INNOMATIX
Senior Member
- Aug 24, 2013
- 113
- 47
Mkuu wa milaya ya kinondoni,dc makonda amekuja na wazo zuri kuhusu walimu wa mkoa wa dar es salaam kusafiri bure.Hili ni wazo zuri na la kuwa mfano wa kuigwa na wakuu wa wilaya hata wabunge wa sehemu mbali mbali Tanzania licha ya chama cha walimu kuleta changamoto.......ila swali langu linakuja....serikali halioni matatizo ya walimu katika mishahara?Mwalimu wa sekondari kulipwa laki nne au tano kwa mwezi ni sahihi?mi nadhani kuna mambo yalitakiwa kuwekewa mkazo zaidi kuliko hili swala la nauli za walimu kwenye dala dala.....nyumba nzuri za kuishi,mishahara,mikopo isiyo na riba ni katika matatizo machache ya kuangaliwa na serikali kabla ya nauli za mabasi kwa walimu