Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Pre paid cards ndiyo jawabu la hiyo changamoto. Ina maana sekali itagharamia kwa kutambua umhimu wa Mwalimu.
 
...hao walimu ndio watakaoanza kuchelewa shuleni badala ya wanafunzi sasa,ni bora kubeba mwanafunzi mwenye shs 200 kuliko mwalimu wa bure!!
 
Kwanini wasiwaongezee hela ya mshahara
 
Yan awa wameona matatizo ya waalimu ni kupanda daladala to ngo wakasimangwe na makonda
 
Wataanza kunyanyaswa sasa Na makondakta wa daladala.
Naona daladala nyingi pia zitaanza ruti zao baada ya muda huo wa kusafirisha walimu bure. Kwa nini wasingetafuta mabasi ambayo yangekuwa yanawasafirisha bure? Serikali iingie tu gharama ya kuyaendesha haya magari??
 
Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji. Yangu macho na masikio - tutasikia na kuona mengi awamu hii ya 'KICK'
 
Serikali ikumbuke na kuwapatia mafuta wamiliki wa daladala walau 500 lts kwa mwezi hapo serikali itakuwa imewaweza makondakta wakorofi
 
Hivi kweli na hao wazee waliokaa nae hapo pembeni wanamchukuliaje huyu kijana?? Kwa kweli ni fedheha kufanya kazi na kijana mkurupukaji kama huyu
 
Okay! Ameongea na makondakta pia? madereva je? ...Wangenunua mabasi special ya walimu ingekua poa sana. Vinginevyo wanataka kuleta ugomvi!
Kama wamiliki wa magari wameridhia, Kondakta au dereva atakataa vipi?
 
Ugomvi/tatizo la walimu na serikali, hili ni janga la bara zima la afrika na baadhi ya nchi zilizo endelea lazima tulijue hilo
Hizo Nchi Ambazo Zimeendelea Zenye Hilo Tatizo Ni Zipi!!?? Au Ukiona Ama Uganda Ndio Unaelewa Bara Zima La Africa!!! Weka Evidence Zako Sio Porojo!! Humu Jf Ni Great Thinkers Mkuu!! Evidence Ndio Mtaji Wako!!
 
Je, Waalimu wenye vyombo vyao vya usafiri wamefikiriwaje kwenye mpango huu
Sawa na kusema unaenda kwenye sherehe unapewa unakaribishwa chakula we unasema umeshiba ila wakupe hela utanunua chakula ukiumwa njaa wanasaidiwa ambao wanashida ya usafiri wenye magari wao wana nafuu..basi wapaki magari wapande bure.
 
Huyu dogo akipewa huu mkoa hakika mtaona mengi msiyoyatarajia
 
haiwezekani..kwani wao ni askari.kwani swala ni nauli au swala ni foleniya dar
 
Hii anatafuta mgogoro to na makonda wa daladala
 
Nawa mikoani muwape pikipiki na baiskeli kuongeza tija, bila hivyo mtakuwa mnaleta utengano kwenye kada ya ualimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…