katika swala hili na pia wamewaomba walimu kuacha woga kwani woga ndio yatakuwa mateso yao.
 
wakaze buti sana manake hawakawii kusalitiana sababu kunawanao jikomba komba huko juu.
 
wakaze buti kama madaktari bwana hii habari ya kila siku stori ndio inaleta shida kubwa
na mambo hyaendi bwana
 
Walimu hawawezi kugoma na daima hawateweza sababu vyeti vyao vina shida na pengine akili ya kutatua matatizo yao wameachia chichiem
 
Tusubiri kisingizio kikuu "Chadema wapo nyuma ya Mgomo huu". Yani imefika wakati hata ukivunjiwa nyumba na vibaka ama korofishana na Mkeo utaambiwa CDM wana mkono hapo. TZ Dhaifu ya VISINGIZIO.
 
hili haliwezekani kwa walimu wa tanganyika...maybe!!! ngoja tuone...
 
Walimu waoga sana hata kugoma siku moja wameshindwa!

Kweli pori la mwabepande linaogopwa sana
 
Walimu mpaka watakapobadilika lakini wakiendelea hivi watakuwa wanyonge mpaka kiama.

Ni waoga, dhaifu wanaoridhirika kama wamefoji vyeti na kazi hiyo kama siyo stahili yao!!!!

Ni full ubabaishaji.
 
wakaze buti kama madaktari bwana hii habari ya kila siku stori ndio inaleta shida kubwa
na mambo hyaendi bwana

Ahahahaha, kuna usemi ambao waaalimu wanautekeleza unasema kwamba " heri mwoga aliyepona kuliko shujaa aliyeuawa". Kwao mambo kama hayo ni magumu sana kutekeleza.
 
hii inaonyesha jinsi walimu wasivyo na umoja, bado ni waoga waangalie wenzao madaktari walivyofanya
 
Huku chama cha walimu kikiwa bado kimya kuhusiana na mgomo wa walimu.Walimu mkoani Dodoma wameanza mgomo huo kimya kimya katika shule mbalimbali za mkoa huu.Nikiongea na baadhi ya walimu ambao hawakutaka majina yao kutajwa hadharani wamesema hawatasubiri tamko la CWT kwani wao ndio wanaoathirika kwa kiasi kikubwa.Wametoa wito kwa walimu nchini kote kupigania haki zao wenyewe na wameomba kuungwa mkono katika swala hili na pia wamewaomba walimu kuacha woga kwani woga ndio yatakuwa mateso yao.

Wawe makini kwani Serikali haitachelewa kuwafuta kazi wote na kuajiri walimu wapya kwani walimu ni wengi sana.
 
Huku chama cha walimu kikiwa bado kimya kuhusiana na mgomo wa walimu.Walimu mkoani Dodoma wameanza mgomo huo kimya kimya katika shule mbalimbali za mkoa huu.Nikiongea na baadhi ya walimu ambao hawakutaka majina yao kutajwa hadharani wamesema hawatasubiri tamko la CWT kwani wao ndio wanaoathirika kwa kiasi kikubwa.Wametoa wito kwa walimu nchini kote kupigania haki zao wenyewe na wameomba kuungwa mkono katika swala hili na pia wamewaomba walimu kuacha woga kwani woga ndio yatakuwa mateso yao.
Kama kweli wana dhamira ya dhati ya kudai haki zao kwa nini wagome kimya kimya?
 
Back
Top Bottom