Walimu mnaofundisha shule za binafsi mnaishije?

Modestproposal

Senior Member
Joined
Jan 6, 2022
Posts
127
Reaction score
230
Kwanza nadeclare interest kuwa mimi ni mwalimu by professional.

Nilihitimu chuo miaka 7 iliyopita. Baada ya kuhitimu tuliambiwa tusubiri ajira kwa muda wa mwezi mmoja au mmoja na nusu ili mwenda zake aondoe wafanyakazi hewa, hadi napoandika uzi huu mwezi mmoja na nusu haujaisha!

Basi, nilipoona mambo hayaendi kabisa nikatafuta kazi kwenye open school ambayo ilikuwa inanza. Nilipiga kazi hajapata kutokea, kituo kikapata wanafunzi wa kutosha, wakati huo nilikuwa nalipwa sh.10800 kwa wiki kwa makubaliano kuwa wanafunzi wakiongezeka posho ingeongezeka. Nakumbuka mwajiri alikuwa na formula mmoja matata ya kikokotoo, ngoja nikumbuke; 270*number of period*number of students.

Wakati naanza kulikuwa na wanafunzi 20*2periods per week* 270=10800 usafiri juu yako. hahahaha acha nicheke. Mungu saidia tukapata wanafunzi kama 50 hivi wa QT na PC. Kwa hiyo nikawa na vipindi 4 *50*270=54000 per week,hee jamaa akabadilka eti atakuwa ananilipa 40000 flat kwa week. Nikaona isiwe tabu hata hiyo inatosha mana something is better than nothing. Cha ajabu nikawa silipwi hata hiyo 40000 nikaamua kuondoka nikatafute kwingine.

Nikaenda mkoa wa Songwe kwa rafiki yangu ambae ameajiriwa huko na alikua ameanzisha kituo chake tukashirikiana vizuri na tukapata wanafunzi, tulikuwa tunagawana kinachopatikana baada ya kutoa matumizi.

Kule nilikoondoka wakaanza kunitafuta, kila mara simu oh rudi Mwl wanafunzi wanakuhitaji sana, ghafla nikatumiwa pesa niliyokuwa nadai kama laki 40000, nikaona sasa huko Kumenoga. Kweli nikarudi mwaka 2019, wanafunzi walinishangilia sana kuniona aisee kumbe walimu tudhalaulika lakini tuna umuhimu mkubwa sana ktk shule binafsi.

Kwakuwa shule hiyo ilikuwa na majengo ya kotosha waliamua kusajili na tukawa na form one hadi form 3 kwa wahamiaji. ikateuliwa kuwa academic master. Mshahara 350000. Nikafurahi sana kwani kwangu ilikuwa inatosha. Sikuwa na mke wala nini so kwa bata bata za hapa na pale mbona nilkuwa done.

Bila kuwachosha, kumbe mshahara uko kwenye makaratasi, kulipwa ni issue nyingine. Hapa ninapoandika Nina miezi sita sijaona mshahara, mkitishia kugoma ndio mnapewa laki moja halafu kimyaa. Kibaya zaidi nimeoa na Nina mtoto. Yaani kichwa kinawaka moto.kibaya zaidi Nssf nakatwa wala hapelekwi, loans board ndio usiseme.natamani kuacha kazi laki ndio niache pesa yangu kweli?

Basi naomba mnishauri nifanye nini ili nilipwe pesa yangu.
 
Ulikosea pale ulipooandoka Songwe. Hapo unaendeleza empire ya mwanaume mwenzako. Jitoe hapo Kama una udhubutu mkuu anzisha kituo chako. Kama vipi tushirikiane Mana mwishowe itakuwa shule. Think like 20yrs to come don't expect instant gratification
 
Huu ndio ushauri sasa
 
Hakuna manyanyaso kama shule za private bhana asee
 
Uwezo wa kufundisha inaonekana unao. Ulichoenda fanya kule Songwe ungekiendeleza. Either urudi kule au ufanye kama ulvyokua unafanya kule hapo ulipo sasa.
Kama uko na mkataba kawashtaki pia.
 
Kwanza nadeclare interest kuwa mimi ni mwalimu by professional.

Nilihitimu chuo miaka 7 iliyopita. Baada ya kuhitimu tuliambiwa tusubiri ajira kwa muda wa mwezi mmoja au mmoja na nusu ili mwenda zake aondoe wafanyakazi hewa, hadi napoandika uzi huu mwezi mmoja na nusu haujaisha!

Basi, nilipoona mambo hayaendi kabisa nikatafuta kazi kwenye open school ambayo ilikuwa inanza. Nilipiga kazi hajapata kutokea, kituo kikapata wanafunzi wa kutosha, wakati huo nilikuwa nalipwa sh.10800 kwa wiki kwa makubaliano kuwa wanafunzi wakiongezeka posho ingeongezeka. Nakumbuka mwajiri alikuwa na formula mmoja matata ya kikokotoo, ngoja nikumbuke; 270*number of period*number of students.

Wakati naanza kulikuwa na wanafunzi 20*2periods per week* 270=10800 usafiri juu yako. hahahaha acha nicheke. Mungu saidia tukapata wanafunzi kama 50 hivi wa QT na PC. Kwa hiyo nikawa na vipindi 4 *50*270=54000 per week,hee jamaa akabadilka eti atakuwa ananilipa 40000 flat kwa week. Nikaona isiwe tabu hata hiyo inatosha mana something is better than nothing. Cha ajabu nikawa silipwi hata hiyo 40000 nikaamua kuondoka nikatafute kwingine.

Nikaenda mkoa wa Songwe kwa rafiki yangu ambae ameajiriwa huko na alikua ameanzisha kituo chake tukashirikiana vizuri na tukapata wanafunzi, tulikuwa tunagawana kinachopatikana baada ya kutoa matumizi.

Kule nilikoondoka wakaanza kunitafuta, kila mara simu oh rudi Mwl wanafunzi wanakuhitaji sana, ghafla nikatumiwa pesa niliyokuwa nadai kama laki 40000, nikaona sasa huko Kumenoga. Kweli nikarudi mwaka 2019, wanafunzi walinishangilia sana kuniona aisee kumbe walimu tudhalaulika lakini tuna umuhimu mkubwa sana ktk shule binafsi.

Kwakuwa shule hiyo ilikuwa na majengo ya kotosha waliamua kusajili na tukawa na form one hadi form 3 kwa wahamiaji. ikateuliwa kuwa academic master. Mshahara 350000. Nikafurahi sana kwani kwangu ilikuwa inatosha. Sikuwa na mke wala nini so kwa bata bata za hapa na pale mbona nilkuwa done.

Bila kuwachosha, kumbe mshahara uko kwenye makaratasi, kulipwa ni issue nyingine. Hapa ninapoandika Nina miezi sita sijaona mshahara, mkitishia kugoma ndio mnapewa laki moja halafu kimyaa. Kibaya zaidi nimeoa na Nina mtoto. Yaani kichwa kinawaka moto.kibaya zaidi Nssf nakatwa wala hapelekwi, loans board ndio usiseme.natamani kuacha kazi laki ndio niache pesa yangu kweli?

Basi naomba mnishauri nifanye nini ili nilipwe pesa yangu.
Unafundisha masomo gani mkuu, uko Dar sehem gani?. I wish tuonane tubadishane mawazo
 
Back
Top Bottom