Walimu 40 waenda likizo kwa kukosa mishahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu 40 waenda likizo kwa kukosa mishahara

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by VIKWAZO, May 23, 2011.

 1. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  HALMASHAURI ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa imekubali walimu wake 40 kwenda likizo baada ya kushindwa kuwalipa walimu wapya 40 wa shule za sekondari za Serikali zaidi ya Sh milioni 60.

  Hizo ni fedha za malimbikizo ya mishahara yao kwa miezi minne iliyopita wanayoidai manispaa hiyo.

  Tayari walimu hao wameuomba uongozi wa manispaa hiyo kuwaruhusu kurudi nyumbani na kwamba watakuwa tayari kurudi pindi halmashauri itakapokuwa na uwezo kifedha.

  Walimu hao ambao wanatoka mikoa mbalimbali nchini wanadai kuwa hawajalipwa mishahara yao tangu mwezi Januari mwaka huu walipoajiriwa na halmashauri hiyo na kuanza kazi kwenye vituo vyao vipya.

  Kwa mujibu wa walimu hao ambao walikuwa wamekusanyika kwenye ofisi za halmashauri hiyo jana mchana, kwamba Kaimu Mkurugenzi James Biseko amewataka kila mmoja wao amwandikie barua Mkuu wake wa Shule ya kuomba ruhusa kurudi walikotoka kwa kuwa
  halmashauri hiyo haina uwezo wa kuwalipa mishahara yao wanayodai kwa sasa.

  “Tangu halmashauri hii ituajiri Januari mwaka huu hadi hii leo hatujalipwa mishahara yetu. Leo (jana) tumekutana na Kaimu Mkurugenzi huyo wa Manispaa hapa ofisini kwake tukampatia mapendekezo yetu mawili,......watulipe malimbikizo ya mishahara yetu yote ya miezi minne tunayodai, lakini amedai kuwa hilo haliwezekani kwa kuwa eti halmashauri haina pesa ya kutulipa.

  "Basi tukamwambia (Kaimu Mkurugenzi) kwa kuwa hana pesa za kutulipa mishahara yetu yote kwa sasa atuwezeshe na atupe ruhusa turudi kwetu tulikotoka hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kutulipa ...ndipo Kaimu Mkurugenzi huyo alipokubali kutupatia ruksa hiyo ila kwa sharti kuwa kila mmoja wetu aandike barua yake binafsi akiomba ruhusa kwa Mkuu wa Shule tunakofundisha,” alisema mmoja wa walimu hao aliyejitambulisha kama Clever Moses.

  Kwa mujibu wa walimu hao wamekataa kuendelea kukopeshwa kiasi cha Sh 100,000 na Manispaa hiyo, ili wajikimu kimaisha hadi pale itakapokuwa na uwezo wa kuwalipa malimbikizo hayo ya mishahara yao wanayodai.

  “Tumekuja hapa kwa hiari yetu kama wahitimu wa Chuo Kikuu ngazi ya mshahara kwa mwezi ni Sh 400,000, sisi tumeajiriwa na halmashauri hii na tayari tumeanza kufundisha kwenye vituo vyetu vipya vya kazi tangu Januari mwaka huu hadi leo hii lakini hatuna mshahara.

  “Maisha kwetu ni magumu tuna madeni lukuki, ikiwemo malipo ya kodi la pango… huku tukiwa hatarini kufukuzwa kwenye nyumba ambazo tumepanga,” alisema Fadhili Sanga, mmoja wa walimu hao wapya.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sumbawanga, James Biseko alikiri kuwa halmashauri hiyo haina uwezo wa kifedha kwa sasa wa kulipa malimbikizo hayo ya mishahara ya walimu hao wanayodai.

  "Ni kweli hawa walimu ni waajiriwa wetu tangu Januari mwaka huu....tumekuwa tukiwakopesha Sh 100,000- siku zilizopita ili wajikimu, lakini mpaka sasa hatuna hiyo pesa ya
  kuwalipa. Sasa kama hatuna mie nifanyeje sina la kufanya....mshahara wa mwalimu mpya kwa mwezi baada ya makato yote ni Sh 380,000.

  habari leo

  MAONI: ni lini serikali itakili kufulia na kupunguza matumizi yake ili kuleta unafuu kidogo kwa wafanyakazi wake wa chini walau kuwalipa mishahara
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,512
  Trophy Points: 280
  Zitto aliongea na Mkulo akajibu niniii?????????
  we Tanzanians voted for ccm les than a year ago huh!!

  are we stupid? -- disscus in essay form
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu tutashuhudia mengi.
  Rais wa Malawi alipoenda kwenye mkutano NY aliamua kutumia usafiri wa daraja la kawaida economy kwa sababu ya matatizo ya uchumi wa nchi yake, lakini viongozi wetu pamoja na shinda ya kuishiwa pesa naona misafara ya viongozi haiashirii tahadhari yo yote juu ya kubana matumizi.

  Hakika atakayefuata kushika madaraka nchi hii kama ni chama cha upinzani kitashuhudia mashelve matupu na safe tupu.
   
 4. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  duh kawaida yao afu kwa nini mbuzi wa kafara awe mwalimu hela ya kulipana posho ipo lkn mwalimu hamna na sio huko tu sehemu nyingi walimu wanakopwa tu
   
 5. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo!
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Yeye huyo Kaimu Mkurugenzi naye hajalipwa miezi minne?
   
 7. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Si huwa wanasema kuna upungufu mkubwa wa walimu?
   
 8. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Bado serikali na Waziri wake wa fedha itaknusha!!
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Wananchi wa rukwa,kigoma,mtwara,singida,lindi.pemba,songea mnapaswa muelewe kuwa nyie hampo tanzania.serikali haioni umuhimu wa mikoa yetu kupata huduma muhimu na maendeleo kwa ujumla.milioni 60 zinakosekana lakini kukitokea kitu cha manunuzi kama gari,haraka haraka kwa muhindi wa toyota zinapelekwa 280milioni.
   
 10. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  wao wanaishi hotelini,
  sasa ili ni anguko la kielimu pia maana hao wanafunzi tarehe za mitihani ziko pale pale
  na hakuna wa kuwafundisha, kwa nini wasipaki mashangingi na kutumia daladala
   
Loading...