sinajinasasa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 2,989
- 4,129
Kilio hiki naomba kimfikie Waziri husika, hapa Morogoro kuna Shule ya Msingi ya Mzinga inatesa Wanafunzi wake, kwa vile Walimu wana hofu ya wanafunzi wa shule ya msingi wa darasa la saba na la nne kufeli mitihani, walimu hawa wamekuwa nyuki, wanawachapa sana wanafunzi viboko, yaani watoto wanalalamika sana kwa wazazi nyumbani.
Mtoto mdogo anaamka giza kabisa asubuhi anawahi shule, walimu wanawapa mitihani Watoto saa 12 asubuhi na asipofanya ni fimbo tu, kuna watoto wanatoka maeneo ya umbali hadi wa km 5 kwa miguu kuja shule, na wao wakichelewa ni fimbo tu hawajali kwamba mtoto anatoka mbali.
Wakati fulani hadi tunahisi labda watoto waache tu shule basi maana si kwa mateso hayo ya watoto.
Walimu badala ya kufundisha, wao wanawapigisha strori za udaku kwa watoto, yaani mwalimu anatumia dakika 40 za kipindi kuwalaani wazazi wa watoto eti hawana ushirikiano na walimu.
Sasa ninyi walimu nawauliza ushirikiano gani mnataka? Je, tuwape rushwa ili mfundishe watoto, matendo yote hayo tunaletewa na watoto wenyewe kama mashahidi. Walimu hawa wengi wanahangaika kutafuta wateja wa QNET badala ya kufundisha.
Naomba niwataje kwa majina yao;
Walimu wengine wao wana stress za kutapeliwa na qnet. Sasa hasira zao zinawaangukia watoto. Waziri wa elimu mama yangu okoa jahazi. Naomba mnisaidie kumtagi mhusika achukue hatua.
Mimi Mzazi.