Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
338
Reaction score
180
Walimu wa shule za msingi na sekondari za umma mkoani Dar es Salaam wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia tarehe 7 Machi 2016.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paulo Makonda na viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria jijini Dar wanazungumza na wanahabari hivi sasa.

Walimu wstatengenezewa vitambulisho maalum ili kuwaondolea usumbufu.

Huduma hiyo ni katika kuwapunguzia adha ya usafiri na ugumu wa maisha ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure.

Muda wa kuwasafirisha bure ni saa 11.30 hadi 2 asubuhi na saa 9 hadi 11 jioni.
 
Uzalilishaji kwa walimu waongezewe maslai wapewe ela za nauli waweze kusafiri kwa Uhuru huku ni kufanya walimu waonekane ni wafanyakazi Wa chini katika jamii yeye angesema wanafunzi wasafiri bure
 

KAMA NAWAONA WALIMU WATAVYONYANYASWA NA MAKONDAKTA WA DALADALA,
TENA BORA HATA WANAFUNZI WATATHAMINIWA KWA KUWA WANALIPA 200/=
KULIKO WALIMU WATAKAOPANDA BURE.
______
NAUONA MTITI ZAIDI PALE KONDA ANAPOONDOA GARI PALE MAWASILIANO AU MAKUMBUSHO KUELEKEA MBEZI, TEGETA, GONGO LA MBOTO
NA
MBAGALA AKIAMINI AKIAMINI KABISA KUWA BASI LIMESHAJAZA ABIRIA ZAIDI YA 40,

KUMBE WOTE NI WAALIMU!
____________
TASWIRA MPYA NAIONA PALE 97.8% YA WABONGO TUTAVYOGEUKA WAALIMU KWA KUTEMBEA NA VITABU VYA KEMIA NA CIVICS WAKATI NI WAMACHINGA TU WA PALE mtoni KWA AZIZI ALLI,

NA
IKIZINGATIWA HATUONI KAZI KUFOJI VITAMBULISHO VYA KAZI YA UALIMU ILI TUPUNGUZE MAKALI YA NAULI.
_____

INGAWA SIJAJUA KAKA'ANGU @KAKA_MAKONDA AMEANDAA STRATEGIES ZIPI,
ILA
NASUBIRI KUSHUDIA VICHWA VYA UTOSI NA MAKONZI WATAYOPIGWA NDUGU WALIMU KWENYE DALADALA.

NIMEMALIZA!
 

Attachments

  • 1456652401480.jpg
    1456652401480.jpg
    51.3 KB · Views: 46
Uzalilishaji kwa walimu waongezewe maslai wapewe ela za nauli waweze kusafiri kwa Uhuru huku ni kufanya walimu waonekane ni wafanyakazi Wa chini katika jamii yeye angesema wanafunzi wasafiri bure
Vipi kuhusu askari
 
Vipi kuhusu askari
Shida ya walimu sio kusafiri bure sio nauli shida ya walimu ni maslai mishara mizuri sehemu Bora ya kufanyia kazi waboreshe shule vifaa kama kila shule ziwe Na maabara Na library wapewe na nyumba za kuishi hapo ndio atakuwa katatua shida za walimu askari wapewe mishara mizuri Na maslai Bora
 
Tusubiri kuanza kuona walimu wakinyanyaswa kama wanafunzi. Sifa kama hizi ni bora kuzitafakari kwanza
 
Je, Waalimu wenye vyombo vyao vya usafiri wamefikiriwaje kwenye mpango huu
 
Mawazo ni mazuri lakini changamoto yake ni kubwa Sana. Walimu wetu watanyanyasika Sana. Wazo nzuri ni kuwapa pre-paid card ambazo zimelipiwa tayari na makonda waelemishe maana ya hizo pre-paid cards,lakini bure itakuwa kuwavunjia heshima walimu mbele ya jamii na wanafunzi wao.
 
SHIDA Yetu Viongozi Wengi, Kila Kitu Ni Siasa Tu!!! Makonda Kwa Kutafuta Njia Ya Kutokea, Kweli Anaweza Kuwashawishi Hao Wamiliki Wa Magari Ya Daladala, Kuwezesha Lengo Lake Kufanikiwa!! Na Hilo Litakuwa Halina Ubishi Kwao, Kwa Vile Wanabembeleza Magari Yao Yasitoke Mijini Na Kupelekwa Pembezoni Mwa Miji, Kutokana Magari Ya MWENDOKASI!!! Ila Shida Kubwa Ni Kwa Wanaotembeza Hayo Magari, Madereva Na Makondakta Tu!! Kwa Vile MATAJIRI Wao Wamegoma Kuwapatia Mikataba Ya Ajira, Badala Yake Wanaendelea Kutafuta HESABU Ya Tajiri Ya Siku, Mafuta Na Posho Zao, Wacha Traffic Barabarani Na DC Makonda Analijua Hilo!!! Kila La Kheri Kwao, Ila Hilo La WAALIMU Kusafiri Bure Ktk. Madaladala, Lina Changamoto Lukuki!!!
 
Huyu bwanamdogo ni jipu toka kitambo! Maamuzi mengine yafaa kuwa universal; k'ndoni siyo nchi, nawaunga baadh ya wadau hapo juu kwamba tatizo LA mwalimu ni zaid ya hiyo nauli!
Me ni mwalimu pia, nachoona hapo ni siasa kwenye mambo ya msingi! Maamuzu hayo hayajalenga kumsaidia mwlm was nchi hii Bali kumdhalilisha na kumfanya awe inferior. Yawezekanaje mwanafunzi anaelipa 200 akeshe kituoni na mwalm apande bure tukiamini atawahi kazini? Me naona anatutekenya walimu huku anacheka yeye!!!
Nasubir nione matokeo!
 
Kama watatengenzewa kitambulisho ambacho kinawekeka mfukoni au kwenye handbags sioni Kama kutakuwa na manyanyaso mana mwalim ataingia kwenye Gari bila hata kujulikana Kama ni mwalim ila wakat wa konda anadai chake ndo pale anaonyeshwa kitambulisho, pia nafkiri iwekwe sheria kali kwa konda yoyote atakae mnyanyasa mwalim.mbona hatujawah kuskia wanajeshi wananyanyasika kwenye madaladala? Hii nchi sheria zikisimamiwa vizuri kila mtu atakuwa na adabu na hata mwanafunzi anaweza kusafiri bure tuache ujinga ujinga
 
Tatizo la kufanya siasa kwenye maslai ya taifa ni upumbavu walimu shida yao sio kusafiri bure walimu wanaitaji mishara mizuri kulipwa malimbikizo yao ya madeni ikiwezekana wasamehewe kodi kwenye kuingiza vyombo ya usafiri hili sio kwa walimu tu wafanyakazi wote Wa taifa wanaumuhimu kuboresha mazingira ya kazi nauli bure ni swala la wanafunzi ambao ni wategemezi ndio ingekuwa Na maana huu uzalilishaji Wa walimu upingwe Na walimu wenyewe
 
Back
Top Bottom