Wanajamvi habari.
Kuna habari nimetonywa na jamaa yangu ambaye ni mwalimu katika shule moja jijini Dar. Mtonyaji anasema kuna mwaliko umetolewa kwa walimu kuhudhuria kongamano litakalofanyika ukumbi wa Yombo - UDSM.
Mtonyaji anasema kongamano hili linaratibiwa na makada wa ccm lenye lengo la kuushawishi umma kuwa walimu wanaunga mkono serikali 2 na mwenendo wa mchakato wa katiba mpya.
Anaongeza kwa kusema mwaliko unatolewa kwa walimu ambao ni wapenzi wa ccm watakao ungana na mashabiki wa ccm jijini Dar na kuingia ukumbi wa Yombo kana kwamba wote ni walimu.
Mtonyaji anasema walimu nao hawako nyuma kuna mikakati wamejiwekea ya kuhakikisha wanafika ukumbini hapo kwa wingi na kuufichua ufedhuli huo. Pia mtonyaji anasema wataichana ccm laivu kwa kuomba fedha inayofujwa Dodoma kwa kuandika katiba ya ccm ilipe malimbikizo na madeni mengine ya walimu.
Akamalizia kwa kusema kesho ccm itawatambua.