Walimu endeleeni na mgomo baridi tu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu endeleeni na mgomo baridi tu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NG'OMBE, Jun 22, 2012.

 1. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi naamini walimu walishagoma siku nyingi, ila kwa vile serikali ni dhaifu haioni, inajifariji hakuna mgomo. Hivi mtu mzima na akili yako timamu unaanza kuhoji eti kwa nini watoto wamejiunga form one hawajui kusoma wala kuandika. Wakati jibu liko wasi "hakufundishwa ndiyo maana hajui" sasa unaanza kuunda tume eti ichunguze sababu, huo ni puuzi mtupu wa serikali dhaifu. Walimu walishapuuzwa na serikali hadi wameshachoka. Ushauli wangu ni kwamba, endeleeni na utalatibu huo hadi siku moja tupate form four amemaliza hajui kusoma na kuandika, Labda ndiyo serikali itawajali.
   
 2. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Umenena Mkuu!
   
 3. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngombe!

  Una akili kweli you have just said what many people don't want to hear. Bora Mgomo wa Madaktari ! Do you know why wnawapatia watu taarifa ila Mgomo baridi wa Waalimu umekuwepo for almost a decade. Walitafuta a safe harbour ya kujikimu kwa kuanzisha Tuition Enzi za Ruksa alipo kuja Mkapa tuition zikapigwa marufuku shuleni

  Siku hizi zimehamia kwenye vibanda hasara na Vitoto vinaishia kubakwa/ kulawitiwa and no control. Kushuka kwa elimu ndiyo matokeo. Hamshangai watoto wanafaulu darasa la Saba lakini hawajui kusoma na kuandika and CCM inaendelea na Dhaifu. Shule ni zaidi ya Majengo you need to have dedicated teachers who should be well paid siku za wito zilikwenda na Mwalimu.

  Nauliza swali moja na ningetaka Pinda ajibu : Serikali ya CCM has copied and pasted uanzishwaji wa Regulatory authorities Kama EWURA, SUMTRA, and a lot of Agencies. Lakini sijaona mtu anazungumza Regulator wa sector ya Afya wala Elimu it's liberal na Kodi haikusanywi . Angalia utitiri wa vyuo vikuu mashule Hadi chekechea no formula, mahospitalini binafsi yote ni maeneo ya kutozwa kodi lakini we acha tu .

  Back to mgomo wa Madaktari sijasahau yaliyotokea February wakati Pinda alisema watatumia wanajeshi and it was a flop. Kesho mgomo utaanza Pinda ankimbilia CMA. CMA is a government arm and every body knows the rulling shall always be in favour of the Gvt. Hivi kweli Pinda na CCM hawana aibu? Last time Makinda alikataa hoja isizungumzwe Bungeni kwa kuwa waliunda tume and the outcome bado hivi tunakwenda wapi? Kweli JK Dhaifu huku budget kule Mgomo we Madaktari?..?
   
 4. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli maisha ni magumu mno ni juzi tu nimetoka kuchukua ka slip kangu nikakuta
  bodi ya mikopo nao wameanza kukata kale kamshahar ambako kanaishia tarehe 12
  sasa nilishachukua mkopo mwingine kumalizia deni nililokua nadaiwa chuoni .nilivyocheki
  kinachobaki ni dusko yaani hii habari ya mgomo sio kwamba inazungumzwa ni kama ipo tu
  ila udhaifu
   
 5. s

  swrc JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  :deadhorse:CMA ni ninini?:llama:
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Waalimu ndio kundi kubwa zaidi la watumishi wa serikali lakini pia ndio kundi dhaifu kupita mengine. Chama chao (CWT) kimechangia unyanyasaji na uduni wao kimaslahi lakini hawaoni hilo, so they're at a proxy war with everyone!
   
 7. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hapo penye nyeusi nakuunga mkono. LIKE.
   
 8. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi si juzi juzi tu nimesikia kuwa Rais JK ameapisha wakurugenzi sijui na wasuluishi wa pale CMA hii inamaana kuwa walijua linakuja ndio maana wakajiandaa kuwaandaa watu wao itakula kwao hii
   
Loading...