Pamoja na kuwaasa walimu wajiheshimu, ila sisi kama wazazi tuna jukumu kubwa sana la kuhakikisha watoto wetu wanapata malezi bora n stahiki.
Hao wadogo zako, wanaonaga kwenye TV. Kukumbatiana na kunyonyana ndimi, unaona ni jambo la kawaida. Kwamba, wanafurahia shows.
Ila ukumbuke vitoto vya sasa balehe ni miaka 12 mpaka 15. Hao wapo form 1 au 2. Vinakuwa na mchecheto na mgegedo. Wakishawishiwa kidogo tu, na walichokiona kwenye TV, wanakuwa fundi kuliko hata wazazi wao. Ukijumlishia na vinavyojua kucheza mziki kwa kunengua, ptyuuu mbaka.
Wazazi tujitahidi kutilia mkazo malezi ya watoto wetu. Huyo hata akitongozwa, anakataa. Anajua si jambo jema.
Lawama zote tusizielekeze kwa walimu pekee. Bali sisi pia kama walezi tunastahili.